Watanzania tuwe makini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tuwe makini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by rugumye, Oct 30, 2012.

 1. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndugu Watanzania wenzangu baada ya kusoma tamko la Ustadhi Kondo Bungo Naibu Amir Jumuia na taasisi za kiislam Tanzania (T) Dar es salaam. Kuhusu udini hapa nchini; Ustadhi Kondo anasema kuwa suala la udini liliasisiwa na Wakoloni na kurithiwa na Mwalimu nyerere kwa kuwapendelea wakristo katika Nyanja mbalimbali na kuwabagua waislam, na pia akasema kuwa kuwa eti kwa bahati mbaya serikali zote zilizofuata ziliendeleza mfumo kandamizi ukitumia mawakala wa kanisa walioko serikalini. Suala hili lilifikia kilele katika uchaguzi uliopita ambapo viongozi wa kanisa kwa makusudi walipanga kutomuunga mkono Rais wa chama tawala katika uchaguzi huo. Na kudai kuwa kama si busara za waislam leo tungekuwa na serikali ya namna nyingine.

  Awali ya yote ningependa tujikumbushe kidogo historia juu ya Tanzania.

  DINI YA KIISLAMU ILIANZA KABLA YA UKRISTU. Historia ya Uislamu nchini Tanzania imeanza kunako miaka ya 960-1000 AD, wakati Ali ibn al-Hassan Shirazi alikuwa mmoja kati ya watoto saba wa kiume wa Shah wa Shiraz, Uajemi, mama'ke ani mtumwa wa Kihabeshi. Kufuatia kifo cha baba'ke, Ali alitimuliwa na kunyimwa urithi na ndugu zake. Kachukua jahazi lake kupitia Hormuz, Ali ibn al-Hassan Shirazi, na kikundi kidogo cha wafuasi wakafanikiwa kufanya mapumziko yao ya kwanza mjini Mogadishu, bohari la kibiashara katika pwani ya Afrika Mashariki.Miji Mikuu ya Afrika Mashariki, iliyotaliwa na Usultani wa Kilwa. Wakaendesha jahazi lao kuelekea pwani ya Afrika, Ali ibn al-Hassan Shirazi kasema anataka kununua kisiwa cha Kilwa kutoka kwa mfalme wa Kibantu aliyeitwa 'Almuli' na kuunganisha sehemu ndogo ya daraja la nchi kavu ambalo linaonekana wakati wa maji madogo. Mfalme yule alikubali kuiuza Kilwa kwa bwana Ali ibn al-Hassan Shirazi kwa nguo zenye rangirangi na hariri kwa lengo la kupendezesha kisiwa hicho. Mara baada ya kuinunua Kilwa, Washirazi wale wakaanza kuchimba daraja mpaka wa nchi kavu, na Kilwa ikawa sasa kisiwa na baadaye yakawa makao makuu ya Usultani wa Kilwa.Wakati wa umaarufu wake wa nguvu kunako miaka ya 1300-1400, Usultani wa Kilwa ukamiliki au ukadai umiliki wa miji ya bara kama vile Malindi, Sofala na nchi za visiwa kama vile Mombassa, Pemba, Unguja, Mafia, Comoros na Inhambane - kwa lengo la kutawala ambapo sasa hivi hutajwa kama Pwani ya Waswahili.Jengo ambalo la zamani na bado lipo zima Afrika Mashariki ni Msikiti wa Kizimkazi huko mjini kusini mwa Unguja tangu mwaka 1107. Inaonekana ya kwamba Uislamu ulikuwa una enea kwa haraka zaidi katika maeneo ya Bahari ya Hindi kunako karne ya 14. Wakati Ibn Battuta katembelea Afrika Mashariki mnamo 1332, ameripoti kujisikia kama yupo nyumbani kwa sababu ya Uislamu ulioenea katika maeneo hayo.

  Kawaida ya idadi kubwa ya wakazi wa pwani ilikuwa Waislamu, na Kiarabu ilikuwa lugha ya kufundishia na vilevile ya kiabishara. Bahari yote ys Hindi ilipata kuonekana kama vile bahari ya Kiislamu. Waislamu walishika hatamu katika biashara na uanzashwaji wa makazi katika pwani ya Kusinimashariki mwa Asia, India na Afrika Mashariki.Uislamu ulienea hasa kwa njia ya shughuli za kiabisha katika pwani ya Afrika Mashariki, sio kwa ushindi na uenezi wa mabavu kama jinsi ilivyokuwa huko Kaskazini mwa Afrika, na ikabaki kama pwani ya ajabu kwa muda mrefu. Wakati wa uvamizi wa mabavu wa Wareno katika maeneo ya pwani yaliyotokea mnamo karne ya 16, Uislamu ulikuwa tayari ushajikita vya kutosha karibia kila familia ilikuwa imeungamana na Uarabu, Uajemi, Uhindi na hata kuungana kisiasa na Kusinimashariki mwa Asia na baadhi ya sehemu za kaskazini na mashariki mwa Bahari ya Hindi.

  Mwishoni mwa karne ya 17 na mwanzoni mwa karne ya 18, Waislamu wa pwani waliweza kuwatimua Wareno kwa msaada wa
  Oman. Waomani wakaongeza athira ya kisiasa hadi hapo mwishoni mwa karne ya 19 ambapo Wazungu walipoanza kuwasili katika pwani ya Afrika Mashariki.Wakati wa Oman inatawala pwani hiyo kisiasa, uenezi wa wa Uislamu uliongezeka pia ndani ya Afrika Mashariki. Mawasiliano ya kibiashara na watu wa ndani, hasa Wanyamwezi, na kuanza kupewa umuhimu kwa sehemu kama za Tabora katika maeneo yenye Wanyamwezi na Ujiji katika Ziwa Tanganyika ikawa kitovu kikuu cha uongezaji wa biashara ya utumwa na pembe za ndovu.Machifu wengi, hata sehemu za Uganda, wamesilimu na kuwa Waislamu na kuanza kushirikina na Waislamu wa pwani. Biashara ya utumwa haijasaidia kueneza Uislamu tu, bali pia lugha ya Kiswahili na tamaduni ya Waswahili. Kabla kuanzishwa kwa Afrika Mashariki ya Kijerumani kunako miaka ya 1880 athira za Waswahili zilikuwa na kikomo hasa waliishi katika maeneo yao tu walioyazoeaHivyo waislamu wanapaswa kulaumu mfumo wa dini yao kwaani kama ni elimu wao ndiyo wangekuwa mbali kuliko hata wakristu. Lakini kwa bahati mbaya waarabu walijenga miskiti kwa ajili ya ibada bila kuangalia huduma nyingine za jamii kama afya na elimu. Baada ya uhuru waislam ama hawataki kujua tatizo lilipo au wanafanya makusudi kuwa na chukia kwa wakristu.

  Wameshonari kutoka ulaya walianza kuja Tanganyika baada ya mkutano wa Berin 1884, Kuhusu hoja ya Mwalimu Nyerere kuwapendelea wakristo: Ndugu waislamu tuwe wakweli, hivi mwalimu Nyerere angekuwa na upendeleo kwa wakristu waislamu wangesoma wapi? Mwalimu Nyerere kujua kuwa kulikuwa na tatizo alibinafsisha shule zote za misheni hata za wakatoriki wenzake, mfano ni shule alizowahi kifundisha Pugu na Milambo ya Tabora iliyokuwa inaitwa ST. MARYS Ili waislamu wapate elimu sawa na wakristu. Hilo waislamu hawataki kuliona. Baada ya uhuru waislamu wangapi walikuwa na elimu ya juu au ni shule ngapi zilizo achwa na Mwarabu aliyetawala Tanganyika kwa muda mrefu? Au baada ya uhuru waislamu wamejenga shule ngapi kwa ajili ya kutoa elimu ya kawaida? Katika mfumo wa elimu baada ya uhuru wanafunzi walichaguliwa kwa kufaulu mitihani na si kwa majina, je waislamu walitaka wapewe shule za kusoma pekee yao? Suala la viongozi wa kanisa kwa makusudi kupanga kutomuunga mkono Rais wa chama tawala katika uchaguzi 2005 na 2010: Kwa kumbukumbu zangu katika uchaguzi wa mwaka 2005 maaskofu walitoa tamko kuwa mgombea kupitia CCM Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alikuwa ni chaguo la Mungu. Tatizo la waislmu ni kutojitambua kama wanatumiwa na Chama tawala CCM hasa wakati wa uchaguzi kupitia bakwata.

  Hitimisho: waarabu na wazungu wote walituachia madhara, mwarabu alifanya biashara ya utumwa na alituuza kama bidhaa na kutuachia uislamu, Mzungu alitunyonya sana na kutuachia ukristu. Mababu zetu hawakuwa na madhehebu haya mpaka wageni walipokuja. Tuvumiliane kwa yote tukipigana kwa sababu ya udini hakuna tutakachopata. Kama kuua ni dhambi mwarabu aliwaua babu zetu wengi sana hasa walipokaidi kukamatwa utumwa. Mzungu pia aliua waafrika wengi sana wakati wa vita za kugombania rasilimali zetu.
   
 2. doup

  doup JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Yote umemaliza, hakuna cha Mzungu na ukristo wake wala mwaraabu na uislam wake,wate wametunyanyasa sana, kama kweli tungekuwa na hasira nao hizo dini tungezitosa siku nyingi.

  kwa ujinga wetu, miafrica, hasa mi-tanganganyika na ma-zanzibar ndio yanajidai utafikili yalikuwepo siku ya kuweka jiwe la msingi makka, au pale vatican.

  hawapati uchungu na vitu vya msingi kwa maslai ya taifa na mustakhabari wa vizazi vyao.
  nguvu hii ingetumika katika kutafuta maendeleo na kuelimisha watu tungekuwa mbali
   
 3. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  well said mkuu
   
 4. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ustadhi kondo ana elimu gani??
   
 5. G

  Gene Senior Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ELIMU YAKE PLEAAAASE..... Atuchangiii mada za.........
   
 6. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Waafrika hatuzano kama waarabu. angalia waarabu wanavyokubali kuingia kwenye mitego na kuuana wao kwa wao. wanalipuana ndugu kwa ndugu. sasa hawa wenzetu bongo wanasema eti Tanzania imetawaliwa na mfumo kristu. wakati kuanzia Rais, makamu wa Rais, Jaji mkuu, mkuu wa jeshi la polisi na mkuu wa usalama wa taifa na nk. lakini mimi sioni tatizo wao kuwa viongozi kwaani cha msingi wanadeliver?
   
Loading...