Watawala: Mbegu hii mnayoipanda, itawagharimu.

sir j

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
317
212
Kumetokea wimbi la watawala wetu kupishana kauli na huku wakiwadanganya watanzania, hususani vijana ambao wanasubiri ajira. Mmoja akasema mwezi may wangeajiri watumishi, lakini cha kushangaza ni kimya mpaka leo. Mwingine akasema, ooh ajira zitatoka mapema mwaka huu. Mbaya zaidi mkubwa kabisa, yeye akasema itakuwa ni mwezi mmoja unusu na haitazidi miezi miwili mara baada ya zoezi la uhakiki kukamilika, lakini cha kushangaza leo ni takribani miezi minane, hakuna jipya lolote, ni uongo ule ule tuu.

Lakini cha kushangaza, hakuna mtawala hata mmoja aliyetoka hadharani na kuwataka RADHI watanzania kwa kuwadanganya, wanaona kudanganya ni sawa tuu.

Ingetokea hukumu ya moto ikawa leo......Mwenyezi Mungu angeanza na kuwaadhibu watawala wa Tz kwa dhambi kubwa ya UONGO. Sio mkulu wala nani,,,,wote ni wale wale,......
Anyway......watanzania tushikamane na tuungane ili kuishinikiza siri kali, kutolea ufafanuzi kwa kuwapotezea vijana muda wao mwingi (wa kuwa masomoni & mtaani), na pia kuwaomba radhi watanzania kwa uongo mwingi ambao umesemwa kwao.

Hii haikubaliki kabisa, watawala wanatengeneza taifa la watu waongo tuu,,,,kama viongozi wakuu wa nchi wanakuwa waongo namna hiyo, tena wakiwadanganya raia wao bila kupepesa macho wala kuwa na japo lepe na aibu....then tutegemee nini kwa raia....wao si ndo UONGO ndio utakuwa ni ukweli wao..!!!!

Mbadirike viongozi wa nji hiii...........wacheni uongo.............uongo ni dhambi kubwa saaaana.......na kwa hakika dhambi hii mnayoipanda, itawagharimu sana. Pia italipeleka taifa hili pabaya mno, maana mbegu mliyoipanda/mnayoipanda ni mbegu ya uharibifu, mtajuta........kwani hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Days are coming.

Rai yangu: Viongozi, muwaambie watanzania ukweli na sio blaa blaah tu (uongo), maana ukweli humweka mtu huru. Jitokezeni hadhari kuomba radhi umma wa watanzania.

John 8:31
" tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru"
 
Back
Top Bottom