Watanzania wenye fedha nje waanza kuchunguzwa

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Serikali yetu itakuwa inaongoza duniani kwa kutwanga maji kwenye kinu. Hivi mmeona wapi serikali ikawa na mawaziri 60? wote hao wana hitaji ulinzi, magari, walipiwe nyumba etc etc

sasa hebu niambieni waingereza washarudisha kiasi gani kilichoibiwa Kenya na Moi? au waswisi wamerudisha kiasi gani kilichoibiwa na Abacha?

Hivi leo benki gani duniani itakubali hao TUKURU kufanya upekuzi?

Je watawala kama akina Amani Karume nao itabidi wajieleze kuhusu zile nyumba zao pale Kesington na Chelsea achilia mbali zile za kule Palm Beach?




 
GT,
1. Wizi ni kitu mbaya- ila heri ya wizi kuiba na kujenga viwanda na kufungua mashamba hapa hapa watu wapate kazi- kuliko kupeleka huko Ulaya!

2. Uwezo wa TAKURURU ni finyusana- sina data how much in monetary terms has been saved by them. Sasa kama wameshindwa hata kigogo mmoja hapa home kumtia ndani- ndo wapi wataweza UK au Uswisi?

Mimi naona kama ni maneno tu ya kufurahisha kisiasa- hakuna kitu hapo!
 
Nadhani to be more realistic, uchunguzi ungeanzia ndani kwanza kabla ya kukurupukia kwenye nchi za nje. Bado tunaisubiri report ya BOT, au ni kutaka tu kudistract attention yetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…