Watanzania tunasubiri Mkapa na Kikwete watoe kauli kuhusu Makinikia!!

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
5,279
2,000
Kamati zote 2 zilizoundwa na Mhe.Rais JPM na kutoa taarifa zenye kuanika uoza wa Mikataba ya Madini a.k.a Makinikia tangu 1998 ni wakti mwafaka sasa kwa waliokuwa Marais katika awamu husika kujitokeza na kutoa neno. Hawa ni Ben William Mkapa( 1995-2005) na Jakaya Mrisho Kikwete(2006-2015).Maana hapa ilipofikia sasa hii imeanza kukolea moto na muda si mrefu tutaanza kusikia miripuko ya hapa na pale!!

Inashangaza kuona taarifa ya Kamati ya Prof. Ossoro ikipendekeza kuchukuliwa kwa hatua kwa wote waliohusika na Mikataba hii mibovu wakiwemo Mawaziri/Manaibu Waziri katika Wizara ya Nishati na Madini, Wanasheria Wakuu wa Serikali na Viongozi wa TMAA na taasisi zinazohusika na Madini katika Awamu ya 3 ana ya 4.

Hii vita aliyoitangaza Rais JPM ni vita kali ya Kiuchumi na hata yeye amekiri hii vota siyo lelemama na awe kweli amejiandaa. Waswahili walisema ukitaka KUUA NYANI wanaoingia kula mahindi shambani usiwaangalie usoni.Kama JPM amedhamiria kupambana vita hii basi tunaomba aanze na Mzee Mkapa aliyemwingiza kwenye Ubunge na kumpa Uwaziri wa Ujenzi katika awamu yote ya 3. Akimaliza na Mkapa aje kwa Mzee Kikwete aliyemkabidhi Ikulu mwaka 2015!

Lakini wakti JPM akijaribu kuwakomalia Watangulizi wake, lazima naye ajitathmini kama anastahili kupigana hii vita na yeye ni msafi kiasi gani!! Hili ni angalizo kwa JPM. Kwamba katika awamu zote 2 John Pombe Magufuli alikuwa ni sehemu ya Serikali hizo 2 zilizopita akiwa Mbunge na Waziri Mwandamizi katika Wizara ya Ujenzi/Miundombinu aliyekuwa akishiriki kwenye Baraza la Mawaziri(Cabinet) na Bunge na kwa mantiki hiyo naye ni sehemu ya uoza uliobariki hizi sheria na Mikataba mibovu ya kuwanyonya na kuwatapeli Watanzania!!!

Kamati ya Prof. Ossoro kuja na hoja ya kuwabana walokuwa Mawaziri na Manaibu wao au Wanasheria Wakuu haitoshi kiujanja ujanja huku wengine wakiachwa haitakubalika. Kamati wamemtaja marehemu Abdulla Kigoda(RIP) huku ikinyamaza kumtaja Jakaya Mrisho Kikuete aliyekuwa Waziri wa Maji,Nishati na Madini katika kipindi hichohicho kabla hajawa Rais!!

Mwisho, nampongeza JPM kwa ujasiri wa kuthubutu japo kachelewa sana kuhoji wizi huu wa Raslimali za Watanzania hoja iliyokuwa ikipigiwa kelele na Upinzani kwa miaka yote hii!! Swala la msingi la kujiuliza hapa ni Je, Rais JPM alikuwa wapi miaka yote hii 20 wakti wapinzani wakizomewa,wakitukanwa, wakitupiwa virago nje ya Bunge kwa kuhoji mambo ya msingi kuhusu Mikataba ya Madini?? Je, hivi leo JPM kwa tiketi ya CCM anawezaje kutuaminisha Watanzania kuwa hii vita ataiweza kama siyo ujanja ujanja na kutafuta kiki za 2020???
Tusubiri.
 
arch67

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
260
250

Baba j keshasema waachwe wapumzike
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,418
2,000
Nadhani wewe unataka kuwa kielelezo kwa wote mnaotaka kuwasumbua hao wazee. Mkuu kesha onya jamani kuhusu kuwasumbua hao wazee. Amesema; Sijaribiwi (in his own voice) Ohoooo. msijesema hamkusikia vyema
 
spika

JF-Expert Member
Dec 7, 2014
458
500
Mwenyekiti alimaanisha aliposema wapumzike. Na ndio maana amewawekea mazingira halisi ya kupumzika katika medani za siasa nchini. Naamini umenielewa!
 
Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
5,279
2,000
Mwenyekiti alimaanisha aliposema wapumzike. Na ndio maana amewawekea mazingira halisi ya kupumzika katika medani za siasa nchini. Naamini umenielewa!
Vita ikishaanza kubagua na kuchagua nani ni adui na nani rafiki basi VITA IMESHAKUSHINDA!!! Kwa lugha rahisi kabisa John Pombe Magufuli AMESHINDWA VITA MAPEMA NA ASUBUHI!!!!.Hana hoja baali hii ilikuwa ni longolongo tu na kiki za 2020!
Baba wa Taifa Mwl Nyerere9RIP) aliwahi kusema ukiwa Rais WAAMBIE NDUGU ZAKO NA RAFIKI ZAKO KUWA IKULU NI MAHALI PATAKATIFU kwa LUGHA THABITI!!! Lakini JPM hana lugah thabiti hapa na ndo maana ukimwangalia alipokuwa akiongea baada ya ripoti ya Osoro alionekana kuwa ana wacwac na hajiamini. Haya ndiyo matokeo.
Sidhani kama kina Mzee Yonnah, Karamagi,Chenge, William Ngeleja n.k watakubali wawe BANGUSILO( Kondoo wa sadaka).

JPM ajaribu kuwagusa hawa jamaa aone kama atarudiai Ikulu 2020!!! Chezea Mizee ya Chama Cha Makininikia-CCM wewe, labda kama hujitaki!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom