Richard Mlangi
JF-Expert Member
- Sep 10, 2012
- 380
- 194
Tuna majukumu mengi ya msingi sana yanayotuhusu km watanzania 2015.
Kwa ujumla 2015 ni fursa tuliyopewa na Mwenye Enzi !
A. Tuwe na msimamo mmoja kuhusu Urais. Tumuunge mkono Rais ambaye ana CV nzuri ya vitendo na kazi zinazoonekana na sio maneno. Tumkatae Rais wa kupangiwa na mtu au kiongozi mwenye maslahi binafsi, na katika hili tusiangalie vyama.
B. Tuwe na msimamo mmoja kuhusu kura ya HAPANA kwa katiba ya kina Sitta.
Tuikatae katiba hiyo kwa kuwa :
1. Inaruhusu mafisadi kuficha fedha nje ya nchi - ibara 29(2)(b)
2. Imempa Rais madaraka makubwa sana na haina separation of powers, mfano;
- Rais ni sehemu ya Bunge 129(1)
- Rais anateua Katibu wa Bunge 151(1)
- Rais anateua wabunge 15 ibara 129(2)(b)(c)
- Rais anateua Jaji mkuu 175(1)
- Rais anateua majaji 176,177
- Rais anateua mkuu wa mahakama 202 (1)
- Rais anateua tume ya utumishi 210 (1)
- Rais anateua Mwenyekiti na viongozi wa Tume ya Uchaguzi 217(2)
- Rais anateua wajumbe wa kamati ya uteuzi 218(1)
- Rais anateua Mkurugenzi wa Uchaguzi 222(1)
- Na taasisi nyingine zote ambazo ni nyeti zipo chini ya Mwenyekiti huyu wa ccm ie 225,226,243,270,273,276 nk
3. Katiba hii ina jumla ya marais 6 ibara 80,99,164
4. Pia ibara nyingi hasa zinazohusu muundo wa nchi zinakinzana ie 1(1), 75, 76, 77, 163.
C. Tukishindwa kuamua sasa au mwaka huu kuwa na msimamo mmoja bila kujali vyama vyetu basi tutaendelea kuwa na nchi isiyoeleweka na isiyo na utaifa.