Watanzania wanne wafanyabiashara wauawa Msumbiji na majambazi kwa risasi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,689
55,662
Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara limethibitisha kupokea maiti nne za wafanyabiashara wa kitanzania waliouawa na majambazi nchini Msumbiji na kuporwa mali na fedha katika kijiji cha Mtoro wilaya ya Mtepwezi jimbo la Deboderobage.

Akithibitisha kupokelewa kwa maiti hizo kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Henrry Mwaibambe amesema watanzania hao walikuwa ni wafanyabiashara ya dhahabu na wamepigwa risasi wakiwa eneo la machimbo ya dhahabu.

Amesema baada ya uchunguzi wa maiti hizo kufanyika katika hospitali ya mkoa wa Ligula imethibitisha watanzania hao wameuawa kwa kupigwa risasi na vitu vyenye ncha kali.

Hata hivyo daktari mfawidhi wa hospitali ya Ligula Diksoni Saini hakutaka kuonyesha ushirikiano kwa waandishi na kudai hana taarifa za kupokelewa kwa maiti nne katika hospitali ya mkoa ya Ligula.

Wakizungumza kwa masikitiko jamaa na ndugu wa waliosafirisha maiti hizo kutoka Msumbiji wanaelezea mazingira ya vifo hivyo.

Maiti hizo zimepokelewa mkoani Mtwara na baada ya kukabidhiwa ndugu wa marehemu zilipelekwa katika msikiti wa Majengo kwa ajili ya kufanyiwa usafi na kusafirishwa kwa gari kuelekea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi.

Chanzo: ITV
 
Wafanyabiashara wanne wa Dhahabu wameuwawa kwa kupigwa risasi Msumbiji akiwemo ndugu yangu Salim Mfanga, R. I. P BROTHER, Inauma kwa kweli , KUENI MAKINI MNAOENDA MSUMBIJI SI SALAMA

Chanzo mimi mwenyewe na Radio One

Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara limethibitisha
kupokea maiti nne za wafanyabiashara wa
kitanzania waliouwa na majambazi nchini
Msumbiji na kuporwa mali na fedha katika kijiji
cha Mtoro wilaya ya Mtepwezi jimbo la
Deboderobage.
Akithibitisha kupokelewa kwa maiti hizo kamanda
wa polisi mkoa wa Mtwara Henrry Mwaibambe
amesema watanzania hao walikuwa ni
wafanyabiashara ya dhahabu na wamepigwa
risasi wakiwa eneo la machimbo ya dhahabu.
Amesema baada ya uchunguzi wa maiti hizo
kufanyika katika hospitali ya mkoa wa Ligula
imethibitisha watanzania hao wameuawa kwa
kupigwa risasi na vitu vyenye ncha kali.
Hata hivyo daktari mfawidhi wa hospitali ya
Ligula Diksoni Saini hakutaka kuonyesha
ushirikiano kwa waandishi na kudai hana taarifa
za kupokelewa kwa maiti nne katika hospitali ya
mkoa ya Ligula.
Wakizungumza kwa masikitiko jamaa na ndugu
wa waliosafirisha maiti hizo kutoka Msumbiji
wanaelezea mazingira ya vifo hivyo.
Maiti hizo zimepokelewa mkoani Mtwara na
baada ya kukabidhiwa ndugu wa marehemu
zilipelekwa katika msikiti wa Majengo kwa ajili ya
kufanyiwa usafi na kusafirishwa kwa gari
kuelekea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
mazishi.
 
Poleni sana mkuu. Mungu awapunguzie adhabu za kaburi Marehemu wote. Marehemu walikuwa ni wakazi wa Msumbiji au walienda kibiashara tu!?
 
Poleni sana wafiwa kwa kupoteza wapendwa wenu muhimu.

Ila chakusikitisha dhahabu tele wameiacha nyumbani huku wageni wakiifaidi. Tunahangaika sana watanzania wa hali ya chini kutafuta riziki ilihali watu wachache wanaishi kama wako peponi
 
R.I.P wote mliyofikwa na maut.

wengne kama mko salama endeleeni kupambana maisha hayataki lele mama. mungu ndio anapanga.
 
Dhahabu!!, walikuwa wanachimba?, wanunuzi? Wameporwa kiasi gani?, hii habari haijakamilika
 
Mmoja ni mwanamke anaitwa halima mwenyeji wa Tanga.wawili ni wapare ila majina yao siyakumbuki vizuli na mmoja ni mchimbaji pia simkumbuki jina.
 
katika nchi ambazo sifikirii kwenda ni Msumbiji, jamaa wana roho mbaya sana na wanatuchukia sana watz na ukizingatia malalamiko ya kunyanyaswa kwa watz serikali inajua toka zamani lakini hakuna hatua yoyote yanayochukua, inauna sn BTW R.I.P wahanga
 
Back
Top Bottom