Watapangiwa kazi nyingine - wanalipwa mishahara huku wakisubiri?

gogomoka

Senior Member
Jun 13, 2008
124
89
Wanabodi,

Nimejiuliza hili swali bila majibu - hawa wanaondolewa na Mheshimiwa kisha wanasema watapangiwa kazi nyingine.
1. Je wanaendelea kulipwa mishahara?
2. Mishahara kwa kiwango kipi cha zamani walichofikia au?
3. Wanaenda kazini - wanaripoti kwa nani?

Mh JPM anajaribu kupunguza gharama za uendeshaji, sasa hawa ambao watapangiwa kazi nyingine halafu wamekaa inamaanisha bado ni waajiriwa halali wa serikali, hivyo ni wanastahili malipo. Je, ni haki walipwe mishahara bila kufanya kazi? NB: Hawa sio wafanyakazi hewa - ni watu wanafahamika. Tunaposema tunafanya maamuzi ya kupunguza matumizi inabidi tuache hii tabia ya kusema watapangiwa "kazi nyingine" , kwa nini hao hao wapangiwe kazi nyingine wakati Watanzania wengi hawana kazi wanazitafuta. Hizo kazi nyingine kama zipo basi zitangazwe ili wote tuziombe. Hakuna mwenye hati miliki ya kazi. Hao waliotolewa wameshindwa sasa kwa nini wapangiwe nyingine? Tunatunza failures!!!

Karibuni tujadili.
 
Hiyo ni kauli ya kisiasa tu hakuna kaz hapo ni kukaa tu zaid mtu ujiongeze upige tu mishe zako...chukulia mfano sefue atapangiwa kaz gan?si kumshusha cheo huko
 
Hii Ndio sirikali.
Fuatilia sheria za utumishi wa umma zinasemaje kwa mtumishi aliesimamiswa kazi.
Nini anapata na nini anakosa. Utaelewa.
 
Back
Top Bottom