Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,091
- 34,899
WATANZANIA waishio ughaibuni wameanza kushirikishwa kwa kupewa ajira serikalini, ikiwa ni njia kuwapa nafasi ya kuchangia maendeleo ya nchi.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe alisema hayo wakati wa ufunguzi wa semina kwa wakufunzi watakaotekeleza mradi wa kushirikisha Watanzania waishio nchi za nje (Diaspora) katika
kuchangia maendeleo ya Tanzania.Membe alisema kwa miaka miwili iliyopita, Rais Jakaya Kikwete amekuwa akiwapa nafasi za uongozi serikalini Watanzania waishio nje ya nchi.Kwa takribani
miaka mwili, Rais (Kikwete) amekuwa akiwaajiri diaspora (Watanzania waishio nje ya nchi) ili kuonesha ulimwengu kuwa tunawajali,alisema Waziri Membe. Alisema, Mfano mmoja
ameajiriwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais Zanzibar na Mkuu wa Wilaya, lakini tutegemee watu wengi kupewa ajira ili kuchangia maendeleo ya nchi.Membe alisema katika mpango wa kutaka
kushirikisha Watanzania waishio nje kuleta maendeleo ya nchi, wamebaini Watanzania wengi walio ughaibuni ni masikini na hawana kazi za maana, kutokana na kukosa uraia wa nchi husika.
Tulichofanya ni kwenda kuzungumza nao kuangalia changamoto zinazowakabili, tulichobaini ni kuwa watu hao ni masikini na hawana uwezo wa kuchangia maendeleo, na pia hawana kazi za
maana pamoja na kuwa na taaluma ambazo zingewafanya wapate kazi ya maana,alisema.Alisema nchi nyingine, raia wake walikwenda ughaibuni kama wakimbizi hivyo kupewa nafasi ya upendeleo
ya kufanya kazi na kusoma, lakini Watanzania wanashindwa kufanya hivyo kutokana na kukosa
uraia wa nchi hizo. Alisema ufumbuzi wa tatizo hilo ni kubadili sheria ya Uhamiaji iruhusu Watanzania kuwa na uraia pacha.Tunashukuru mchakato wa Katiba umeliweka hilo,alisema
na kuongeza ana imani, ifikapo 2015 suala hilo litakuwa historia. Membe alitoa mfano wa nchi ambazo raia wake wanachangia uchumi kuwa ni Kenya, ambao wanachangia dola bilioni 1.6 kwa
mwaka, Ghana dola bilioni 2.1 na Nigeria dola bilioni 3.5 kwa mwaka.Aidha, Membe aliwataka wakufunzi wanaopewa mafunzo hayo, kuhakikisha wanatoa elimu kwa Watanzania wanaopinga
mpango huo ili wajue kuwa kuishi ughaibuni siyo uhaini au usaliti bali ni njia ya kutafuta
Tumefanya sensa ya kutambua Watanzania wanaoishi nje ya nchi, pamoja na kuwa bado
haijakamilika mpaka sasa kuna Watanzania milioni 3.7, alisema.Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Damien Thuriaux alisema wamezindua mradi huo baada ya kupokea maombi ya
msaada wa ufundi na fedha kwa Serikali ya Tanzania.Alisema mradi huo umelenga kuimarisha uratibu miongoni mwa wizara kuhusu masuala ya wahamiaji, kuelewa njia ya kushirikisha
Watanzania waishio nje ya nchi, na kusaidia kutengeneza mtandao na itadhaminiwa na Mfuko wa Maendeleo wa IOM (IDF). chanzo.http://www.touch.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/20982-watanzania-wa-nje-kupewa-ajira-serikalini