Watanzania tuwe Serious na Rasilimali zetu.

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,982
45,900
Wakati sisi tupo busy na kujadili leo wema kamwambiaje zari, na diamond naye kasemaje, idris na alikiba pia na yale maji ya Ray....

Wakenya wapo busy kuimegua nchi yetu kwa propaganda kali, na wanafanya hivyo kwa kuwekeza kwa vizazi vyao...

Just imagine ile speech ya yule binti....anadai kafundishwa hivyo, that means amekua akiambiwa kuwa hizo ni mali zao...

Wameanza na Kilimanjaro tumekua kimya na sasa wameendeleza huko, na bado watalipua kwingine...

After years to come si ajabu wakaanza kudai vyao maana utakuta vizazi vyao vijavyo wamekua wakiamini kua ni mali zao...

Kama kweli tunaipenda nchi yetu...

It is time to act now...

Kuna haja ya vyombo husika kuhakikisha hili linafikia mwisho...

Huu uongo utatupeleka pabaya kama tukiacha uendelee...
 


stroke na wenzako nyie si mpo busy na siasa hamna shughuli na mali zenu, Wakenya wanazitumia vizuri.

Mlima huo hapo tena wa bure utumieni mnapiga blahblah.

Tembo hizo hapo zitumieni kuingiza pato la Taifa, hamtaki mnauwa.

Kila kitu tumepewa watanzania lkn mijitu mipumbavu ndiyo imehodhi as if ni Mali yao.

Akililess, Ujinga umewatawala
 
Waache tu waendelee kuwafundisha watoto wao, kama wakija kudai kuwa ni maeneo yao tutawaachia maana sisi tunapenda amani
 
kwani nini kimebaki ambacho unasema tuwe sirious madini gas mbuga za wanyama kote wamepewa makampun ya wazungu

wakati sisi tunagombana kuhusu zanzibar wazungu wana fanya kazi hawana sikukuu ya dini wala serikali wala hawana jmosi wala jpili
 
WACHUKUE TUNA WAO MBONA RASILIMALI NYINGI TU WAMEPEWA TENA WA MBALIKO MAJIRANI ZETU. WACHUKUE HAMNA NAMNA NAMI NASEMA WACHUKUE TU VIWASAIDIE NA WAO EEEE. WACHUKUE TU.
 
WACHUKUE TUNA WAO MBONA RASILIMALI NYINGI TU WAMEPEWA TENA WA MBALIKO MAJIRANI ZETU. WACHUKUE HAMNA NAMNA NAMI NASEMA WACHUKUE TU VIWASAIDIE NA WAO EEEE. WACHUKUE TU.
Nasubiria kusikia kauli ya Lowasa na Mbowe kuhusiana na hili
 
Kama kuna wizara na inapewa bajeti kubwa inashindwa nini kutangaza vivutio vya utalii huko nje? Wewe unasema tuliambie taifa, Diamond mwenyewe keshawahi kuzushiwa ni mkenya lakini mpaka leo hajakanusha, mi nadhani kwa mambo yanayo endelea nchi hii hata milima ingesema, kilimanjaro ungesema uko kenya kama ingekuwa ina uwezo wa kuhama kilimanjaro ungehama kabla ya kupandishwa ndege uhamishiwe usikopenda, hiyo olduvai nayo ungejichaguliwa mahali pa kwenda, maana kama kitu hakithaminiki kwao kwa nini kulia kwa kuthaminiwa na mwingine? Wem na zari wana nafasi zao hata Kenya wanafuatilia wafanyayo kina prezoo sana tu.
 
Back
Top Bottom