Watanzania wanataka nchi ya aina gani?

Watanzania wanataka nchi ya aina gani?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,277
Reaction score
13,920
Bila kupindisha maneno nchi yetu kwasasa inakabiliwa na mabadiliko makubwa ya mfumo.

Mfumo wa zamani wa vyama vingi na demokrasia unaelekee kufa na kuja mfumo mpya kama wa Rwanda, Urusi na China.

Utawala wa Chama kimoja na mtu mmoja wa awapendaje. Huu mfumo wa aina yake unaonekanaga mzuri pale tu ukiwa na kiongozi mzuri mzalendo lakini ukipata kiongozi mbinafsi mmoja tu anaweza kubadilisha nchi na akawa mfalme na kuwapa Watoto wake madaraka.

Je, Tanzania tunataka maendeleo ya muda ambayo haturuhusiwi kuhoji chochote zaidi ya wale tu wanao support au tunapenda demokrasia ya muda mrefu ambayo pamoja na matatizo yake ni Watanzania wanachagua watu wenyewe wawapendao

Tatizo kubwa tulilonalo kwa sasa ni kuwa na waaandishi wa Habari ambao wamebobea kuunga mkono kila kitu badala ya kupigania uhuru. Wenye ushabiki kuliko hoja na wanaopenda vihoja kuliko kuwa makini.

Tatizo lingine kutokana na nchi yetu kuwa na vijana wadogo wengi zaidi ya 80% chini ya miaka 28 tumekuwa ni nchi ya malimbukeni wengi kwasababu hawa madogo bado wengi hata hawajui dunia inapoenda.

Tushishangae wahamasishaji wakubwa ni wasanii ambao wengi hata Form 6 hawajafika, wasanii wanao toboa masikio, pua na kupaka rangi nywele. Kwa kimsingi wasanii sio Maisha halisi ya hawa vijana na hata majina wa usanii sio yao na ni waigizaji. Lakini hawa ndiyo wanatumika kuomba kura.

Kwa sababu ya mapungufu yetu ya kuwa na vijana wengi wasio jua na tamaa kubwa ya madara kwa viongozi wetu wanaopenda kusifiwa Tanzania inalekea kwenye udikteta. Kibaya zaidi inaelekea wachache wanaojua kinachoendelea nao wanatafuta pesa ambayo imezidi kuwa ngumu.

Wapinzani wamekuwa wanapigwa risasi, kufunguliwa kesi na kufungiwa biashara na wale wasioelewa wamekuwa wanakejeli tu bila kujua yajayo.

Tatizo lingine Watanzania wengi hawajui wanataka Tanzania gani?
 
Tatizo kubwa ZAIDI NI UJINGA WATANZANIA WENGI NI WAJINGA SANA Hawaelewi kitu chochote. Hasa upande wa siasa.

Mfumo wa Elimu za chini hauruhisu wanafunzi kusoma Elimu ya siasa na uraia kwa mapana yake..

CCM wameua ELIMU makusudi kwa KULETA SHULE MBOVU NA MITAALA MIBOVU ILI KUTENGENEZA WAJINGA AMBAO NDIO MTAJI WAO KISIASA.

Elimu.
Elimu.
Elimu
 
Ukiangakia kwa juu juu utadhani Rwanda, China na Urusi zinafanana katika mifumo ya uongozi wa nchi lakini kuna tofauti kubwa sana za kimsingi. Rwanda imesimama katika nguzo inayoonekana kama imara lakini kwa maoni yangu ni nyembamba sana na fragile

Kama umewahi kufika Rwanda na ukatembea miji michache utagundua kua kuna silent tension hivi. Nchi ina amani, usalama na utulivu lakini unahisi kuna hofu iliyojificha miongoni mwa watu na kutokuridhika kusiko elezeka.

Nafikiria Rwanda ya bila PK kama itakua the same. Yeye ndio muhimili wa kila kitu kuanzia "amani na utulivu", chanzo cha sheria za nchi, ustawi wa kiuchumi na siasa za nchi. Kwangu mimi ki mfumo wa siasa na uongozi wa taifa kuna mfanano kati ya Pyongyang na Kigali. Atakapo ondoka yeye kwa sababu yoyote ni suala la kuomba Mungu kwakweli

China na Urusi vyenye nguvu ni vyama tawala, tena hasa China. Xi Ji Pin kawekwa pale kwa maslahi ya nchi kutokana na uwezo wake na jinsi anavyoipaisha China. Nawahakikishia akizingua ni suala la masaa tu wanamuweka pembeni. Lakini ustawi wa China chini yake kila mtu anaushuhudia ndani na nje ya mipaka yao

Urusi wao kuna umafia flani kwenye mifumo yao lakini lengo ni kulitumikia Taifa na kulifanya liwe kubwa. Ile kauli mbiu ya Trump ya 2016 wakati akiwania kuingia madarakani kwa mara ya kwanza ya "Make America Great Again" ina sadifu sana kwa Putin kwa namna alivyoitendea Urusi. Wamarekani na kelele zao zote za ubabe wa teknolojia waliwahi kulialia kua Urusi inaingilia kwenye chaguzi zao!!!!

Yote kwa yote sisi kama dunia ya tatu ili tupige hatua za maana kimaendeleo ya kweli tunahitaji kutengeneza taasisi zenye nguvu kwenye mifumo yetu na kuhakikisha zinaendeshwa na watu wenye uwezo. Lakini hata kama watabadilika katikati ya safari vyombo husika viwe na uwezo usiotetereka wa kuchukua hatua bila chuki wala upendeleo
 
Wenye Chakula hawana appetite (hamu ya kula) na wenye appetite hawana chakula. Wenye majumba ya kifahari wanakosa usingizi, na wenye usingizi wa kutosha hawana hata pakulala. Wagonjwa mahututi wanaomba uzima, wazima wa afya wanajiua. Wagumba wanalilia watoto, wasio wagumba wanatoa mimba na kutupa watoto chooni. Wenye mialiko mingi hawana nafasi ya kwenda na wenye nafasi hawana mialiko.

Wasio na kope wamejikubali kama walivyo, wenye kope wanavaa za bandia. Anayepewa upendo hauthamini asiyependwa analilia upendo.

Wenye amani wanaomba vita na kutishia machafuko, wenye vita wanalilia amani.

Mwenye nafasi ya kusoma na ada analipiwa hataki shule wala haitilii maanani, mwenye kiu ya kusoma hana ada.

Ni kama binadamu hajui anachokitaka hivyo hata akipata alichodhani anataka bado haridhiki kwani sicho hicho anachotafuta.

CHA KUSHANGAZA

1. Hicho unachokidharau Leo ndicho kilikuwa kinakuliza jana na kukunyima usingizi.

2. Hayo unayotafuta Leo pia kesho hayatakuwa na mashiko kwako.

MAISHA NI FUMBO LILILOSHEHENI VIFUMBO KAMA MFALME SULEIMAN ALIVYOSEMA " TUNAFUKUZA UPEPO" ambao hatutakaa tuukamate!!

SHUKURU KWA UHAI. VINGINE VYOTE VINATHAMANI USIPOKUWA NAVYO, UKIVIPATA THAMANI YAKE INAISHIA HAPO. HIVYO USIRUHUSU VIKAKUTAWALA

Jiulize!
Unadhani ni kitu gani ukikipata ndicho kitakupa utulivu wa moyo!!???

Ukilipata jibu, tufundishe nasi hapa Wana JF wenzako!!
 
Serikali ya CCM ya miaka 5 iliyopita imeiharibu nchi. Miaka 5 tena imeingia madarakani kwa uchafuzi mkubwa. Yajayo yanasikitisha.
 
Jiwe ameturudisha nyuma kama taifa kwa miaka 50. Kwa utopolo huu aliouanzisha hatutatoboa.
 
Tunataka tuwe na mfalme ,kama huyu Raisi na kwa vile bunge lote ni limeundwa na CCM itakuwa rahisi kubadilisha cheo badala ya Raisi awepo Mfalme na pia ufalme usitokane tena na CCM bali tutumie Kabila la Mheshimiwa magufuli ndio liwe linatoa wafalme.
Tutapendeza zaid kulivyo tulivyo sasa.
 
Tatizo kubwa ZAIDI NI UJINGA WATANZANIA WENGI NI WAJINGA SANA Hawaelewi kitu chochote. Hasa upande wa siasa.

Mfumo wa Elimu za chini hauruhisu wanafunzi kusoma Elimu ya siasa na uraia kwa mapana yake..

CCM wameua ELIMU makusudi kwa KULETA SHULE MBOVU NA MITAALA MIBOVU ILI KUTENGENEZA WAJINGA AMBAO NDIO MTAJI WAO KISIASA.

Elimu.
Elimu.
Elimu
Kwani Bwashee Hao akina Lema,Mbowe,Zito,Mdee,Bulaya,LISSU n.k wamesoma mitaala ya Nchi gani?na imetengenezwa na utawala wa chama gani?
 
Bila kupindisha maneno nchi yetu kwasasa inakabiliwa na mabadiliko makubwa ya mfumo.

Mfumo wa zamani wa vyama vingi na demokrasia unaelekee kufa na kuja mfumo mpya kama wa Rwanda, Urusi na China.

Utawala wa Chama kimoja na mtu mmoja wa awapendaje. Huu mfumo wa aina yake unaonekanaga mzuri pale tu ukiwa na kiongozi mzuri mzalendo lakini ukipata kiongozi mbinafsi mmoja tu anaweza kubadilisha nchi na akawa mfalme na kuwapa Watoto wake madaraka.

Je, Tanzania tunataka maendeleo ya muda ambayo haturuhusiwi kuhoji chochote zaidi ya wale tu wanao support au tunapenda demokrasia ya muda mrefu ambayo pamoja na matatizo yake ni Watanzania wanachagua watu wenyewe wawapendao

Tatizo kubwa tulilonalo kwa sasa ni kuwa na waaandishi wa Habari ambao wamebobea kuunga mkono kila kitu badala ya kupigania uhuru. Wenye ushabiki kuliko hoja na wanaopenda vihoja kuliko kuwa makini.

Tatizo lingine kutokana na nchi yetu kuwa na vijana wadogo wengi zaidi ya 80% chini ya miaka 28 tumekuwa ni nchi ya malimbukeni wengi kwasababu hawa madogo bado wengi hata hawajui dunia inapoenda.

Tushishangae wahamasishaji wakubwa ni wasanii ambao wengi hata Form 6 hawajafika, wasanii wanao toboa masikio, pua na kupaka rangi nywele. Kwa kimsingi wasanii sio Maisha halisi ya hawa vijana na hata majina wa usanii sio yao na ni waigizaji. Lakini hawa ndiyo wanatumika kuomba kura.

Kwa sababu ya mapungufu yetu ya kuwa na vijana wengi wasio jua na tamaa kubwa ya madara kwa viongozi wetu wanaopenda kusifiwa Tanzania inalekea kwenye udikteta. Kibaya zaidi inaelekea wachache wanaojua kinachoendelea nao wanatafuta pesa ambayo imezidi kuwa ngumu.

Wapinzani wamekuwa wanapigwa risasi, kufunguliwa kesi na kufungiwa biashara na wale wasioelewa wamekuwa wanakejeli tu bila kujua yajayo.

Tatizo lingine Watanzania wengi hawajui wanataka Tanzania gani?
Swali
Watanzania tunaitaji nchi ya aina ipi?
Jibu inatakiwa nchi yenye maendeleo ya kweli kwa mtu mmoja mmoja na taifa na democracy nzuri, kuludi mfumo wa chama kimoja hatuendi popote, democracy na maendeleo huwezi vitenganisha, mfano tu kenya kiuchumi wanazidi buruza nchi nyingi tu ndani ya afrika mashariki, na wako kwenye mfumo wa vyama vingi ,
So Kama yupo anaewaza kwamba mfumo wa chama kimoja utatufanya songa mbele,hamna kitu hapo ,
 
Utawala wa Chama kimoja na mtu mmoja wa awapendaje. Huu mfumo wa aina yake unaonekanaga mzuri pale tu ukiwa na kiongozi mzuri mzalendo lakini ukipata kiongozi mbinafsi mmoja tu anaweza kubadilisha nchi na akawa mfalme na kuwapa Watoto wake madaraka.
Kinachonipa faraja ni kwamba, jamaa anaumwa sana ila anajikaza kaza tu mbele za watu! 2021 kama ataimaliza nasi ashukjru Mungu sana!
 
Tunataka tuwe na mfalme ,kama huyu Raisi na kwa vile bunge lote ni limeundwa na CCM itakuwa rahisi kubadilisha cheo badala ya Raisi awepo Mfalme na pia ufalme usitokane tena na CCM bali tutumie Kabila la Mheshimiwa magufuli ndio liwe linatoa wafalme.
Tutapendeza zaid kulivyo tulivyo sasa.
Una maana Wah.......
 
Tunataka mambo ya gulio la katerero na senene.
 
Tunataka nchi ambayo haiongozwi kwa propaganda, nchi ambayo mgombea Kama aliahidi kushusha vifaa vya ujenzi Basi vishuke Mara tu anapochukua madaraka. Huyu wa Sasa ameapishwa juzi tayari bei ya simenti imepanda Mara mbili
 
Bila kupindisha maneno nchi yetu kwasasa inakabiliwa na mabadiliko makubwa ya mfumo.

Mfumo wa zamani wa vyama vingi na demokrasia unaelekee kufa na kuja mfumo mpya kama wa Rwanda, Urusi na China.

Utawala wa Chama kimoja na mtu mmoja wa awapendaje. Huu mfumo wa aina yake unaonekanaga mzuri pale tu ukiwa na kiongozi mzuri mzalendo lakini ukipata kiongozi mbinafsi mmoja tu anaweza kubadilisha nchi na akawa mfalme na kuwapa Watoto wake madaraka.

Je, Tanzania tunataka maendeleo ya muda ambayo haturuhusiwi kuhoji chochote zaidi ya wale tu wanao support au tunapenda demokrasia ya muda mrefu ambayo pamoja na matatizo yake ni Watanzania wanachagua watu wenyewe wawapendao

Tatizo kubwa tulilonalo kwa sasa ni kuwa na waaandishi wa Habari ambao wamebobea kuunga mkono kila kitu badala ya kupigania uhuru. Wenye ushabiki kuliko hoja na wanaopenda vihoja kuliko kuwa makini.

Tatizo lingine kutokana na nchi yetu kuwa na vijana wadogo wengi zaidi ya 80% chini ya miaka 28 tumekuwa ni nchi ya malimbukeni wengi kwasababu hawa madogo bado wengi hata hawajui dunia inapoenda.

Tushishangae wahamasishaji wakubwa ni wasanii ambao wengi hata Form 6 hawajafika, wasanii wanao toboa masikio, pua na kupaka rangi nywele. Kwa kimsingi wasanii sio Maisha halisi ya hawa vijana na hata majina wa usanii sio yao na ni waigizaji. Lakini hawa ndiyo wanatumika kuomba kura.

Kwa sababu ya mapungufu yetu ya kuwa na vijana wengi wasio jua na tamaa kubwa ya madara kwa viongozi wetu wanaopenda kusifiwa Tanzania inalekea kwenye udikteta. Kibaya zaidi inaelekea wachache wanaojua kinachoendelea nao wanatafuta pesa ambayo imezidi kuwa ngumu.

Wapinzani wamekuwa wanapigwa risasi, kufunguliwa kesi na kufungiwa biashara na wale wasioelewa wamekuwa wanakejeli tu bila kujua yajayo.

Tatizo lingine Watanzania wengi hawajui wanataka Tanzania gani?
Hayo ndio matamanio yako,hayo yote,yanahasara kuliko faida kama bado hujabaini.
 
Back
Top Bottom