Watanzania tusizoee bunduki

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,428
13,936
Nadhani matumizi ya bunduki na kutishiana bunduki haukuwa utamaduni wetu na haupaswi kuwa utamaduni. Kila mtu atumie nguvu zake zote na njia zote kuulani. Hatufai, hafai na alaaniwe kabisa anayetaka bunduki zigeuke matoi ya kutishiana hadharani hata pale pasipohitajika. Utamaduni huu ulizitesa na unazitesha hadi leo nchi nyingi duniani.
 
Kwani huko unakoishi ushakutana na bunduki ngapi, ukiachilia kuzisikia
nimeziona na kusikia eti watu wamevamia na kuonyeshana bunduki, lakini eti ni mwiko kusema kuwa nimeona mtu kamtishia mwenzake kwa bunduki.
 
nimeziona na kusikia eti watu wamevamia na kuonyeshana bunduki, lakini eti ni mwiko kusema kuwa nimeona mtu kamtishia mwenzake kwa bunduki.
Vizuri,

Si kila unokiona na kukisikia chafaa kukisema,

Mnunue plasta muwe mnatembea nazo mfunge midomo yenu,.

Mfanye kazi jamani,
 
Nadhani matumizi ya bunduki na kutishiana bunduki haukuwa utamaduni wetu na haupaswi kuwa utamaduni. Kila mtu atumie nguvu zake zote na njia zote kuulani. Hatufai, hafai na alaaniwe kabisa anayetaka bunduki zigeuke matoi ya kutishiana hadharani hata pale pasipohitajika. Utamaduni huu ulizitesa na unazitesha hadi leo nchi nyingi duniani.

..kuna siku bwana mmoja alivaa mavazi ya kivita ya jwtz.

..baadhi yetu tukakemea kwamba huyu ni raia kwanini anavaa mavazi ya kivita? Tena hata watangulizi wake hatukuwaona wakivaa mavazi ya jeshi ya kivita.

..tuliona hatari huko mbeleni kwa hulka tabia na mienendo yake atakuja kuwa mtegemezi(addicted) kwa vyombo vya usalama. Kwamba badala ya kushawishi wananchi kwa hoja atakuwa akiwatisha kwa mabavu ya kijeshi.

..kilichomtokea Nape siyo tukio la kwanza. Kuna waandishi wa habari walishambuliwa mkoani Geita na askari waliovaa kiraia.
 
Back
Top Bottom