Watatu waongezwa kuandaa ripoti ya ESCROW

Watatu waongezwa kuandaa ripoti ya ESCROW

.....updates

Na Ally Kesi mbunge wa Nkasi pia ameongezwa katika hiyo kamati.
 
Kangi Lugola alisema kuwa "Kama ikibainika kuwa fedha zile ni za Umma hatakuwa na msamaha hata kama Prof. Muhongo atakuwa anahusika" kwa hiyo si kwamba alisema kuwa fedha si Umma tu, no, aliongezea hayo maneno.

Kama yupo Lugola Watanzania tuondoe wasiwasi. Tuikubali taarifa yoyote itakayotolewa. Wakienda kinyume na atakachokiona kwenye ripoti ya cag atawaumbua ndani ya bunge.
 
Kangi lugola aliwai kusema Hela sio za Umma.
 
Mbona mahakama imezuia kuzungumzia report hiyo?
 
Hapo namba mbili na tatu wamepandikizwa kuua msimamo, kwani namba mbili na tatu walishasema wazi kuwa msimamo wao ni kuwa fefha hizo SI ZA UMMA. Kama ni kweli wamewaongeza hao tusitegemee jipya.

Zitto nae ni mpigaji rf Maswi, lugola alisema fedha sio za umma. hapo hakuna jipya.
 
Kamati ya Zitto kabwe imeona umuhimu wa kuazima majembe matatu kusaidia katika kuandaa ripoti ya kuwasilisha bungeni kutoka katika taarifa ya CAG iliyowasirishwa ktk kamati ya PAC....Majembe hayo ni:

1. Luhaga Joelson Mpina-Mbunge wa Kisesa(CCM)-Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya uchumi viwanda na biashara.

2. Kangi A.Lugola-Mbunge wa Jimbo la Mwibala (CCM)

3. Hamis Kigwangala-Mbunge wa Jimbo la Nzega(CCM) mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya maendeleo ya jamii.

Kwa watu hawa makini kiongezwa katika panel ya kufukunyua Mafisadi watatokea wapi?

Hapo Mtanzania ni Kagi Lugola peke yake hao wawili ni wapiga filimbi wa mfalme hamna kitu hapo.
 
2nataka ripoti ya CAG,sio wao watengeneze ya kwao!ili iweje
 
Hakuna kitu hapo na tusitarajie lolote la maana,wote waaminifu kwa magamba!
 
Kamati iwaite na kuwahoji wakionekana na hatia watiwe kwenye karandinga wakajisaidie kwenye debe.
 
Kamati ya Zitto kabwe imeona umuhimu wa kuazima majembe matatu kusaidia katika kuandaa ripoti ya kuwasilisha bungeni kutoka katika taarifa ya CAG iliyowasirishwa ktk kamati ya PAC....Majembe hayo ni:

1. Luhaga Joelson Mpina-Mbunge wa Kisesa(CCM)-Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya uchumi viwanda na biashara.

2. Kangi A.Lugola-Mbunge wa Jimbo la Mwibala (CCM)

3. Hamis Kigwangala-Mbunge wa Jimbo la Nzega(CCM) mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya maendeleo ya jamii.

Kwa watu hawa makini kiongezwa katika panel ya kufukunyua Mafisadi watatokea wapi?

Zitto kama M/kiti wa PAC hana madaraka ya kuongeza hata mbunge mmoja kwenye kamati yake.

Kama Zitto ameona kuna haja ya kuongeza wabunge kwenye kamati ya PAC, basi ametuma maombi kwa spekear wa bunge la JMT.

Kama kweli wajumbe hao wameongezwa kwenye kamati ya PAC kufuatilia suala la report ya CAG na uchunguzi wa TAKUKURU wa Escrow basi watakuwa wameongezwa/chaguliwa na spekear Anne Makinda.
 
Back
Top Bottom