Watanzania wanaichukia Tanzania yao?

Kahtan Ahmed

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
765
489
Kuna ushahidi wa kutosha kuwa watanzania wanaichukia nchi yao ya Tanzania na miongoni mwa ushahidi huo ni kama ifuatavyo;

1. Watanzania walio wengi wanafanya kila jitihada kukwepa kulikpa kodi kwa hali na mbinu yoyote.

2. Watanzania kuchukia viongozi wao kama inavyoonekana mpaka kuna watu wanashtakiwa na jamhuri kwa kosa kumtukana raisi wao.

3. Watanzania walio wengi hawashirikiani kabisa na vikosi vya usalama kama polisi n.k.

4. Watanzania waliowengi hawawezi kupongeza juhudi yoyote nzuri iliofanywa na serikali yao zaidi ya kubeza juhudi hizo.

5. Watanzania walio wengi wapo tayari kushirikiana na raia wa nchi jirani kujinufaisha wao wenyewe raia huku serikali ikipata hasara kwa kitendo hicho.

Na sababu hizi ndio tunapata tafsiri kuwa watanzania hawana uzalendo wa nchi yao ila swali la kujiuliza kwa sisi watanzania ni kwanini tunakosa uzalendo wa nchi hii?

Naomba maoni yenu tafadhali.
 
Kodi inakwepwa popote ulimwenguni ndugu yangu. ..ingekuwa huko watu wanapenda kulipa kodi wasingewekewa sheria ngumu kiasi kile...angalia kwa mfano china na marekani pekee utapata jibu
Pili watanzania tunaipenda nchi yetu tena tunaipenda sana ndio maana unaona mpaka sasa amani imetamalaki
KINACHOCHUKIWA TENA SANA NA WATANZANIA NI CCM
 
Kwa sababu somo la uraia linafundishwa shuleni tu tena kwa kiingereza unawamezesha wanafunzi maneno kama "amendment", " referendum", "rule of law", " jurisdiction" bila wao kuelewa jinsi ya kuyaishi maneno hayo.
 
Kodi inakwepwa popote ulimwenguni ndugu yangu. ..ingekuwa huko watu wanapenda kulipa kodi wasingewekewa sheria ngumu kiasi kile...angalia kwa mfano china na marekani pekee utapata jibu
Pili watanzania tunaipenda nchi yetu tena tunaipenda sana ndio maana unaona mpaka sasa amani imetamalaki
KINACHOCHUKIWA TENA SANA NA WATANZANIA NI CCM
 
Tatizo linaanzia juu kabisa kwenye uongozi wa nchi. Hawa wanajihusisha na ufisadi, wanatumia nyadhifa zao kujitajirisha kwa njia mbali mbali za haramu, wanakwepa kulipa kodi ama kwa kutumia misamaha ya kodi au kinyemela. Wanasaini mikataba ya rasilimali za nchi ambayo haina maslahi kwa Tanzania na Watanzania. Kwa sababu hizo nchi pamoja na kuwa na utajiri mkubwa sana bado iko nyuma sana kimaendeleo miaka 55 baada ya uhuru.
 
Bahati mbaya kwa nchi na wananchi nikuwa kikundi hicho kimeendelea kung'ang'ania madaraka tena kikatiba.

Na mbaya zaidi wamewekeza ktk kuhakikisha ufahamu wa wananchi unazidi kuwa mdogo kwa faida yao.
 
MKUU UMEFIKIRI SANA AISE. PONGEZI KWAKO.
Watanzania hawaipendi nchi yao? Namba tano imeniumiza sana. Kwa hali hiyo baadhi yao siyo wazalendo kamili.
 
Na hawa kwenye kundi hili dogo wanaendelea kulindana kwenye maovu yao kwa gharama yoyote ile bila kujali maslahi ya nchi. Kwa hali hii ufisadi, wizi, upokeaji rushwa, kusaini mikataba isiyo na maslahi kwa nchi, vyote hivi vitaendelea kushamiri.

Bahati mbaya kwa nchi na wananchi nikuwa kikundi hicho kimeendelea kung'ang'ania madaraka tena kikatiba.

Na mbaya zaidi wamewekeza ktk kuhakikisha ufahamu wa wananchi unazidi kuwa mdogo kwa faida yao.
 
Nchi moja hapa jirani pamoja na ukabila lakini jamaa wanvyoipenda nchi yao, yaani hadi nawaonea wivu. Jamaa wana mapenzi makubwa hasa bendera ya nchi yao. Tulikuwa tumeakata tamaa na viongozi wetu hasa huyu aliyetoka chama tawala na wezi wenzake wakaamia upinzani na kuuharibu kabisa ndio walinifanya mimi binafsi kuichukia Tanzania.
 
KhatAn Indian boy unajua kwanin watz wako hivyo...hii imesababishwa na JAMAA za asil yako na wawekezaj baadhi Kwa kushirikiana na watawala Wa chache enzi hizo kuwafAnya watz waichukie nchi huko nyuma_,but for now on Tanzanian we like our country more than ever and you know that...We have a faith ...we have magu most important we have God...kodi mtalipa end of time u will come with a thread now we like our country janja janja zenu kwishinei mtasaga meno maghorofa ya mjini tutapohitaj kuyarekebisha muamishie makaz yenu uswaz na biashara zenu zote
 
Nchi ilishaharibiwa tokea zamani, sisi tunaendeleza tu ukichanganya na njaa zetu haya mambo yataendelea kuwepo.
 
KhatAn Indian boy unajua kwanin watz wako hivyo...hii imesababishwa na JAMAA za asil yako na wawekezaj baadhi Kwa kushirikiana na watawala Wa chache enzi hizo kuwafAnya watz waichukie nchi huko nyuma_,but for now on Tanzanian we like our country more than ever and you know that...We have a faith ...we have magu most important we have God...kodi mtalipa end of time u will come with a thread now we like our country janja janja zenu kwishinei mtasaga meno maghorofa ya mjini tutapohitaj kuyarekebisha muamishie makaz yenu uswaz na biashara zenu zote
sijui kwasababu ya jina au sijui umetumia vigezo gani vya kunifikiria kua mimi ni muhindi ila wanajamii forum wengi wananifahamu mimi sio muhindi narudia kukuelekza kua mimi sio muhindi mm ni mtanzania halisi pengine kuliko wewe unaojiita mtanzania
 
Kodi inakwepwa popote ulimwenguni ndugu yangu. ..ingekuwa huko watu wanapenda kulipa kodi wasingewekewa sheria ngumu kiasi kile...angalia kwa mfano china na marekani pekee utapata jibu
Pili watanzania tunaipenda nchi yetu tena tunaipenda sana ndio maana unaona mpaka sasa amani imetamalaki
KINACHOCHUKIWA TENA SANA NA WATANZANIA NI CCM
Halafu hajitambui huyo mkuu, watanzania tunaongoza kwa kulipa kodi ila CCM kupitia high ranking official wake (be in the government or in the party) ama wao wenyewe au kwa kushirikiana na wafanya biashara. Mtanzania wa kawaida mshahara wake unakatwa kodi hata kabla hajaulipwa Halafu baada ya hapo the balance which is already taxed bado ataendelea kulipa kodi zote kama VAT katika kila anachonunua sasa mtoa mada asituletee hoja mufilisi hapa.

Pili watanzania hawakosoi kila kitu serikali inafanya bali wanachukia double standard inayoendelea , ufanyaji kazi kwa mihemko, zuilio la freedom of speech na sasa tunaona tunaelekea kufuta vyama vya upinzani
 
out of point
 
Watanzania wengine hawataki kujitambulisha kuwa wao ni wabongo wakiwa abroad. Hii tabia wanayo Wazanzibar we better grants them autonomous state. Wanakera Sana .
 
Mbona unanziba mdomo c uniache niseme!!!
System ndo mbaya tanzania ni nzuri kama malkia wa sheba!!
kitanda ni kizuri ila kikiwa na kunguni wanakukula utakiona kibaya!ili utam wa kitanda urudi ni kuangamiza kunguni.
 
Back
Top Bottom