Watanzania ughaibuni

Nani amesema hakuna matajiri wakitanzania Ughaibuni? Swali nililouliza je pamoja na hizo pesa zao wamewaisaidia jamii ya kitanzania, tukiachana na hizo western union ambazo pesa zinakwenda kwa ndugu tu. Au mpaka tumngoje Will Smith na John Legend kuja kusaidia maji masafi au kujenga shule Tanzania.
Au mnafikiri kwamba Will Smith hajui kwamba kuna serikali ya Tanzania?
 

Kinyume kabisa, umeweka msumari wa nguvu kubwa kwenye hoja. Ninaishi Tanzania lakini nimejaliwa kusafiri sana sehemu mbalimballi duniani. Nakutana na watanzania. Wengi wao niliwafahamu kabla, wazazi wao kama wa kwangu na shuleni walikuwa wazuri tu. Lakini wakaja Ulaya and by default wakaanza kuonja huduma hizi unazoziita first class, lakini kumbe siyo wala. Hawawezi kupata huduma first class hawa hata mara moja ila huduma wanazopata zinazidiana ubora na za pale nyuumbani. Wapo Wasomi wazuri wanataaluma wanafanya kazi za ajabu, ashakum si matusi(sijui wanaisema hivi!) nimeona Engineers, Accountants wanafanya kazi za kuwalisha wazungu wazee, wanafajia, wameajiriwa na watu ambao hawajaenda shule kabisa.

Wanaishi maisha ya kubabaisha. Na wengi wao ni kama omba omba wanapokutana na sisi tunaopita pita. Sasa Mzee wapate huo mshahara wa mwisho wa mwezi, acha bwana ni hizo party unazozisema. Call them anything. Kwa maana halisi ni rahisi hawa kushabikia viongozi wa CCM na wakati mwingine kutaka kuwa karibu na Balozi zetu kama sehemu ya hifadhi. NINAJUA SIO WOTE wanafanya hivi, lakini ni namna ya wale wenye uchovu kutafuta kinga.

Ushauri wangu na hasa kwa hawa ambao wana taaluma (maana wasio na taaluma ni kibao, nadhani SA ni wengi, lakini naona Sweden, Denmark, USA na UK nao ni wengi) WARUDI tuje tusaidiane kuendesha taasisi zetu hasa vyuo ambako kuna uhaba mkubwa kweli wa wakufunzi. Kuna ambao wamerudi na wanang'ara sasa hivi, mifano ni mingi
 

Mawazo yako ndio yanayomfanya Bill Gates aje kumijengea UNI badala yakujenga wenyewe!!!




Tanzania inajengwa na watanzania wenyewe.
Bill Gates anawajengea hospitali kwa sababu rais wenu kutwa anatembeza bakuli kuomba omba msaada. Badala ya kuwauliza watanzana walioko nje wanaifanyia nini nchi uliza serikali inafanyia nini kodi inayokusanya kila siku.
 

Uzi ungepata positive responses ikiwa ungeacha lugha ya kulaumu, kushambulia na kutuhumu.

Mi binafsi nionavyo kuhusu hii ishu, naamini watz tungefika mbali sana kama tungekuwa organised. Organisation ni mbovu kuanzia serikalini mpaka kwa watu binafsi. Kuna elements zingine pia za ubinafsi, utapeli n.k n.k nazo zinachangia..lakini tungekuwa na organisation hata hukohuko bongo mambo mengi sana yangefanikiwa.
 
 

mZEE..

Kuna watu CCM na dili zake za feki za kukata tawi wanalokalia, ndio zinawalisha, kuwavisha na kuwawezesha kufanya fujo zao mjini. Sasa mtu kama huyu kila thread JF inamtia kiwewe.
 
Wadau nimesoma post zote hapo juu. Nimekutana na mawazo mchanganyiko sana kuhusu ughaibuni. Nimepata opportunity ya kumtembelea mdau US. bongo hapa nafanya kazi. Nina bachelor ya utawala wa biashara. Kaniambia naweza kwenda then nikasaka ajira huko na hata nikikosa naweza kurudi au kuangalia mbadala mwingine. Nachouliza ni kuwa, maisha US yanawezekana? Au bora kubaki na ajira yangu hapa bongo
 
Yote sawa kila kitu sawa. Na ninaongeza hivi ili mzizi wa fitina uishe na hayo maendeleo muyaone na wasomi wengi walioko nje warudi basi kateni mziz wa fitina wa CCM kwa kuwaonyesha kuwa mmebadilika na democrasia ya ukweli ni kuipa mshikemsike ya kutoipigia kura au muaelimishe wananchi wawapeleke wabunge wengi wa upinzani bungeni acheni maneno hay ya ajabu ajabu. Hapa kuna wamarekani wameikimbia nchi yao kwa kuja kufanya kazi Australia akijua atafanya kazi na kulipa kodi ili apate afya bure kabisa (Medicare) ya first class. Kwa hiyo kinachofanya watu waikimbie nchi ni mfumo wa sera mfano wa kitanzania ni wa kibinafsi kuanzia serikali ya juu mpaka famialia na mtu binafsi .
 


Achana na wapiga porojo wa JF, chukua likizo nenda US, utaona hali halisi ya maisha bongo unafanya kazi ama kibarua? wanofanya kazi ni JK na mafisadi wenzake kuimaliza nchi, jipange mwanangu, mbele kwa mbele.
 

Ata ungeweka wengi wao bado kungekua na makosa, huwezi kuja na speculation ukafanya ni hoja. Kwanza kabisa, umefanya research? Unachodai hakina msingi bila kuwa umefanya research, which involves a good method for collecting data, analysis etc. Ungesema umefanya hivyo na hizi ndio fundings labda ningekuelewa. Otherwise, ulicholeta ni speculation attracting watu wenye chuki zao, kutaka kutoa frustration etc. Hata hivyo kama hiyo ndio ilikua target basi hapa JF watu hao sasa wamejaa...hautakosa wataokupongeza for an empty analysis
 
Njilembera usiongee kama kada wa CCM hao wasomi warudi utawapa kazi? Sera mbovu za CCM zimechangia sana kwa wasomi wengi kuikimbia nchi yetu, binafsi nina mifano mingi tu wapo watanzania wenye taaluma zao walianzia nyumbani bado wanaendeleza fani zao US kilichowaondoa ni kutothaminiwa na serikali yetu, suala la kumuona mtu akifagia, akilisha wazee huo ni mwanzo tu, tatizo linalowakabili watanzania ni mfumo wa elimu ya marekani kwani mara nyingi vyetu vya Tanzania havikubaliki, nimeona vijana ambao wameweza kujisomesha wenyewe na hivi sasa wana kazi nzuri tu, kumbuka maisha ni kuchagua, tatizo la party mbona lipo hata Tanzania labda kama unaishi Ifakara, Je unataka kuniambia msomi aliyetoka Kigoma kwenda kutafuta kazi DSM arudi kwa Kigoma kwa sababu amepata kazi ya ulinzi Ultimate Security? Umeongelea suala la wakufunzi jiulize wanalipwa kiasi gani? Malipo duni wanayopewa ndiyo yamechangia kuanguka kwa elimu ya juu, sidhani kama umewahi kutembea US vinginevyo usingeandika utumbo kama huo!
 
Achana na wapiga porojo wa JF, chukua likizo nenda US, utaona hali halisi ya maisha bongo unafanya kazi ama kibarua? wanofanya kazi ni JK na mafisadi wenzake kuimaliza nchi, jipange mwanangu, mbele kwa mbele.

haina mbaya mkuu. Nadhani una experience na unayoongea. Ajira ninayo, tena serikalini sema ndio hivyo unaweza kuruka majivu ukakanyaga moto
 
Kama ajira unayo poa katembee utoe vumbi la macho hakuna ubaya, ninachokueleza nina uhakika nacho kupanga ni kuchagua!
 

Haina hata haja ya research kujua ya Wengi watanzania waishio Ughaibuni.

Kila kona ughaibuni unaona sijui kuna white party Stockholm, London, sijui wapi kwingine ambazo ndio tunaongoza watanzania kwa hizo party.
Tunaona kwenye blog zenu.
Au mkiwaona wakina Vodacom kuchangia mashule hawajui kwamba kuna serikali?

Mwisho ni kwamba pamoja na kwamba navututiwa na sera za CHADEMA lakini sio kwamba navutiwa kwamba Slaa atawapa watanzania wali na halua au zabibu bure.

Sana sana atawapa watanzania ndoana nakuwaonyesha namna yakuvua samaki ili wapate kitoeo na SIO kwamba atawapa samaki.
 
Bill Gates anawajengea hospitali kwa sababu rais wenu kutwa anatembeza bakuli kuomba omba msaada. Badala ya kuwauliza watanzana walioko nje wanaifanyia nini nchi uliza serikali inafanyia nini kodi inayokusanya kila siku.

Ufisadi sio kujikusanyia mapesa peke yako tu, uko ufisadi wa kila aina naona katika hizo aina umo kati ya hizo aina za ufisadi.
Unaweza ukawa masikini lakini ukawa fisadi
 
Bado upo ulaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…