Watanzania wanapoteza muda mwingi kwenye kusubiri...

zeus

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
213
55


Watanzaniawanapoteza muda mwingi kwenye kusubiri.........


Wakuu,


Wana JF, tumeshaongea sana kuhusumambo mengi yanayorudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu, nakutuzidishia umaskini. Lakini hebu tutizame na upande huu wa pili wawatu kupotezewa muda wake kwa kusubiri huduma fulani. Juzi niliendaRITA kuomba cheti cha kuzaliwa, nikaambiwa nisubiri nje kwenyebenchi. Nimesubiri kwa zaidi ya saa moja..., nilipomuuliza mhudumukuwa naomba anisaidie niwahi mahali, akaninijbu kwa ukali ..sinimekwambia subiri, kama huwezi kusubiri ondoka.....na wakati huokuna watu wengine wanaingia wanatoa malipo fulani wanaondoka. Kilasehemu ukienda ni kusubiri, kusubiri.... ukienda kuomba leseni tatizoni hilohilo.ukienda hospitali, mahakamani na kwingineko tatizo nihilo hilo.. Kusubiri huduma ni sawa lakini isiwe kusubiri kupitakiasi... kwa hiyo mtu ukienda sehemu tano tofauti kwa siku utajikutaunapoteza masaa matano (kwa siku) bila kufanya chochote. Hivi wakuuhuu muda tunaopoteza kusubiri si tungetumia kufanya shughuli zingineza maendeleo kama mtu angepata huduma mapema? Hii hali sio chanzomojawapo cha umaskini wetu?


//Mod hii thread usii move....kwanitatizo la kusubiri linahusu pia uwajibikaki//
 
Sasa hapo we si una uhuru wa kuchagua kusubiri au..... kwanini unamwambia MOD asiiondoe, isubiri nini? Si we unakerwa na kusubiri subiri?
Mkuki kwa nguruwe..... kwa binadamu.....
 
hujawahi kuingia benki ya NMB ungeacha kulalamika na KUSUBIRI michango ya watu hapa jf badala ya kufanya kazi nyingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom