kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,428
- 13,936
Rais Magufuli anafanya mabadiliko kila mara ya kuwaondoa watumishi wasiokuwa waaminifu kwenye nafasi zao angalau kurudisha heshima nchini kiuchumi na kimaadili. Lakini kuna jambo moja ambalo lazima tumfahamishe Rais wetu kuhusu watanzania, na jambo hilo sio lingine zaidi ya kumwambia kuwa watanzania wengi kama sio wote ni wezi. Ushahidi wa hili ni kwamba, mishahara ya watumishi wengi kiuhalisia haitoshi kwao kutumia japo kwa siku 10, lakini wao wanafika hadi tarehe 30 pamoja na kulipa kodi zote, sadaka, kunywa pombe, kusaidia ndugu zao vijijini, kujenga vijumba, kununua magari, kusomesha watoto shule binafsi, na kuchangia harusi. Hii ina maana kuwa kuna mahali pengine wanapata pato la ziada mbali na kamshahara wanayopewa na waajiri wao. Inawezekana kabisa kuwa watu wako ama wanaiba pesa, muda au wanapokea rushwa za aina mbalimbali ili kufidia mapungufu yao ya kipato. Hata kama utaongeza mishahara ya watumishi ni kazi bure kama ndugu zao kijijini hawana kipato. Ndugu hawa watamzonga mtumishi huyo ambae ni mtoto/mjukuu/mpwa/dada/kaka/mkwe/ shemeji/shangazi au mjomba wao kwa shida zao mbalimbali. Hivyo mtumishi huyo lazima ataingia majaribuni tu hata kama hapendi.
Ushauri wangu kwako ni 1. kuangalia upya mishahara ya watumishi wako pamoja na kodi mbalimbali za watumishi ili wawe na uhakika wa kuwafikisha siku 30,
2. kuinua kipato cha watanzania wote hasa vijijini ili wapunguze utegemezi kwa watumishi. Fufua plantations, ranch, viwanda ili watu wapate ajira huko,
3. Wapatie watumishi nyumba, ushafiri, canteens, uniforms ili kuwapunguzia ughali wa maisha na vishawishi.
Vinginevyo kila siku utabadilisha maofisa wako bila mafanikio. Ofisa aliyebadilishiwa ofisi itamchukuwa miezi 6 hadi mwaka 1 kuweza kujua nini cha kufanya kwenye ofisi yake mpya. Lakini hakuna mtumishi ambaye hajazunguukwa na pressure za extended families na mahitaji yake mengine. Waaminifu wapo lakini majaribu kwao ni mengi mno. Wapiga dili wanautumia udhaifu huu wa watumishi wako kufanikisha mipango yao ovu. Usiwabadilishe bali wakemee hapo hapo walipo