Tuwaseme
JF-Expert Member
- Oct 8, 2014
- 645
- 1,191
Habari zenu wanaBodi,
Kilichomtokea aliyekuwa Waziri wa Michezo na Mbunge wa Mtama, Mh. Nape Nnauye, kwa mtazamo wangu sio ushujaa, bali ni matokeo ya siasa zake chafu katika Nchi hii ama kwa lugha nyepesi kilichomtokea tunaweza sema ni ajali kazini.
Kama mtakumbuka vizuri wakati wa Uchaguzi Mkuu 2015, Nape amehusika kwa kiwango cha Lami kutuletea huyu kiongozi aliyepo sasa, Rais Magufuli. Kwa hiyo sasa hivi wanavyotumbuana ni haki yao. Ni sawa na kusema acha wafu wazikane.
Nchi hii ina Mashujaa wengi wa kuitwa Mashujaa lakini Sio Nape. Mimi ni MwanaCCM lakini nilitambua wazi katika uchaguzi Mkuu, kuwa Rais Magufuli hafiti kuwa Rais. Uwezo wa Rais Magufuli mwisho ni kwenye ngazi ya Uwaziri.
Rais Magufuli hafiti hata ngazi ya Uwaziri Mkuu. Lakini nilishangaa kuona Vita yake binafsi na Lowassa ndiyo ilimfanya amuone Magufuli bora kuliko Lowassa (Mm sio Team Lowassa). Kwa hiyo anachokipitia Nape kwa sasa sio Ushujaa ni Matokeo ya Matendo yake.
Kama hiyo haitoshi, hivi ni kweli leo Watanzania tumesahau kuwa Nape ndiye alieondoa Bunge Live. Hata kama alikuwa ameamrishwa na Rais. Basi Ushujaa wake ungeanza wakati ule, angekataa kuondoa Bunge Live.
Japo siungi mkono vitendo vya Makonda lakini kwanini ushujaa wa Nape uanze sasa kwenye Sakata la Makonda? Kwanini hakuwa Shujaa kwenye Bunge Live?
Tafsiri yake ni kwamba, Nape ni Kiongozi wa kubadilika badilika. Mara anaunga mkono uovu (Kuondoa BungeLive), Mara anapinga uovu (Ishu ya uvamizi wa Makonda). Kwa hiyo tunashindwa kujua hasa rangi ya Nape ni ipi.
Hatutaki Mashujaa wenye ndimi mbili.
------------

Nashangilia yaliyokukuta Comrade Nape Moses Nnauye, nitashangilia milele..
Kabla ya Uchaguzi wa mwaka 2015, ulikuwa ukitumika kama Katibu wa Itakadi na Uenezi wa Chama chama cha Mapinduzi. Katika nyakati hizo pengine tuliokupenda ni sisi wanachama wa chama cha Mapinduzi, na watu wachache wasio na chama. Kwa wale wasiopenda CCM wewe ulikuwa adui Mkubwa.
Nakumbuka ulivyokuwa unawapa shida wapinzani, kiasi cha wengi kukuona wewe ni kiumbe aliyejaa kiburi na dharau. Sitasahau siku moja ulikuwa kwenye kipindi kimoja cha Star Tv, ambapo ulikuwa unalumbana na Rais wa TLS, ndugu Tundu Lissu. Ulionekana ukicheka kwa dharau, huku ukikuna shingo kana kwamba Tundu Lissu anaongea 'utumbo'. Hiyo ilikuwa sura uliyowaonyesha wapinzani siku zote. Nani atasahau kauli yako kwamba wanaohama CCM ni [HASHTAG]#MafutaMachafu[/HASHTAG]? na nani atasahau kwamba utapigana vyovyote ili [HASHTAG]#CCM[/HASHTAG] iingie madarakani hata kwa [HASHTAG]#GoliLaMkono[/HASHTAG].
Baada ya wewe kushinda Uchaguzi wa jimbo la Mtama, baadhi ya watu walianza kusema Rais atakosea kukupa Uwaziri kwa sababu wewe ni 'mropokaji'. Iliwashangaza ulipoteuliwa kuwa Waziri. Utendaji wako uliwashangaza wengi na waliokuwa wanakuona mropokaji walishangazwa na busara zako. Siku hadi siku umezidi kuwa kipenzi cha watu, na hata wale adui zako wamekuja kukuelewa na kujua wewe ni Kiongozi wa kweli.
Mimi najivunia maisha uliyoishi katika nafasi zote mbili : kiburi wa CCM, na Waziri shujaa mwenye busara tele.
Nafasi yako CCM ilikuhitaji kuwa vile na uliitumikia. Kama ungekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi kisha wapinzani wakupende ulipaswa kuondoka. Ile ilionyesha kwamba uko tayari kutofautiana na watu ili usimamie ITIKADI.
Uwaziri ulikuhitaji kuwaunganisha Watanzania. Hilo ulilifanya, ulisimama upande wa watu. Wapinzani wenye nia njema walikuelewa, na wengi waliokuwa wanaokuwa hawana imani na wewe walibadilika kuwa wafuasi wako. Bado naiona picha yako ukihangaika kukamata wezi wa kazi za wasanii kule Kariakoo, na bado nakuona unavyohangaika kwenye viwanja vya Michezo kuinua hata michezo ya mchangani. Nakuona ukiwa [HASHTAG]#VIP[/HASHTAG] ya Fiesta pale Dodoma na kisha ukapanda jukwaani, na nakuona ukipiga gitaa kwenye majukwaa mbalimbali. Nakuona ukitembelea vyombo vya habari kuomba maoni yao kuhusu kanuni zinazoihusu Tasnia, kisha nakuona ukijivika Bomu baada ya uvamizi wa [HASHTAG]#CloudsMediaGroup[/HASHTAG].
Kwanini nashangilia? : Umeondoka katika wakati ambapo [HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG] inafahamu uwezo wako na uthubutu kama kiongozi. Kama ambavyo ulikuwa tayari kutumia kila mbinu dhidi ya Wapinzani ili utetee ITIKADI YA CHAMA, ndivyo ambavyo umekuwa tayari hata kutofautiana na SERIKALI kwa maslahi ya wengi.
Nape, wapo Mabondia wengi watajuta mpaka kufa kwao kwa sababu wakati wanastaafu hawakuwa na mikanda ya Ubingwa. Lakini ni furaha ya Milele kwa bondia kustaafu akiwa na Mikanda yake ya ubingwa.
Ubingwa uko kwako, ningeumia sana kama ungeendelea kuwa Waziri halafu uharibu imani Watanzania tuliyokupa. Lakini umeondoka tukiwa na imani ya kiwangi cha juu zaidi kwako. NASHANGILIA NAPE UMEONDOKA ULINGONI UKIWA NA MIKANDA YAKO.