Watanzania tuongee hapa bila kuwa na mihemko!!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,751
9,002
Nimeona kuna vitu vimetrend katika mitandao hapa nchini.
1.Ni la.Mh Rais wa Jamuhuri wa Tanzania,
Dr John P.Magufuli kuteua tume iliyochunguza mchanga gafi uliokuwa ukipelekwa nje kwa ajili ya kuchenjuliwa,ambapo kamati ilikuja na mapendekezo, na Mh Rais akapiga marufuku kupeleka mchanga nje .

2. Ni juu ya uteuzi wa Kamanda Siro kuwa IGP.

Watanzani tufike mahali tuwe postive katika maswala ya msingi.

Mh Rais kupiga marufuku mchanga ni kwa ajili ya ya watanzania na sidhani ni kwa maslahi yake binafsi,ikumbukwe tulikuwa tukioiga mayowe kuhusu huu mchanga hadi tukasema hata wakiweka madini hatuwezi kufahamu!pili tukasema hadi ndege zipigwe marufuku kuingia kule mchimboni!.

Sasa leo inakuwaje tunalalamikia hili???

Swala la teuzi

Hili ni swala la mamlaka maana wanateuliwa na Rais kwakumsaidia kazi anapoona hanaitaji kubadilisha haiitaji mjadala hivyo hili swala tuliachie mamlaka.

Lengo

Maoni yako ni yapi au wewe ulishauri vipi.
 
Hili ni swala la mamlaka maana wanateuliwa na Rais kwakumsaidia kazi anapoona hanaitaji kubadilisha haiitaji mjadala hivyo hili swala tuliachie mamlaka.
Naelewa Kiswahili kilivyo kigumu kijana [B]KakaKiiza[/B], lakini unasemaje kuhusu Marais waliotangulia? Je na wao walikuwa na haki kama hii unayodai kwa Magufuli? Kama walikuwa na haki ya kutenda watakavyo bila kuhitaji mjadala, kwa nini Magufuli analalamikia maamuzi waliyoyafanya hadi tukajikuta hapa tulipo? Je tusubiri hadi huyu naye atakapostaafu ndio tuanze kulalamikia mapungufu yake ya kukurupuka hovyo na kulinda mabashite? Je hapa Tanzania, kulingana na Katiba, mwenye maamuzi ya mwisho ya hatma ya nchi ni Magufuli au wananchi? Wabeja baba!
 
Uongozi unamabo makuu matatu..
■Uweledi
■Utashi binafsi na uthubutu
■Uwajibikaji
Yawezekana waliotangulia hawakuwa na hivi vitu vitatu katika uongozi sasa leo Mh Raisi ameamua kiwa na utashibinafsi,Uwajibikaji na uweledi na ndiyo maana kwa uweledi alitambua kuwa mchanga unaondoka na mali za watanzania,ndiyo maana kwakutumia uweledi akajua scanner inaharibiwa na makontena yanapita bila kulipiwa ushuru!kwa uweledi ule ule akaona airport camera na scanner viharibiwa makusudi ili wizi uendelee,na kwa utashi na uwajibikaji akaenda muhimbili nakuwambia watumishi waende wizarani hapo akina mama wapewe mahali pakulala na kuagiza vitanda vikaja na leo tumeona wenyewe ila kuna maraisi wamepita katika Awamu hizo sitaki kuwazungumzia ila nimekupa vitu vitatu katika uongozi ila siku zote uthubutu ndiyo kitu cha msingi.
 
Katiba irekebishwe ili rais ashitakiwe akifanya makosa akiwa madarakani, hii itapunguza kufanya mikataba ya kijinga kama hii. Bila ya kubadilishwa kifungu cha rais nae ashitakiwe kwa makosa basi na huyu atayafanya kama watangulinzi wake.

Ndukiiiii
 
Kwanin huyu mwenye utashi na uthubutu wa kugusa ambavyo wastafu walishndwa ni muoga wa kukosolewa? Kwanin kila jambo anapenda yeye aonekane ndio mzalendo. Tmeshuhudia akiwabana wapnz ktk kufanya siasa, tnashuhudia double standard kubwa. Ktokana na haya nakuwa mgumu sana kuamin kama kwel mkuu ana nia njema kwa taifa.
 
Mi bado Nina muhemko!
Ngoja niwaachie hao ambao hawana mihemko kama ulivyosema
 
Watu mnajua kupotosha mambo!!

Hivi ni mwendawazimu gani anaweza kupinga hatua ya kunusuru mali zetu!!!

Watu wanachosema ni kwamba let's be smart katika kushughulikia hili suala na sio kufanya tu ili eti uonekane mzalendo!!

Tusijitie upofu, hii nchi tumeshalipa mabilioni mengi sana kwa kesi za kijinga jinga kama hizi!!!

Pamoja na kwamba Richmond ni utapeli mtupu lakini kila tukisimama nao mahakamani tunapigwa za uso!!!

Hivi kwa mfano, kulikuwa na sababu gani za msingi za kutowashirikisha ACACIA kwenye ule uchunguzi!!!

Hivi utasimama kwenye mahakama gani duniani kutetea uchunguzi uliofanyika bila kuhusisha upande wa pili?!!
 
Kwanin huyu mwenye utashi na uthubutu wa kugusa ambavyo wastafu walishndwa ni muoga wa kukosolewa? Kwanin kila jambo anapenda yeye aonekane ndio mzalendo. Tmeshuhudia akiwabana wapnz ktk kufanya siasa, tnashuhudia double standard kubwa. Ktokana na haya nakuwa mgumu sana kuamin kama kwel mkuu ana nia njema kwa taifa.
Unajua kuna nadharia watu wamekuwa nayo siko zote na ujue nchi ya tanzania kwa sasa inajikomboa katika mikono ya wezi wakubwa waliotumia usomi kuididimiza na kuitoa kwa sasa haiitaji majukwaa kwani ya taturudisha katika mambo ndiyo mzee kule kwetu tunasema mambo ya (Tatamshanage) hivyo tufanye siasa za kawaida huku tukinyanyua nchi hata Hayati Mzee wetu Karume alifanya haya anayoayafanya Mh Rais Magufuli nenda michenzani uone sasa hivi ni nchi kwanza siasa 2020.
 
Katiba irekebishwe ili rais ashitakiwe akifanya makosa akiwa madarakani, hii itapunguza kufanya mikataba ya kijinga kama hii. Bila ya kubadilishwa kifungu cha rais nae ashitakiwe kwa makosa basi na huyu atayafanya kama watangulinzi wake.

Ndukiiiii
Point
 
Nakuunga mkono Kakakiiza

mi sielewi tunaenda wapi watanzania.

Kila linalofanywa tunaponda tu

ni ngumu sana kuongoza watanzania.
 
Watu mnajua kupotosha mambo!!

Hivi ni mwendawazimu gani anaweza kupinga hatua ya kunusuru mali zetu!!!

Watu wanachosema ni kwamba let's be smart katika kushughulikia hili suala na sio kufanya tu ili eti uonekane mzalendo!!

Tusijitie upofu, hii nchi tumeshalipa mabilioni mengi sana kwa kesi za kijinga jinga kama hizi!!!

Pamoja na kwamba Richmond ni utapeli mtupu lakini kila tukisimama nao mahakamani tunapigwa za uso!!!

Hivi kwa mfano, kulikuwa na sababu gani za msingi za kutowashirikisha ACACIA kwenye ule uchunguzi!!!

Hivi utasimama kwenye mahakama gani duniani kutetea uchunguzi uliofanyika bila kuhusisha upande wa pili?!!

Muanzisha thread na watu wengine walio in love na Magufuli watapita hii post
kama hawaioni
 
Ndio Rais kajitahidi.Lakini tunachoshauri ni kutibu chanzo cha tatizo. 1.Sheria zetu za madini zinawapa wawekezaji kiasi kikubwa kuliko wenye mali.
2. Waliouza Nchi kwa wawekezaji wapo,lakini hawachukuliwi hatua kwa kusaini mikataba ya ovyo.eg Karamagi na Buzwagi yake.
3.Rais atusikilize wananchi wake, tunataka mikataba hii irudi bungeni na kujadiliwa kwa uwazi.
 
Naelewa Kiswahili kilivyo kigumu kijana [B]KakaKiiza[/B], lakini unasemaje kuhusu Marais waliotangulia? Je na wao walikuwa na haki kama hii unayodai kwa Magufuli? Kama walikuwa na haki ya kutenda watakavyo bila kuhitaji mjadala, kwa nini Magufuli analalamikia maamuzi waliyoyafanya hadi tukajikuta hapa tulipo? Je tusubiri hadi huyu naye atakapostaafu ndio tuanze kulalamikia mapungufu yake ya kukurupuka hovyo na kulinda mabashite? Je hapa Tanzania, kulingana na Katiba, mwenye maamuzi ya mwisho ya hatma ya nchi ni Magufuli au wananchi? Wabeja baba!
Sasa kama kuna mapungufu nyuma basi mazuri yasifanywe?? Magufuli yuko sahihi kwa hili ilipendeza sana tungemuunga mkono na kumtia moyo.

Lakini pia kumbuka rais ni mwakilishi wa wananchi anafanya kwa niaba ya wananchi.

Hivi utawapaje wananchi watoe maoni yao huku kukiwa na kelele nyingiiiiii...itapigwa kura ama??
Uongozi unamabo makuu matatu..
■Uweledi
■Utashi binafsi na uthubutu
■Uwajibikaji
Yawezekana waliotangulia hawakuwa na hivi vitu vitatu katika uongozi sasa leo Mh Raisi ameamua kiwa na utashibinafsi,Uwajibikaji na uweledi na ndiyo maana kwa uweledi alitambua kuwa mchanga unaondoka na mali za watanzania,ndiyo maana kwakutumia uweledi akajua scanner inaharibiwa na makontena yanapita bila kulipiwa ushuru!kwa uweledi ule ule akaona airport camera na scanner viharibiwa makusudi ili wizi uendelee,na kwa utashi na uwajibikaji akaenda muhimbili nakuwambia watumishi waende wizarani hapo akina mama wapewe mahali pakulala na kuagiza vitanda vikaja na leo tumeona wenyewe ila kuna maraisi wamepita katika Awamu hizo sitaki kuwazungumzia ila nimekupa vitu vitatu katika uongozi ila siku zote uthubutu ndiyo kitu cha msingi.
 
Kwanin huyu mwenye utashi na uthubutu wa kugusa ambavyo wastafu walishndwa ni muoga wa kukosolewa? Kwanin kila jambo anapenda yeye aonekane ndio mzalendo. Tmeshuhudia akiwabana wapnz ktk kufanya siasa, tnashuhudia double standard kubwa. Ktokana na haya nakuwa mgumu sana kuamin kama kwel mkuu ana nia njema kwa taifa.
Nadhan hakuna siasa za kufanya kwa sasa,,kama watu wenyewe ndiowale wakuongelea mambo ya kenya kana kwamba ya hapa yamekwisha ni afadhal alishtuka mapema kupiga marufuku
 
Watu mnajua kupotosha mambo!!

Hivi ni mwendawazimu gani anaweza kupinga hatua ya kunusuru mali zetu!!!

Watu wanachosema ni kwamba let's be smart katika kushughulikia hili suala na sio kufanya tu ili eti uonekane mzalendo!!

Tusijitie upofu, hii nchi tumeshalipa mabilioni mengi sana kwa kesi za kijinga jinga kama hizi!!!

Pamoja na kwamba Richmond ni utapeli mtupu lakini kila tukisimama nao mahakamani tunapigwa za uso!!!

Hivi kwa mfano, kulikuwa na sababu gani za msingi za kutowashirikisha ACACIA kwenye ule uchunguzi!!!

Hivi utasimama kwenye mahakama gani duniani kutetea uchunguzi uliofanyika bila kuhusisha upande wa pili?!!

Hivi kweli mwizi ashirikishwe kwenye uchunguzi unaomuhusu??

Sijawahi ona toka nizaliwe.

Naonaga watuhumiwa huwa wanaondolewa kupisha uchunguzi
 
Uongozi unamabo makuu matatu..
■Uweledi
■Utashi binafsi na uthubutu
■Uwajibikaji
Yawezekana waliotangulia hawakuwa na hivi vitu vitatu katika uongozi sasa leo Mh Raisi ameamua kiwa na utashibinafsi,Uwajibikaji na uweledi na ndiyo maana kwa uweledi alitambua kuwa mchanga unaondoka na mali za watanzania,ndiyo maana kwakutumia uweledi akajua scanner inaharibiwa na makontena yanapita bila kulipiwa ushuru!kwa uweledi ule ule akaona airport camera na scanner viharibiwa makusudi ili wizi uendelee,na kwa utashi na uwajibikaji akaenda muhimbili nakuwambia watumishi waende wizarani hapo akina mama wapewe mahali pakulala na kuagiza vitanda vikaja na leo tumeona wenyewe ila kuna maraisi wamepita katika Awamu hizo sitaki kuwazungumzia ila nimekupa vitu vitatu katika uongozi ila siku zote uthubutu ndiyo kitu cha msingi.
Niruhusu na mimi nikueleze uongozi unahitaji nini...Uongozi ni suala la busara, uaminifu, utu, ujasiri, na nidhamu vyote kwa pamoja. Kwa bahati mbaya Rais wetu Magufuli sifa pekee aliyo nayo labda ni ujasiri na utegemezi wa hiyo peke yake matokeo ni utawala wa kibabe (udikteta uchwara)

Kila aina ya fadhila iliyotajwa katika hizi tano ni muhimu na sahihi kwa kazi yake na kiongozi mzuri anatakiwa awe nazo zote. Kichwa cha habari kama uivyoitoa hapo juu, ni ujumbe mzuri ambao ilitakiwa uuelekeze kwa Rais Magufuli...afuate sheria na taratibu, asiwe na mihemuko na aache kukurupuka.
 
Back
Top Bottom