Watanzania tunakwama wapi?

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
10,098
12,472
Habari za mda huu wakuu,

Kwa wagonjwa poleni na mungu awafanyie wepesi mrudi katika Hali ya zamani wazima poleni na majukumu na mihangaiko ya kila siku.

Wakuu Kuna hili swala naona linaota mizizi siku za karibuni na huenda likawa tatizo baadae kwa wachezaji hata hawa wanaochipukia,

Kucheza mpira nchi za nje hasa ulaya ni ndoto ya wachezaji wengi Tanzania na barani Africa kwa ujumla Ila kwa wachezaji wengi wa Tanzania wakipata nafasi wanashindwa na hatimae kurejea tena nchini wachache wanaoshindwa baadhi ya team za nchi za nje na kuamua, kupambana sehemu nyingine tofauti na nyumbani Ila wengi hushindwa kuwa wavumilivu.

Tumeona baadhi ya wachezaji Kama:
Ninja- karudi yupo yanga
Farid - karejea na yeye yupo yanga
Chilunda-karejea nchini yupo Azam
Kichuya-karejea nchini Ila kwa sasa yupo namungo.

Hao ni wachache wa hivi karibuni Ila wapo wengine wengi waliorudi nchini kwa aina hiyo, hivi wakuu wachezaji wetu Wana feli wapi katika Hilo tatizo Nini hawadumu wakienda kucheza nje?
 
What goes around comes around.

Leo hi mnamponda Carlos wa yanga mnamtukana kua mzembe.

Wakifika huko wanafanyiwa hivyo hivyo

Ikichangiwa na lugha + kujituma
 
Viwango vyao ni vidogo sana, hawafundishiki/hawabadiliki kwani wengi hawajapita academy hivyo hawana basics za football...hivyo huchezea bench la nguvu na mwisho kuachwa au kukimbia na kurudi bongo.

NB; Ni maoni yangu binafsi tu.
 
Habari za mda huu wakuu,
Kwa wagonjwa poleni na mungu awafanyie wepesi mrudi katika Hali ya zamani wazima poleni na majukumu na mihangaiko ya kila siku.

Wakuu Kuna hili swala naona linaota mizizi siku za karibuni na huenda likawa tatizo baadae kwa wachezaji hata hawa wanaochipukia...
Haya mambo yanazunguka kwenye elimu/exposure na uchumi.

Nchi yenye uchumi mdogo hata lishe tu ni mgogoro, na kuna mambo fulani ukikosa utotoni kiyaweka sawa ukubwani ni kazi sana.

Ndiyo hapo unakuta watu wanachezea timu kubwa Tanzania, lakini miili yao midogo.

Kwenye elimu kunataka mchezaji aweze kupanga strategy, ajue kufuatilia ma valangati ya international football, strategies za kujioanga vizuri atambulike startegies za mazoezi ya ngazi ya kimataifa, kuusoma.mchezo kama somo la darasani halafu kuhamishia mambo uwanjani.

Suala la academies za soka ni muhimu sana, nchini kwetu tuna academies ngapi za soka za maana? Watu wanaandaliwa au tunabahatisha tu? Na huwezi kuwa na academies kama huna uchumi mzuri, maana zinahitaji uchumi mzuri kuziendesha.

Tunarudi kwenye uchumi.
 
Mpira wa miguu ni fani...kama fani zingine kama sheria...ualimu na nyingine nyingi tu hivyo ina taratibu zake za msingi...ambazo zinamuhitaji Mtu aingie darasani rasimi ili ajifunze...hapo ndipo suala la shule za mpira ( academy).. linapokuja..,.mchezaji anaweza kuwa na kipaji...lakini akakosa misingi ya uchezaji.

kama kupokea mpira kuficha mpira kukimbia na mpira kukaba kumiliki eneo lako kupiga faulo na mengine mengi yanapatika shule tu tena ukiwa mtoto ukishakuwa Mtu mzima ni ngumu sana kubadilika.

hivyo kumpa shida mwalimu...na ukikutana na wenzio waliopita shule...ww utaonekana hujui kitu.... Kama nchi... Kwa kushirikiana na TFF tunapaswa kuwekeza kwenye shule za mpira kwa wingi. lakini pia huko shule wafundishwe na lugha hasa hii ya mkoloni...maana nadhani hapo Napo ni tatizo.
 
Habari za mda huu wakuu,

Kwa wagonjwa poleni na mungu awafanyie wepesi mrudi katika Hali ya zamani wazima poleni na majukumu na mihangaiko ya kila siku.

Wakuu Kuna hili swala naona linaota mizizi siku za karibuni na huenda likawa tatizo baadae kwa wachezaji hata hawa wanaochipukia,

Kucheza mpira nchi za nje hasa ulaya ni ndoto ya wachezaji wengi Tanzania na barani Africa kwa ujumla Ila kwa wachezaji wengi wa Tanzania wakipata nafasi wanashindwa na hatimae kurejea tena nchini wachache wanaoshindwa baadhi ya team za nchi za nje na kuamua, kupambana sehemu nyingine tofauti na nyumbani Ila wengi hushindwa kuwa wavumilivu.

Tumeona baadhi ya wachezaji Kama:
Ninja- karudi yupo yanga
Farid - karejea na yeye yupo yanga
Chilunda-karejea nchini yupo Azam
Kichuya-karejea nchini Ila kwa sasa yupo namungo.

Hao ni wachache wa hivi karibuni Ila wapo wengine wengi waliorudi nchini kwa aina hiyo, hivi wakuu wachezaji wetu Wana feli wapi katika Hilo tatizo Nini hawadumu wakienda kucheza nje?
Ongeza kessy
Ongeza David Kissu

Sababu ni nyingi lakini tunaweza kuziweka makundi matatu
1.Uvivu wa mazoezi ,kutojielewa na nizamu (Okwi +Bobani +Kessy)
2.Mazingira na utamaduni mpya(farid +chilunda+Kichuya)
3.Maslahi madogo kwenye mpira wa Africa compare na Tz (David kissu)

Wasipozingatia baadhi ya mambo wafuatao ni suala la mda kurudi
1.Habibu Kyombo. - mvivu anajisikia sana (Kiufupi ni ajibu alichangamka)
2.Eliuta Mpepo -Ligi ya zambia maslahi madogo
3.Yahya Zaid - mazingira ya urabuni hayamfevi kabisa
4.Okwi,Jukko,Ballora na shishimbi - hawa hawana uraia wa Tanzania ila mioyo yao ni ya kitanzania hawajitumi,nizamu mbovu,wanacheza kwa mazoea na bado wanataka mishahara kikubwa hivyo care hiyo ipo Dar es salama Tanzania pekee
5.Umri na nyakati -Singano ,mandawa na Magulli

Kongole kwa hawa watastafia huko ata kwa ndumba (Ving'ang'anizi)
1.Samata ata iwe daraja la 5 swewden ila sio Vpl
2. Ulimwegu - ataendelea kuwepo group stage za Ccl na timu tofauti hata kwa miaka mingine mitano
3.Msuva- amewasha moto hauzimiki na anatengeneza jina
4. Nikson kibabage+ Eliud Ambokile - wanajielewa sana
5.Himidi Mao- anajituma,nizamu ,huwa hajali kudharauliwa na mashabiki
 
Nasikia kuna mmoja fundi kweli kweli! Kwa sasa jua limeshazama tayari! Kisa tu aliyamisi huko ughaibuni yale majani yanayovutwa mdomoni na kutolea moshi puani, hivyo akaamua kuchukua kila kilicho chake na kurejea nchini haraka na kuwaacha wadau waliompeleka huko midomo wazi.
 
Kinachoumiza jamaa alikuwa analipwa vizuri na mwaka anaondoka timu yake ilifuzu UEFA champion kwenye stages za awali
 
Nasikia kuna mmoja fundi kweli kweli! Kwa sasa jua limeshazama tayari! Kisa tu aliyamisi huko ughaibuni yale majani yanayovutwa mdomoni na kutolea moshi puani, hivyo akaamua kuchukua kila kilicho chake na kurejea nchini haraka na kuwaacha wadau waliompeleka huko midomo wazi.
Nani huyo mkuu na anacheza timu gani kwa sasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom