Watanzania/waafrika tunadharauliana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania/waafrika tunadharauliana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimbweka, Aug 29, 2010.

 1. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Habarini wakulu!
  Hii imenitokea nikiwa pale arusha! Nilienda kwa ajili ya kupata matibabu ithner asheri charitable dispensary. Wanakawaida ya kutoa namba kwa ajili ya kumuona daktari. Mie nilitaka kumuona dk Mohmd. Cha ajabu wale wahudumu wa pale huchanganyikiwa waonapo ngozi nyeupe(wahindi,waarabu, wazungu.etc) yaani utaratibu wa kufuata zile namba unavurugika wanawaingiza hao weupe bila hata namba hata kama wamechelewa kufika. We mweusi utaachwa hapo na kuona wengine wakija na kuondoka. Tena wengine huzungushwa kwa kupitia mlango wa nyuma! Wale wahudumu huwa wanahongwa! Kwa kweli ckufurahishwa na kitendo hiki maana huduma itolewayo hapo ni ya kulipia na si bure haki itendeke na si kujali rangi au utaifa wa mtu! Watanzania tunajidharau wenyewe jamani eeeh
   
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hilo lipo na sehemu nyingine pia za huduma. Ni kweli baadhi ya wenzetu wanahitaji kubadilika kifikra na kuacha ubaguzi huu.
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hili lilinisikitisha sana mkuu na kuweka uchungu mwingi ndani ya moyo wangu! Hii pia naona ni aina fulani ya kutawaliwa na kwa maana nyingine wakoloni wanarudi kwa mbinu nyingine kabisa hasa katika nyanja nyingi za kutoa huduma katika jamii:confused2:
   
 4. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,312
  Trophy Points: 280
  Kimbweka
  Nadhani itakuwa vizuri sana wewe ukachukua hatua. Mara nyingi maudhi ya namana hii humalizwa kwa kuwaeleza wahusika ukweli. Kwa mfano kama wamempenyeza mzungu na nyie mko kwenye foleni inabidi uchukue hatua palepale... unaweza kum-face palepale na kumwuuliza kwa nini hafuati foleni... pia uongozi wa hospital upewe manung'uniko. Ikishindikana organize watu mfanye demonstration nje ya hospital... hata kama ni ya watu watatu... Mkikaa kimya watawaona kama mnaridhika na wanayofanya.
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu kuna sanduku la maoni ndilo niliona nilitumie kupeleka ujumbe
   
 6. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kuna mchangiaji amesema hapo. Wakati mwingine unamaliza udhia pale pale. Unamface anayetenda kosa hilo na kumpa live pale pale wala huna haja ya kuandika maoni. Si ajabu hicho kisanduku kinafunguliwa kila baada ya miezi mitano! mkosaji anaweza kujibaraguza kama ilivyo kawaida ya watanzania, lakini ujumbe unakuwa umefika!
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Waone wahusika hapohapo!
   
 8. faithful

  faithful JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kuna kaka mmoja nilisoma nae ni raia wa sweden alikuja tz kutembea nikawa nae zanzibar hotel fulani na mimi ndio nilimpeleka hapo hotelini kula raha za hotel za kitalii bs muhudumu alikuwa akija kutusikiliza akiongea na yule kaka anamnyenyekea akija kwangu ananichukulia poa tu!alivyoleta bili baadae sana akampa yule mkaka nae akamwonyesha ishara anipe mimi basi nikafungua wallet nikamlipa na nika mwachia chenji bs alijisikia noma sana kwani alishaonyesha kunidharau mimi na kumthamini sana yule mgeni wangu!
   
 9. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe ulingoja sana. Ulitakiwa nawewe uingie nae kudadeki ndo watapata adabu. hao wafanyakazi waambie kama siyo mimi kuja hapa usingepata huo mshahara na aliye chelewa na kuja kuingia ungemwambia subiri because i was the first to line-up my friend. Duu, wananikomaga mzee.
   
 10. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kaka uwezo huo ningekuwa nao kama ningekuwa mzima :becky::becky: kumbuka nilikuwa naumwa (Mgonjwa) hata kuongea na mtu niliona karaha! Asante kwa maoni:becky::becky: next time tunaende na sirinji zetu tena zikiwa zimetiwa dawa halafu akileta longolongo unamwambia lazima utakuwa na homa ya vichaa ngoja nikudunge upone:becky::becky::becky::becky: mwenyewe ataachia lango upite:becky::becky:
   
 11. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kweli tunajidhalilisha maana Mtanzania akiona rangi nyeupe tu anachanganyikiwa ndiyo maana hata wadada zetu wameibukia kujishoboa kwa wanaume wa ngozi nyeupe hata hawajui history background zao huenda alipotoka ni mhalifu sugu (jambazi) au ni mfungwa wenyewe wanajilengesha wakifikiri watapata fedha sana hawajui kuwa na siye mikaka ya kibantu siku hizi tuna mihela ya kufa mtu:becky::becky::becky::becky:
   
 12. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,501
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mzee hapa issue ni cash,... jsut be you,.. whether with or without cash. Wewe unaweza kupata picha kuwa mtu kakudharau kumbe yeye ndiye anayejidharau, that's why anaweze akamisbehave kwa wengine,...., just be you!
   
Loading...