Watanzania tutakuwa jiwe la chumvi!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tutakuwa jiwe la chumvi!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mageuzi1992, Oct 1, 2012.

 1. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wahenga walisema mkataa pema pabaya panamwita!

  Msemo huu una maana kubwa sana katika jamii na hasa Watanzania wa leo. Ni kipindi kirefu sana Watanzania wamekuwa wakilia maisha magumu,umaskini,shida,hali ngumu,njaa,kukosa kazi,mfumuko wa bei,gharama kubwa za shule,tunakwenda wapi,nchi inayumba,Serekali imeshindwa kazi,hatuna seikali,CCM haifai n.k Swali ni nani aliyewafikisha Watanzania hapo jibu rahisi ni serikali ya chama tawala!!!

  Ajabu ni kwamba pamoja na yote hayo bado watanzania wameshindwa kukubali mabadiliko ya kweli na kukumbatia chama hicho.
  Kuna hata watanzania ambao walienda upinzani lakini baada ya muda wamerudia matapishi yao!!! ajabu hii! Kitu kibaya ni kwamba watanzania wanamlilia Mungu tusaidie lakini wao wanashindwa kupokea ule usaidizi!! Ajabu hii Wana waisrael Walipata Shida sana utumwani MISRI wakalia sana Mungu akawaletea ukombozi kwa kuwapa watu wakuwaongoza kuwatoa utumwani. Lakini kutokana na ugumu wa mioyo yao, na imani finyu pamoja na kutaka mafanikio ya haraka wakatamani kurudi MISRI. Hii ni sawa na Watanzania ambao wamelia sana na Mungu kawaletea watu wakuwakomboa na Utumwa wa SISIM=MIsri.

  Wao wanatamani kurudi utumwani MISRI eti walikuwa wakila na kusaza=ufisadi!!! HADITHI YA MKE WA LUTU INAFANANA PIA NA WATANZANIA......MKE WA LUTU ALIAMBIWA ASITAZAME NYUMA KWA KUA ALIKOTOKA NI KUBAYA KUNA WATU WABAYA KAMA VILE MAFISADI,WAZINZI,WATESAJI,WASIOPENDA WENGINE WAROHO N.K SASA MKE WA LUTU KWA TAMAA AKATAZAMA NYUMA NA TAZAMA AKAGEUKA JIWE LA CHUMVI...naonya watanzania wanaotazama nyuma badala ya mbele chonde chonde mtageuka jiwe la chumvi!!
   
Loading...