TUKANA UONE
JF-Expert Member
- Jan 3, 2018
- 2,842
- 8,598
Kumekuwa na tatizo kubwa mno ambalo limejengeka miongoni mwa watanzania, kutokusema ukweli kwa kudhani wakisema ukweli watamuumiza mtu fulani. Hili limepelekea kuwa na taifa la watu wajinga kila leo.
1. Unaingia kwenye duka kununua bidhaa na hiyo bidhaa hujaipenda ila kwakutaka kumridhisha mwenye duka au kutomkatisha tamaa unaamua kuinunua hiyo bidhaa na ukifika nyumbani unaanza kuugulia maumivu ndani kwa ndani na kubaki kusonya tu, kwanini usimwambie muuzaji hiyo bidhaa hujaipenda na hujavutiwa nayo? Pesa yako halafu unakubali vipi ikupe Taabu?
2. Unapigiwa simu ama na rafiki yako, mpenzi wako au ndugu yako anakuomba hela, wewe unajua kabisa kwa wakati huo huna hela ila kutaka kumridhisha unaamua kumdanganya ya kwamba akucheki baadae utampatia.
Akikucheki baadae unaanza kusonya na kutopokea simu ukianza kulalamika kwamba huyu fulani naye ni msumbufu, utapigiwa simu sana na hutopokea ng'o kwasababu uliahidi uongo. Kwanini useme uongo? Kwani ukisema huna pesa kwa wakati huo utakufa? Mwambie huyo mtu huna fedha na acha kudanganya danganya kijinga kwamba kuna mtu umetoka kumpatia pesa muda si mrefu. Acha uongo wewe mwambie ukweli huna pesa na utakuwa huru.
3. Unaishi na mtu au ndugu nyumbani kwako au gheto kwako na humtaki kwanini usimwambie aondoke? Badala yake utatoka hapo utaenda kumteta kwa ndugu au marafiki zako ya kwamba unaishi na fulani kwako na humtaki kwakuwa amekuwa na tabia za kula tu bila kufanya kazi au kufanya jambo ambalo hulitaki na kibaya hao watu unaowaambia wanabaki kukwambia umfanyie visa ili aondoke mwenyewe!
Hizi tabia za kijinga mtaacha lini? Kwanini usimwambie kwamba kwa tabia zake ambazo hazikufurahishi afungashe virago vyake aondoke? Yaani unashindwa kumwambia aondoke wewe unabaki kusonya tu na kununa kimoyo moyo, mwambie ukweli. Sema ukweli ili ubaki huru kuliko kufura kama chura.
4. Wewe unamiliki chombo cha moto na watu wako wa karibu wanakuazima kila uchwao na wewe huwanyimi ila hutaki kuwapa, sasa ili kuepusha lawama unajikuta unawapa hivyo hivyo kishingo upande, kwanini uumie?
Kwanini usiwaambie ukweli kwamba sitaki kutoa gari yangu au pikipiki kwasababu ya huwa hamjali mnaendesha hovyo hovyo? Utaendelea kuvumilia maumivu hadi lini? Badala uwaambie ukweli wewe unabaki kusonya na kununa, kibaya zaidi watu wenyewe ukiwapa chombo hawaweki hata mafuta wanarudisha chombo kikiwa kimekaukiwa na mafuta wakitegemea wewe uweke wao waendeshe. Waambie ukweli acha uoga wa kijinga utakugharimu.
5. Uko sehemu na kuna mtu anawaambia jambo fulani na unajua kabisa hilo jambo ni uongo kabisa, wewe badala ukanushe palepale kwamba hilo jambo ni uongo wewe unakubali kabisa na ukishatoka hapo ndiyo unaanza kuzungumza na wenzio kwamba yule bwana ametudanganya kwasababu ukweli ni huu! Kwanini hukumchana makavu ili huyo mtu aelewe na asiendelee kuwadanganya wengine?
Hebu tubadirike tuache uoga, ukweli usemwe na utatuweka huru. Kwenye ukweli inapaswa tuseme ukweli ili watu wabadilike.