Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,948
Tanzania na wananchi wa Tanzania, ni wenye bahati mbaya kabisa katika ulimwengu huu.
Watanzania (Watanganyika na Wazanzibari) wamepitia kwenye mateso ya utumwa wa mwarabu. Wakati huo mwarabu ndiye aliyeandaa taratibu zake za namna gani akusanye watumwa, awauze kwa namna gani na wapi, sultani apewe mgao kiasi gani kutokana na biashara hiyo ya binadamu.
Biashara ya utumwa ilipokomeshwa, Mtanganyika akatoka kwenye utumwa wa mwarabu, akaingizwa kwenye ukoloni wa Mjerumani. Mjerumani ndiye alitengeneza taratibu zake za namna atakavyomtawala huyu Mtanganyika. Mtanganyika hakushirikishwa kwa namna yoyote katika taratibu za kutawaliwa.
Akaja Mwingereza, yeye akaitwa ni mwangalizi, siyo mkoloni. Lakini naye hakuwa na tofauti kubwa na Mjerumani.
Baada ya uhuru, hali ya Mtanzania haikubadilika sana. Mabadiliko makubwa ilikuwa sasa badala ya kutawaliwa kwa kanuni zilizotengenezwa na mzungu sasa alitawaliwa kwa kanuni zilizotengenezwa na weusi wenzake wachache kupitia uwakilishi mdogo.
Mwaka 1977, wajanja wachache tena, bila ya kushirikisha umma, Watanzania weusi wenzetu, wakaandaa utaratibu wa kuwatawala Watanzania wote.
Kelele za wananchi hazijawahi kukoma juu ya dhuluma hii ya watawala dhidi ya umma.
Utawala wa Kikwete, ulionekana kusikia kilio hiki cha wananchi. Akaandaa Tume ya katiba mpya iliyoongozwa na mzee mwenye hekima sana, Jaji Warioba. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanganyika, Zanzibar na Tanzania, wananchi wa Tanzania, kupitia ushirikishwaji mpana, wakahusishwa katika kutoa maoni juu ya katiba yao itakayowaelekeza watawala namna ya kuongoza nchi. Mabadiliko haya ya wananchi kuwaandalia watawala utaratibu wa kuwaongoza, badala ya watawala kuwaandalia wananchi utaratibu wa kuwatawala, watawala hawakuupenda. Walifanya kila hila, mchakato ukazimwa.
Utawala wa awamu ya 6 ndiyo ukafanya udanganyifu mkubwa dhidi ya umma. Wakati maoni ya wananchi yalikwishakusanywa kwa ushirikishwaji mkubwa kabisa, awamu ya 6 ikaja na hadaa ya vikamati visivyo na vichwa wala miguu, visivyotambulika kisheria, na kisha hadithi zinazogeuzwa geuzwa kila siku. Lengo ni kuhakikisha WATANZANIA WANAENDELEA KUWA CHINI YA UKOLONI MPYA WA WATANZANIA WACHACHE.
Kimsingi, ukoloni ni pale wanaotawaliwa hawawi na kauli yoyote juu ya namna wanavyotaka watawaliwe.
Kwa tafsiri hiyo, watanzania ni sawa wapo kwenye nusu ukoloni maana mifumo inayowatawala, wao wananchi hawajawahi kujumuishwa katika ushirikishwaji mpana. Tunaweza kuuita ni nusu ukoloni, kwa sababu kuna ushirikishwaji mdogo sana kupitia wabunge waliopatikana kwa taratibu zilizotengenezwa na watawala.
Je, Watanzania wataendelea kuwa chini ya huu ukoloni nusu mpaka lini? Maana kwa hakika kila mara wamekuwa watu wanaobadilishiwa kutoka ukoloni wa aina moja kwenda mwingine, lakini hawajawahi kuondokana na kongwa la ukoloni kwa 100%. Katiba mpya iliyosheheni maoni ya wananchi wa makundi yote nchini, ndiyo ingekuwa uhuru kamili wa Mtamzania, lakini hili, kwa vitendo linapigwa vita kubwa na watawala ambao wanaifurahia nafasi yao ya kuwa wakoloni wapya wa sasa.