Watanzania tusikubali dhuluma hii ya serikali

Mkulima wa Kuku

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,270
533
Mgomo na maandamano yanapaswa kuwa silaha ya mwisho kabisa kwa watawala wasiosikia kelele za vilio vya uchungu wa watu wao. Na sasa nashawishika kuwa kuna haja ya kuandamana na kuigomea serikali yetu. Kwanini?

1. Wiki iliyopita kumekuwa na uprise kubwa ya soo la bei ya mafuta na kusababisha uchumi wa nchi kuyumba kwa kiasi kukubwa. Wakafanya usanii wa kushusha bei ya mafuta ambayo baadaye iligomewa na wafanyabiashara na wakakataa kuuza mafuta yenyewe. Mpaka sasa (labda kwa tangazo la bei mpya leo) hakuna diesel.

2. Serikali imekuwa ikitufanya makanyagio yake na kutukandamiza hata pale inaposhindwa kuwajibika. Wametaka bei ya mafuta ishushwe, wafanya biashara wamekataa kwa hiyo sasa mlaji ambaye ni mwananchi amerudishiwa mzigo kwa kisingizio cha kushuka kwa thamani ya shilingi ukilinganisha na dola. Ni mtanzania mwenye umbumbumbu wa akili tu atakayekubaliana na hoja hii kwani serikali ilichotaka kufanya ni kutii maagizo ya wale waliowapa fedha za kuingia madarakani (wauza mafuta), inataka kuhamishia mzigo kwa mwananchi.

Tutahujumiwa mpaka lini? Watanzania wenzangu hamlioni hilo? Maandamano ni lazima yakafanyike New York wakati waumiaji wako hapa? Imefika wakati tuingie mitaani na kugomea hali mbaya ya maisha hata kama watatuua wachache kwa ajili ya wengi hatimaye ukombozi utawafikia wanaobaki.
Naomba kutoa hoja.
 
Back
Top Bottom