Watanzania tunapongeza mahakama ya Kenya badala ya kuilaani tume yao ya uchaguzi?!!

Martin George

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,695
1,470
Mahakama imetimiza wajibu wake kama inavyopaswa na kwahiyo hakuna la ajabu hapo. Binafsi nailaani tume ya uchaguzi iliyozembea hadi kuwaingiza wakenya kwenye gharama za marudio ya uchaguzi. Tume nzima ya uchaguzi inapaswa kuburuzwa mahakamani kwa kosa la kuhujumu uchumi na Odinga ameshasema hayuko tayari kurudi uchaguzini endapo tume haitatumbuliwa. Ahsante!
 
Ndio raha ya nchi kuwa na jaji mkuu na sio kaimu jaji mkuu.
 
Supreme Court of Kenya kama ingepelekewa kesi ya kupinga matokeo ya kura za Rais aliyetangazwa na Tume ya Uchaguzi Tanzania, naamini majaji hawa wangevunjika mbavu kwa kucheka utitiri wa forgeries wa tume yetu
 
Mahakama imetimiza wajibu wake kama inavyopaswa na kwahiyo hakuna la ajabu hapo. Binafsi nailaani tume ya uchaguzi iliyozembea hadi kuwaingiza wakenya kwenye gharama za marudio ya uchaguzi. Tume nzima ya uchaguzi inapaswa kuburuzwa mahakamani kwa kosa la kuhujumu uchumi na Odinga ameshasema hayuko tayari kurudi uchaguzini endapo tume haitatumbuliwa. Ahsante!

Kabla hujalaani ya Kenya ya kwenu umeisha ilaani?
 
Supreme Court of Kenya kama ingepelekewa kesi ya kupinga matokeo ya kura za Rais aliyetangazwa na Tume ya Uchaguzi Tanzania, naamini majaji hawa wangevunjika mbavu kwa kucheka utitiri wa forgeries wa tume yetu

Mahakama inayokubali kutengua Haki za Wabunge halali ili kuingiza Mamluki wa CCM kwenye vyama vya siasa
 
Vyovyote ilivyo huko kuamuliwa tu na mahakama uchaguzi urudiwe ni hatua kubwa haijalishi wanaingia hasara au lah!umejiuliza kama ingetokea hapa kwetu jambo kama hili ninini kingetokea?sidhani kama kuna judge angeweza kutoa hukumu kama hii ikiwa majaji wenyewe ni wanachama wa ccm kama Jaji Ramadhan Augustine alivyojitokeza hadharani kuchukua form ya kugombea urais bila kujali nafasi aliyokuwa nayo ktk taifa!

sent from my Infinix S2 Pro using JamiiForums mobile app
 
Kama tume na mahakama ni tatizo, wenzetu afadhali upande mmoja uko vizuri. Ni dalili kwamba hata maradhi ya tume yatapona.

Sisi kwetu kuanzia katiba, mahakama, tume kote kumeoza. Nimetaja katiba kwa sababu ndio iliipa nguvu kusmua mambo ya uchaguzi. Sie katiba yetu hata sijui mchakato ulifia wapi na sioni hata ikitajwa kwenye awamu hii.
 
Mkuu hapa Tanzania haiwezi kutokea sababu katiba hairuhusu matokeo ya urais kupingwa mahakamani!
 
Kama tume na mahakama ni tatizo, wenzetu afadhali upande mmoja uko vizuri. Ni dalili kwamba hata maradhi ya tume yatapona.

Sisi kwetu kuanzia katiba, mahakama, tume kote kumeoza. Nimetaja katiba kwa sababu ndio iliipa nguvu kusmua mambo ya uchaguzi. Sie katiba yetu hata sijui mchakato ulifia wapi na sioni hata ikitajwa kwenye awamu hii.
Mahakama za Tanzania bado ziko imara, kama huamini kamuulize Wasira!
 
Back
Top Bottom