Wateja wa benki Barclay walalamika wizi ATM

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WATEJA wa Benki ya Barclays wamelalamika kuwa fedha zao zinaibwa pindi wanapotumia huduma ya kuchukua fedha kwenye akaunti kwa huduma ya mashine kupitia kadi za Visa za Benki ya Biashara ya Taifa (NBC).

Uongozi wa Barclays umekiri kuwepo na madai hayo na kwamba unayafanyia uchunguzi na utakapokamilika, watatoa taarifa rasmi. Mmoja wa wateja hao, Giovanni Meleki, alilieleza Mwananchi kwamba tayari ameibiwa Sh 400,000 kutoka kwenye akaunti yake ndani ya benki ya Barclays.

Pamoja na mteja huyo, mteja mwingine ambaye hakutaka jina lake liandikwe alisema fedha zake zilichukuliwa kupitia mtandao huohuo kupitia tawi la Barclys Azikiwe.
Alisema uongozi wa Benki hiyo unalifahamu fika suala hilo na kwamba wameahidi kurudisha fedha hizo ingawa mpaka sasa hawajafanya hivyo.

Alisema mpaka sasa zaidi ya Sh 3.4 milioni zimeibwa na kwamba katika tawi hilo wapo watu wengi wanaolalamika.
Kwa upande wake Meleki ambaye ni mwanafunzi katika Chuo Cha Ustawi wa Jamii, Dar es salaam, alisema aligundua upotevu huo Novemba 15 mwaka jana baada ya kupata taarifa ya mzunguko wa akaunti yake (bank statement) ambapo aliwasilisha malalamiko kwa Meneja wa benki hiyo tawi la Buguruni Malapa alipofungulia akaunti yake.

Meleki alisema Novemba 1, 2010 alichukua Sh 200,000 tu kwa Visa cardi yake ya Benki ya NBC kupitia Benki ya Barclays tawi la Mbagala na taarifa ya akaunti yake aliyopata Novemba 15, 2010 ilioonyesha kuwa siku hiyo alichukua kiasi hicho cha fedha kwa awamu tatu.

“Siku hiyo nilikuwa nakwenda Lindi, nikachukua Sh 200,000 kwenye ATM mashine ya Mbagala,niliporejea Dar es Salaam nikataka kuchukua hela nikashangaa kuambiwa sina fedha kwenye akaunti, nikaenda kuomba bank statement, ndipo nikagundua Sh 400,000 zilichukuliwa siku hiyo hiyo,”Meleki alieleza.

Alisema mpaka sasa hajarejeshewa kiasi chake cha fedha kilichochotwa kwenye akaunti yake hiyo ingawa mwanzoni mwa wiki hii alielezwa arudi ofisini hapo baada ya miezi mitatu ili afahamu hatua iliyochukuliwa.

Mkuu wa kitengo cha Uhusiano wa Barclays, Kati Kerege, alipoulizwa na Mwananchi alisema hawawezi kuzungumzia malalamiko hayo kwa kina kwa sababu bado yanafanyiwa uchunguzwi.

“Malalamiko hayo bado yanafanyiwa uchunguzi, hatuwezi kuyazungumzia kwa kina ila tunashauri wateja watumie kadi za kuchukulia fedha za kwetu kwa sababu ni rahisi kuzidhibiti,”alisema Kerege. Hata hivyo, alipohojiwa uchunguzi utakamilika lini alisema haijafahamika kwa sababu ni tatizo kubwa ambalo linahusisha benki na ofisi nyingine ikiwemo ya Visa, ingawa wanafanya kila linalowezekana kuukamilisha mapema.

Katika ofisi za benki ya NBC, Mwananchi lilielezwa na ofisa wa mapokezi kwamba ofisa wa uhusiano ambaye angeweza kutoa taarifa hizo yupo likizo mpaka Januari 10, mwaka huu. Mwisho.
 
Back
Top Bottom