Watawala washindwa kufuata nyayo za Simba wa Afrika!

kisugujira

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
773
195
WanaJF,

Kama Nyerere na Mandela waliweza kuleta matumaini, upendo na usawa pale palipokuwa na chuki na unyonyaji, na kuleta nuru pale palipokuwa na giza, kwa nini watawala wengi wa sasa katika Afrika wanashindwa kufanya hivyo?

Leo
ikiwa ni siku ya kukumbuka siku nchi yetu ilipopata uhuru 9/12/1961 toka katika utawala dharimu wa kikoloni wa Mwingereza, ni siku ambayo haiwezi kukumbukwa bila ya kumkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye kwa pamoja na viongozi wengine waadilifu wa TANU na wananchi walishirikiana katika kupigania na kuongoza harakati za kumwondoa mkoloni na kupata uhuru.

Nini kifanyike ili kudumisha na kuendeleza kwa vitendo kwa manufaa ya wananchi yale yaliyofanywa na Simba hawa wa Afrika Nyerere, Mandela, Kwame Nkurumah, Lumumba na wengine wengi waliotangulia mbele ya haki katika kupigania uhuru, haki na usawa katika bara la Afrika?

Daima tutawakumbuka Simba wa Afrika!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom