Watapeliwa ubungo..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watapeliwa ubungo.....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Boss, Dec 26, 2009.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Abiria 200 watapeliwa Ubungo, walikata tikiti za mabasi yasiyokuwepo[​IMG]Minael Msuya na Victoria Kombe

  ABIRIA wapatao 200 waliotaka kusafiri kati ya Dar es Salaam na Mwanza, wamejikuta katika wakati mgumi baada ya kutapeliwa nauli zao.

  Abiria hao, ambao ilikuwa wafanye safari yao jana asubuhi, walipigwa na butwaa baada ya kutafuta mabasi yaliyoandikwa katika tiketi zao na kuyakosa.

  Tiketi za abiria hao, ambao walielezwa kuwa wangetumiwa mabasi mawili tofauti, zinaonyesha kuwa wangesafiri kwa mabasi yanayoitwa Shatco na Scanlink.

  Mwananchi ilishuhudia abiria hao wakihangaika kwa muda mrefu bila kuona mabasi hayo, kitu kilichowafanya wapandwe na hasira na kuanza kuwasaka waliowauzia tiketi za usafiri.

  Walifanikiwa kumkamata mkatatiketi waliyemtaja kwa jina la Mahimbo na kumpeleka kituo kidogo cha polisi cha Ubungo ili kuweza kupata mustakabali wa safari yao na wakashauriwa wafungue mashtaka na polisi, lakini walikataa.

  “Sisi tunachotaka ni kusafiri na sio kufungua mashtaka, kwa sababu alitukatia tiketi jana (juzi) za kwenda Mwanza na kutuambia kuwa leo (jana) tutaanza safari mapema asubuhi,” alisema mmoja wa abiria wa basi la Shatco, Kate Revocatus.

  Revocatus aliongeza kusema:“Haiwezekani kumfungulia mtu mashtaka wakati sisi tunataka kusafiri, kwanza tuna wagonjwa na watoto... hapa tutakaa mpaka saa ngapi, turudishiwe pesa zetu ndio polisi wamchukulie sheria zao.”

  Naye abiria wa Scanlink, Happy Edward alisema kwa kitendo hicho serikali inatakiwa kuwafikiria katika kufanikisha safari hiyo, na baadaye wafungue mashtaka dhidi ya mkatatiketi huyo ili waweze kurudishiwa fedha zao.

  Naye Inspekta Bombwe Kizyalla alithibitisha kukamatwa kwa mkata tiketi huyo na kusema atachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwakatia abiria tiketi za kitapeli.

  “Kesi ya aliyeuza tiketi feki ni moja... kwa sababu yuko chini ya ulinzi, tutahakikisha tunamshughulikia ipasavyo na kuwa mfano mzuri kwa wengine,” alisema Inspekta Kizyalla.

  Makampuni mbalimbali ya usafirishaji wa abiria yameweka ofisi zao za kukatia tiketi nje ya majengo ya Kituo cha Mabasi cha Ubungo (UBT), lakini mawakala wa makampuni hayo wamekuwa wakifuata wasafiri nje ya maeneo ya kituo hicho kubembeleza watu watumie mabasi yao, hali inayojenga mazingira mazuri ya utapeli.

  Mawakala hao husababisha abiria kukata tiketi za mabasi wasiyoyajua na hata kutofika ofisini. Mawakala hao wamewahi kupigwa marufuku mara kadhaa, lakini hali inaonekana ni ngumu kuwadhibiti.

  Naye msimamizi wa zoezi la kuyasaka magari yanayokiuka masharti ya leseni za usafirishaji, Said Kadeem alisema ugumu wa zoezi hilo unasababishwa na abiria kwa sababu hawataki kushirikiana nao katika suala zima la kusafiri kwa nauli halali zilizopangwa.

  “Zoezi hili linakuwa gumu kwa sababu abiria wenyewe wamesharidhika kusafiri kwa bei yoyote wanayoambiwa, kulingana na hali ya upungufu wa mabasi na hata hivyo ukiwauliza wanakuambia tunataka kusafiri hatuwezi kusumbuana na wenye mabasi yao,” alisema Kadeem.
  Mbali na mabasi ya Shatco na Scanlink ambayo yalikuwa yamekatiwa tiketi za kwenda Mwanza, basi dogo aina ya Toyota Coastal lilikamatwa kwa kupakia abiria waendao Kilimanjaro likiwa halina kibali cha safari hiyo.
  Pamoja na kukamatwa kwa gari hilo dereva na kondakta walitoweka, hatimaye abiria kuanza kuhaha huku wakidai kuwa wamelipishwa nauli lakini hawajakatiwa tiketi.
  “Mimi naelekea Korogwe nimelipa Sh 20,000, lakini bado hatujapewa tiketi sasa sijui itakuaje... dereva mwenyewe kishatoroka” alilalama abiria huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mudhihir Salim.
  Kufuatia hali ya kujirudia kwa makosa ya mara kwa mara ambayo yanafuatiliwa na kampuni ya majembe pamoja na kikosi cha usalama barabarani, meneja mawasiliano ya umma wa Simatra, David Mziray aliliambia gazeti hili kuwa watazingatia sheria zilizowekwa na kuboresha ushirikiano na wadau.

  Wakati huohuo Monica Petro,Penina Malundo na Kalonga Kasati hali ya wafanyabiashara jijini Dar es Salaam, imeendelea kuwa nzuri katika kipindi cha maandalizi ya sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

  Wakizungumza na Mwananchi, wafanyabiashara wa masoko mbalimbali wamesema kuwa hali ya biashara imekuwa nzuri kutokana na wanunuzi kuwa wengi katika kipindi hiki. Mwananchi ilishuhudia bei za bidhaa mbalimbali zikiwa zimepanda. Nyama ilikuwa ikiuzwa Sh5,000, mchele kilo Sh1,400 mpaka Sh1,500 na mkungu wa ndizi Sh16,000 hadi Sh20,000.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Vipindi vya sikukuu umakini wa ziada inatakiwa, hasa pale Ubungo stendi...

  Wale wauzaji wanajua vyema kwamba watakuja abiria ambao ndo mara yao ya pili kupanda basi, ukiacha safari ya kwanza ya kuingia Dar...Hivyo wanamake use of the chance!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kwani lazima kusafiri kila sikukuu?????
  ni kujitakia tu huku.......
   
Loading...