Kwa Tanzania ya sasa na sisiemu ya leo sidhani kama kuna kiongozi yeyote mwenye utashi wa kisiasa wa kuzuia pesa haramu zisitoroshwe. Wanaotorosha pesa hizo kwenda katika nchi tajiri sio kwamba 'sirikali' haiwafahamu, wanafahamika sana tu na huenda hata Mhe Meghji anawajua. Sema sasa Mhe Meghji anatoa kauli hii utadhani anaongea na watoto wa shule za awali, ambao hawajui maana ya utoroshaji wa fedha. Ina maana sheria za namna hii hatunazo tangu zama na zama kweli? Mimi ninavyojua ni kwamba Benki Kuu wana utaratibu wao maalum wa kuratibu pesa zote zinazoingia na kutoka nchini, pamoja na kujua baadhi ya vyanzo vyake na kujua wahusika. Pia mabenki yote nchini yana taratibu za namna hii, ikiwa ni pamoja na kuripoti taarifa hizi katika Benki kuu.
Aliyokuwa anayasema Mhe Mrema miaka ya tisini kuwa pesa zilikuwa zinasafirishwa kwenda nje ya nchi katika vifungashio vya majani ya chai ni zipi? Si ndo pesa hizi haramu ama?
Hawa wanasiasa waache usanii, tushawagundua sana.
Anyway, siku zao zahesabika!