Watanzania wakataa "ELIMU YA BURE HADI UNIVERSITY"

Watanzania wakataa "ELIMU YA BURE HADI UNIVERSITY"

Status
Not open for further replies.
Mtoa mada we ni mipumbavu kuliko ata Kondoo.
Hatupo tayari kudanganywa lofa wewe.
S. Africa wameongeza ada vyuo vikuu.
 
Wengi wanapenda tisheti na kofia kuliko elimu.wanapenda mateso zaidi.kwao furaha au maisha mazuri ni anasa inayoweza kuwakosesha mbingu.wanaamini tajiri haendi mbinguni.
 
Acha ujinga, watanzania wamekataa kudanganywa kwa sweet words. Hii kitu hatujafika bado! Watanzania ni very intelligent, HONGERA WATANZANIA WENZANGU, hakika tumezungumza!

Hebu fafanua huu UINTELLIGENT wa watanzania ni upi hebu fafanua, Kumchagua mbunge aliyekaa Miaka 15 na hajakufanyia lolote la kujivunia ndio Uintelligent?
 
Mtoa mada we ni mipumbavu kuliko ata Kondoo.
Hatupo tayari kudanganywa lofa wewe.
S. Africa wameongeza ada vyuo vikuu.

Tuliowahi kusoma bure tunaelewa kuwa elimu bure inawezekana.
 
Yap! South Africa ndo bingwa kwa Africa lakini hata ndoto za Elimu bure hadi chuo kikuu bado!

Sikia....hawapewi huduma hizo utakazo bure ila wanaandaliwa mazingira ya kuyamudu k.m.kupata ajira zenye ujira mzuri,mazingira ya kujiajiri wenyewe na maisha yanakuwa siyo ya manung'uniko ya kupitiliza.
 
Inasikitisha sana. Sijui ni lini ndugu zetu wa vijijini wataamka toka usingizini?
:angry:

Wataamka tu mkuu, Maisha magumu yanayokuja yatawafanya waamke. Cha msingi tujitahidi kwa kadili tuwezavyo tuwaonyeshe ubaya wa CCM kwa kuanzia kwenye Miundombinu, Afya, Elimu, Uchumi Nk. Wataelewa tu.
 
Ndiyo reflection tunayoiona wakti matokeo yakiendelea kutangazwa na badala yake watanzania wengi wameamua kuishia kidato cha nne na huko kwingine watalipia watoto wao wenyewe.

Watanzania wameamua bora kukosa elimu ya juu, bora mgawo wa umeme kuendelea, bora kuendelea kusomea chini, bora kukosa dawa na bora akina mama kulala chini kuliko kukiondoa Chama tawala madarakani

Watanzania wamekataa mfumo mbadala wa kuwaletea maendeleo na wameamua nchi iongozwe kwa mfumo ule ule na watu walele na familia zilezile

Angeanza kuwapa elimu ya kujistili wale wapiga kura wake kule monduli badala ya kutembea dushe nje na wapige suti kama yeye tungemwamini lakini kwakuwa ameshindwa kufanya hivyo basi ilibidi tumkate tu kama walivyofanya ccm
 
Yaani mimi nimeapa, sitomsesha wala kutoa mchango wowote wa kimasomo kwa ndugu yeyote zaidi ya mwanangu wa damu yangu mwenyewe!!!

Nakuambia nilikua na wazo kama lako ila nashindwa sasa kwa kua arusha chadema wameshinda kote sasa nashindwa nifanyaje mkuu
 
Khaaaaaaaaaaaa!!!!!, mutajijua na maisha yenu sasa hivi vile vijitu vinavyopitaga karibu na ofisi yangu kuomba msaada jibu litakuwa HAPA KAZI TU ............................. MSAADA WAONE WAFADHILI.
 
eistein huyo huyo huyo alisema wajinga huwaona werevu kuwa wajinga na wao wajinga kujiona wao ndio werevu. sasa katika hali hiyo nani wa kumtoa mwingine kule aliko kusiko faa na kumpeleka kunakofaa ni shida maana kila mmoja anjiona yuko sahihi.

yawezekana ukawa na mtizamo wako unauona ni sahihi na wengine wanaona mtizamo wako si sahihi je ni nani mjinga na ni nani anayejua? maana ili jamii isonge mbele inahitaji kufuata njia sahihi na pande zote mbili zinajiona ziko sahihi?

kwa mtizamo wangu binafsi ninaamini elimu ya bure ni ujinga unaotupeleka kwenye umasikini kwa hoja kuwa.

hakuna kitu chochote cha bure, ama tukigharamikie kwa kutumia fedha za pamoja tunazozichanga kwenda kwenye mfuko wetu kama watanzania unaosimamiwa na serikali au tulipie kwa fedha zetu za mifukoni.

fedha tunazochangia kupitia kodi na rasilimali nyingine zinatakiwa kutumika kujenga miundo mbinu kama shule, zahanati, barabara, miundombinu ya maji, umeme, gharama za uendeshaji na utoaji wa huduma kwa maana ya kuwalipa watumishi na kujenga miradi kadha wa kadha ya maendeleo katika jamii yetu.

sisi kama jamii masikini michango yetu ni kidogo sana na hii imepelekea kutuongezea umasikini kwa maana huduma ni duni, bado hali ya miundombinu au facilities za kutolea huduma na utaalamu ni duni na hii imesababisha jamii yetu kukosa huduma.

mtu yeyote anayewaza huduma za bure amepitwa na wakati kwa mtizamo wangu kwa maana hiyo ilikuwa ni mahitaji ya watanzania miaka ya 60 na sabini kutokana na hali ya kimaisha ya watanzania. enzi hizo shughuli za kufanya zilikuwepo lakini watanzania walikosa maarifa. mtu alikuwa anahitimu kidato cha nne anapangiwa kituo cha kufanyia kazi maana watu wenye elimu walikuwa wachache. michango ya jamii wakati huo ilikuwa sahihi kusomesha wanajamii hawa ambao uchumi wao ulikuwa duni hawakuwa na uwezo wa kumudu gharama za masomo.

leo hii uchumi wa watanzania umebadilika na mazingira yamebadilika, watanzania uchumi wao kwa sasa wanamudu gharama za masomo ila changamoto zimebadilika kuwa wasomi wanaanza kuwa wengi kuliko nafasi za ajira, ubora na wingi wa huduma mbalimbali katika jamii ndio imegeuka kuwa changamoto kubwa. watanzania wanaohitaji ajira wamekuwa wengi kuliko nafasi za ajira zilizopo. kwa mazingira haya kwangu mimi naamini ni ujinga kudhani huduma za bure zitakomboa jamii hii.

huduma za bure zitapunguza kiasi cha fedha katika mfuko wetu wa pamoja kinachoweza kutengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo. kupungua kwa uwezo wakifedha na kasi ya kutekeleza miradi ya maendeleo kutapunguza uwezo wetu wa kutengeneza nafasi za ajira mpya hivyo un employment itaongezeka.

hivyo watanzania wa leo wanahitaji fedha zao zinawatengenezee mazingira ya kuzalisha au kupata ajira. hatuhitaji wakulima wetu wawe na digrii kila mmoja ndio tuzalishe chakula cha kututosha na kupeleka ziada nje, tusidhani kukosa elimu kwa watanzania ndio kunasabisha asilimia kubwa ya bidhaa ndogo ndogo kutoka nje.

anayefikiria huduma za bure ni kipofu anayestahili kuongozwa na sio yeye kukaa mbele kuongoza wengine. labda nikuulize wewe mwenyewe unachokitaka maishani mwako ni kitu gani, fedha kidogo ya serikali itumike kukutengenezea mazingira ya wewe kufanya kazi na kuongeza kipato chako au fedha hiyo itumike kusomesha watoto wako katika shule za sasa za serikali na kutoa huduma za afya kwenye vituo na zahanati za serikali bure. kumbuka anayekuambia kuwa atakufanyia yote ni mwongo kwa maana fedha yetu ni kidogo hivyo kiongozi anaweza kufanya moja na sio kwa ubora au kasi unayohitaji bali kwa kasi ndogo.

Albert Einstein alisema "uendawazimu ni kufanya jambo lile lile' mara nyingine na kwa namna ile ile huku ukitegemea matokeo tofauti" pongezi ziwaendee wakazi wote wa mijini isipokuwa mwanza tu wamefanya kazi nzuri. watu wa vijijini wanastahili hayo maisha milele zote
 
Ndiyo reflection tunayoiona wakti matokeo yakiendelea kutangazwa na badala yake watanzania wengi wameamua kuishia kidato cha nne na huko kwingine watalipia watoto wao wenyewe.

Watanzania wameamua bora kukosa elimu ya juu, bora mgawo wa umeme kuendelea, bora kuendelea kusomea chini, bora kukosa dawa na bora akina mama kulala chini kuliko kukiondoa Chama tawala madarakani

Watanzania wamekataa mfumo mbadala wa kuwaletea maendeleo na wameamua nchi iongozwe kwa mfumo ule ule na watu walele na familia zilezile
hiyo ccm B iliyonunua cdm ndio chanzo cha shida ulizozitaja. wameamua kuendelea na ccm A yenye matumaini mema chini ya jpm.
 
Tupo tayari kubadili gia angani lakini elimu ya bure ni sawa na kusema no free lunch
 
Kwanzia leo ndugu mwenye uelekeo wa CCM akiomba Msaada jibu ni HAPA KAZI TU, MSAADA NENDA CCM.
 
...Watanzania wameamua bora kukosa elimu ya juu, bora mgawo wa umeme kuendelea, bora kuendelea kusomea chini, bora kukosa dawa na bora akina mama kulala chini kuliko kukiondoa Chama tawala madarakani

''Watanzania (wengi....) ni MALOFA na WAPUMBAVU'' - W.B. Mkapa

Siku nikikutana na Mzee Mkapa ntamnunulia ile Whisky anayoipenda sana
 
Uloi nga mâché68;14474748 said:
Watanzania wana uelewa wa hali ya juu na kamwe hawawezi kudanganywa na porojo za UKAWA za kutoa Elimu bure mpaka Chuo Kikuu wakati huko nyuma SERA hiyo ilishindikana! Ni vijana wanywa viroba tu ndio walidanganyika!
mmesahau kulikuwa na watu hawamkubali mgombea urais wa ukwa. Hivyo wamepigia mmbunge raisi kijani. Hili ni kosa ambalo ukawa ndio wanatakiwa walijutie. Ukubali usikubali, angesimama let say Lipumba au Slaa, magufuli asingeshinda kirahisi hivi. Na CCM hilo walilifanyia kazi ndio maana walimkata Membe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom