Watanzania wanataka kuona tofauti ya "Watawala" na "Waomba ridhaa"!

Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
906
Wapendwa,

Kila baada ya muda fulani huwa napata sababu ya kuona tofauti kubwa iliyopo kati ya Tanzania na nchi nyingine duniani. Na ni wazi kuwa hii ni nchi ya tofauti. Nchi ambayo inaweza kuvumilia mambo mengi ambayo hayavumiliki kokote. Nchi ambayo ina watu wenye kipaji cha kubebwa na upepo mpya, huku wakisahau kabisa mikasa mizito iliyotokea na inayoendelea kuwatesa. Nchi yenye utajiri wa watu ambao wana mioyo myema kiasi cha kuona kuna "tatizo kubwa" kama la Richmond na Dowans na bado wakaletewa habari kama ya "Babu Samunge" na wao bila hata kuona ni mchezo wanaochezewa, wanahamia huko, wanapeleka akili zote huko na kisha wanasahau kabisa "Tatizo kubwa" na wanavumilia athari za tatizo hata kwa miaka 30 bila kuendelea kuhoji! Naam, ni hapa tu ambapo unapata kuona IPTL na Escrow inasumbua vichwa, halafu watu wanakuja na majibu rahisi, kisha wanawaletea hadithi ya Dengue na Panya road, ajabu wote wanaacha kabisa kufuatilia na kuhoji! Media zinanunuliwa kufanya brain washing na tunakuwa brainwashed kwelikweli!

Hata hivyo leo sitaki kuongelea ufisadi. Na siyo nia yangu kuelezea athari zake, pamoja na kuwa ndiyo chanzo cha mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya shilingi yetu, kunakopewa jina jipya la "Dola imepanda!" Leo nimeguswa kuzungumzia hili tatizo la nchi kukosa mwelekeo na dira.

Katika kuongezea maajabu ya Tanzania, niseme hapa kwetu tumeonekana tuna serikali ambayo utendaji wake hauna tofauti sana na wananchi wa kawaida au wapinzani. Hapa utaona mwananchi wa kawaida analalamika jinsi serilkali inavyoshindwa kuleta maendeleo. Lakini utakuta na wapinzani nao wanalalamika serikali kushindwa kufanya hili ama lile. Lakini ajabu ni kuwa utakuta na serikali inakuja kulalamika kwa sababu mtendaji wake hajafanya hili, au kiongozi mwandamizi ni mzigo au mwanachama mwenzetu ni fisadi!

There has to be a difference between the government and the opposition! Kama tunataka kutoka hapa tulipo, ni lazima tuwe na upande unaoweza kutoa solutions kwa matatizo yetu na siyo kulalamika wakati umepewa vitendea kazi vyote. Kwa mfano, huwezi kuwa na wananchi wanaolalamikia kushuka kwa hali ya usalama mitaani, wapinzani nao walalamikie hilohilo kwa sababu hawana resources kisha na serikali ije ilalamike kuwa kuna uhaba wa polisi na vifaa! Sasa hapo tofauti ya mwananchi mmojammoja na chama pinzani na serikali ni nini? Lakini ukienda mbele (kama unataka) utakuta mfano mwingine wa kushangaza. Kwa mfano unakwenda kutoa taarifa ya kufanya mkutano wa hadhara, halafu unaambiwa polisi haina askari wala vifaa! Lakini utashangaa utakapoamua kufanya mkutano huo, askari watakaokuja kukuzuieni ni wengi mara kumi kuliko wale ambao katika hali ya kawaida wangehitajika kuja kuhakikisha hali ya usalama inadumishwa! Hata idadi ya magari itaongezwa na ya ziada kama ya majiwasha yataletwa bila bajeti kufikia ukomo! Now this calls for an analytical question. Ni kwamba serikali haiwezi kutatua matatizo hayo au ni desturi mbaya tu tuliyojizoeza?

Sasa tuakwenda kwenye kipindi kingine cha maajabu. Kampeni. Na hapa mtasikia mambo mbalimbali. Mtasikia hawa wanawatuhumu wale na wale wanawatusi hawa! Na huenda hata msisikie sera wala ilani za vyama. Anyway sera za nini wakati hakuna anayejali kuzitekeleza? Lakini uzoefu unaniambia watafanya kituko cha siku zote. Watawala watakuja na ahadi kemkem kama kawaida. Wapinzani nao watakuja na ahadi zao za kuleta maendeleo ya hiki na kile. Na wananchi nao watachagua viongozi kwa matumbo yao bila akili zao kuwa pamoja nao!

Lakini hii ikoje? Kunatakiwa kuwe na TOFAUTI kati ya kampeni za aliyetawala kwa miaka kama 50 na huyu ambaye hajawahi kutawala kabisa. Wakati huyu Mwomba ridhaa anapokuja na ahadi kuwa "mkinipa nitafanya....." mtawala alitakiwa aje na kampeni tofauti. Yeye kwa sababu alipewa anatakiwa aseme..."nimefanya ...........!" Lakini ajabu ni kuwa na watawala wataahidi na kuahidi kama ambavyo wamekuwa wakiahidi! Sijui ni kwa sababu huwa hawatekelezi hizo ahadi ndiyo maana wanahitaji ku-repromise? Lakini nasikitika na wananchi hawataona hiyo janja yao! NA baada ya kampeni hizo za kitoto na matusi ya nguoni.......watachagua kwa tumbo. Shilingi Elfu kumi ikisaidiwa na njaa ya siku moja itamnunua mtu na kura yake kwa miaka 5!

Walisema wahenga "Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno" Hebu kuwe na anayeongelea lugha ya matendo. Ahadi tuuu hapana. Pia inajulikana kuwa wale hawana resources wala hawakuwahi kupewa nafasi ya kutenda. Sasa na tuliowapa nafasi ya kutenda what is the excuse? Basi walau be men enough to repent the failures before promising anything again!
 
Watakapo acha kuahidi tutakuwa tupo mwisho wa kikia kama taifa.
Ahadi ni muhimu kwa kuwa hutoa dira.


''anayejisifu kwa aliyofanya, leo hajafanya lolote''
 
Watakapo acha kuahidi tutakuwa tupo mwisho wa kikia kama taifa.
Ahadi ni muhimu kwa kuwa hutoa dira.


''anayejisifu kwa aliyofanya, leo hajafanya lolote''
 
Watakapo acha kuahidi tutakuwa tupo mwisho wa kikia kama taifa.
Ahadi ni muhimu kwa kuwa hutoa dira.


''anayejisifu kwa aliyofanya, leo hajafanya lolote''

Najua kuna umuhimu wa kuahidi. Lakini siyo mbaya walau ukiwa na sauti ya kusema nilisema nitafanya abc nimefanya a na c bado d au nimefanya yote! then ahidi upya.

Unapoahidi kuboresha elimu, halafu unaishia kuwaambia wazazi wajijengee madarasa, halafu hakuna walimu,maktaba wala maabara huo ni uhuni. Halafu ukiona wanapigia kelele huo uhuni unalazimisha walimu wakatwe hela kujenga maabara, ambapo tena unaishia kujenga majengo huleti vifaa wala chemical reagents. Huo ni ujuha! Kukamilisha mpango tunashuhudia watoto wanofaulu bila kufanya mitihani huku wengine wkifikia kidato cha tano bila kujua kuandika hata majina yao! Hii inatia hasira.

Mpendwa ahadi ni muhimu katika kuweka dira. Lakini ahadi hizi za kipumbavu na kilofa, hapana ( excuse my language, nimeazima maneno toka kwa rais msataafu pale jangwani leo)
 
Back
Top Bottom