mwanazuoni mgeni
JF-Expert Member
- Sep 11, 2016
- 1,944
- 1,715
Habari wana JF,
Katika jamii nyingi tunazoishi maisha ya watanzania wengi ni level ya kati na ya chini na pia asilimia kubwa ya watanzania hawana elimu ya kutosha kuhusiana na maswala ya afya hivyo basi inapelekea familia nyingi kula chakula kulingana na hela iliyopo na chakushangaza zaidi unakuta kuna aina flani ya mlo ndo unatumika Mara kwa Mara.
Lakini pia ukiangalia upande wa pili hili linasababishwa na umasikini na ukosevu wa elimu kuhusiana na maswala ya afya watu wengi hawajui mlo kamili ni mchanganyiko wa vyakula gani, ninachokiamini ni kwamba hata mtanzania awe wa hali ya chini akiamua kujipangia vizuri mpangilio wa vyakula ataweza, tatizo kubwa ni elimu ya kula mlo kamili watu wengi hawana.
Nimalizie kwa kusema: Kuwa na afya njema inahusiana sana na mfumo wa maisha kwa ujumla pamoja na mlo kamili.