Usiwatamanishe wenzio bure Kigogo,na nyinyi si mrudi nyumbani mpewe sehemu pale machinga complex mfanye hizo biashara au
Usiende nje ya nchi ukitegemea umoja wa WTZ kukusaidia. Kitu muhimu ni kufahamu sheria ambazo zinakulinda ukiwa ugenini, mfano kuwasiliana na ubalozi wa nchi yako na kuwaeleza upo pale kwa shughuli gani utakuwepo kwa muda gani nk. Pindi ukishikwa kitu cha kwanza popote pale utakapokuwepo unawasiliana nao na kuwaambia upo wapi nk. Kama wamekufunga jela na watakupeleka mahakamani au watakurudisha TZ etc.
Jambo jingine ni kuwa na fweza za kuweza kulipa kwa wakili ambaye atakuwakilisha kwenye jambo lolote kama unafanya biashara yenye faida nzuri vile vile kuwa na uhalali wa kuwepo pale. Usiingie kwa njia za panya, nenda na passport na uvuke mpaka kihalali. Know your rights na angalia shughuli unayofanya kama unaruhusiwa kuifanya, usijiingize kwenye biashara ambayo ni ya magendo au pengine wageni hawaruhusiwi kuifanya, declare mali zako kama ni za kuuza na uwe na risiti etc. Usiingize mzigo kwa magendo fuata njia halali ingawaje faida inaweza kuwa ndogo in a long term itajilipa.
Jana usiku wamekuja kutugongea majumbani wamekamata watanzania nane, Hata uwe na paspot wanakuchukua hadi saiz tupo mafichoni!
Dah Poleni sana.Wamalawi wamejaa tele kinondoni wanaishi raha mustarehe hakuna anayewabughudhi hata kidogo.Jana usiku wamekuja kutugongea majumbani wamekamata watanzania nane, Hata uwe na paspot wanakuchukua hadi saiz tupo mafichoni!
hiyo hali sio malawi tu, hata ukifika Bot, Swaz, Leso, Nam, RSA wanakuwaga na kampeni maalumu kwa foreignerz, na nchi hizo lazima karatasi zako ziwe sawsawa,
ni hapa bongo tu unakuta mzawa na foreigner wanagombea kazi ambayo hata mzawa anaiweza vizuri
poleni sana waangaikaji, si siasa yetu ndio inayowatesa,
Dah Poleni sana.Wamalawi wamejaa tele kinondoni wanaishi raha mustarehe hakuna anayewabughudhi hata kidogo.
Pole Edgartz,
1. Nchi zenye sera za mambo ya nje, huwa zina "reciprocation policy". Tanzania ingekuwa na sera kama hiyo, hayo yote yasingewakuta.
2. Endelea kufanya biashara huko. Ila katika kipindi hiki kigumu, kama unaweza rudi Tanzania kwa muda.
3. Uzoefu nilioupata nilipoenda ofisi moja ya ubalozi wa Tanzania, unanifanya nisiwe na matumaini kwamba watawasaidia lolote la maana huko, kwa vile hayo matatizo mnayoyapata huenda hayapo kwenye hadidu za rejea za kuwapo kwao kwenye ubalozi.
Mlenge
Acha masihara wewe unataka kusema huko Malawi maficho yao yana access nya internet?Biashara gani mnafanya au za madawa ya kulevya?Jana usiku wamekuja kutugongea majumbani wamekamata watanzania nane, Hata uwe na paspot wanakuchukua hadi saiz tupo mafichoni!
Msije mkawa mafisadi wa kulowea kama wanyaru waliorudishwa mwaka wa 2006 kama sikosei maana mafisadi wako wa aina nyingi ati. ukiangalia wanyaru wakati wanarudishwa kwao yalisemwa mengi wakati wengine waliingia TZ tangu miaka ya hamsini hata hatujapata uhuru na wakawa wanaishi kama wa TZ lakini hawakuwakuwa na vibali vya kuishi nchini na wala hawakubadilii uraia wao hivyo 40 yao ilipofika wengi walilalamika kuwa wananyanyaswa, wananyang'anywa mifugo n.k wa kadhaa hiyo yote ni kutokana na kutokujua taratibu za uhamiaji na sheria za nchi yetu zinasemaje.
sasa na nyie muangalie kuwa je kwanza mlipofika huko mliripoti kwenye Ubalozi wenu na kujiandikisha? maana unaporipotu naamini mambo mengine ambayo huyajui Ubalozi watakueleza.
2. Mna vibali vya kuishi na kufanya biashara huko Malawi? maana wengine wanafikiria kuwa akishakuwa na pasipoti na kwa kuwa halipi viza ya kuingia malawi basi akishavuka mpaka na kugongewa entry stamp ndio imemhalalisha kuishi na kufanya biashara kwenye nchi ya watu. Unaruhusiwa kuishi kwenye nchi ya watu siku 90 tu zaidi ya hapo unatakiwa kuwa na vibali vya kuishi , kufanya kazi au biashara bila hivyo wewe ni mhamiaji haramu. unatakiwa kabla hujaenda kwenye nchi ya watu ujue taratibu za uhamiaji zinasemaje na pia uzijue haki zako bila hivyo kulalamika hakutakwisha. Ukizijua haki zako hata anayekukamata hawezi kukunyanyasa kirahisi kwa sababu anapokunyanyasa anajua fika na wewe unazijua taratibu na haki zako hivyo wakati wowote kibao kinaweza kumrudia.
3. Je mnalipa ushuru na kufuata taratibu za nchi husika.
kama ni ndiyo mnatakiwa mpige simu Ubalozini mara moja kuwaeleza matatizo yanayowakabili ili uwasaidie. na kama sio hao wamalawi wanatakiwa wawarudishe Tanzania ndani ya 24hrs kama sio kuwafunguliia mashitaka ya kuishi na kufanya biashara kinyume na taratibu za nchi. yaani wahamiaji haramu.
Mkuu iko ivi unaweza kuwa umetoka tz leo ukafika boda wakakupa mwezi mmoja unafika lilongwe wanakukamata ukiwapa paspot wanakwambia twende hapo wanawapeleka gerezani je? Nisheria?