Watanzania tuna wazimu?

Forgo

Member
Apr 7, 2016
27
60
Watanzania tujifunze kufikiri, hili sakata la vyeti halikuibuliwa na wakina Chid Benz, T.I.D, Ray C,Tunda nk sababu hawa wote ni waathirika wa madawa ya kulevya na walistahili kuhojiwa wanayatoa wapi japo taratibu za kuitwa kwao polisi na mkuu wa mkoa zilikuwa kinyume na sheria.

Huyu mkuu wetu wa mkoa ni mpumbavu mwenye chuki na visasi.... Tuelewe kwamba sakata la vyeti vyake lilishikiwa bango na Mch. Josephat Gwajima ambaye yeye alitajwa na mkuu wa mkoa kama mtuhumiwa wa madawa ya kulevya (anauza au anatumia) na baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa mkemia mkuu ilionekana hatumii madawa ya aina yoyote na hata baada ya upekuzi nyumbani kwake pia hakukuwa na kidhibiti au mazingira yenye kuonyesha yeye ni muuzaji.

Sasa je, Huyu mkuu wetu wa mkoa yeye kama Mwenyekiti ni dhahiri kwamba alifanya kazi na vyombo vya ulinzi na usalama vilivyo chini yake ili kujiridhisha kwa kuwataja watu halali kwa taatifa za kiuchunguzi zenye vidhibitisho? au ndio chuki na visasi vyakipumbavu?.

Hakuna mtu anapinga kampeni ya kuzuia madawa ya kulevya ila Daudi Albert Bashite ni ujinga wake wa kulewa madaraka umemfikisha hapa kwenye vyeti fake.

Kama tunayo nia ya dhati, tuunganishe nguvu kumsaidia kamishna Sianga sio kumtetea mtu mwenye akiri za kutengeneza video za uongo kulazimisha kwa bunduki zirushwe hewani na kituo cha televisheni kwa lengo la kuchafua watu then mnamuita Mheshimiwa!!!! Ujinga.

Kwa akiri kama hizo atashindwa nini kumpakazia mtu yeyote na kumuhusisha na madawa ya kulevya?

Na ninani amewaambia vyeti vya Makonda vimezuia vita dhidi ya madawa ya kulevya?

Mjinga ameshindwa vita kwa ujinga wake wa kuingiza chuki binafsi na visasi kwenye swala nyeti la kitaifa.... Tuungane na jemedari wa vita kamishna Sianga.... Anayefanya kazi kwa misingi ya sheria, anazingatia Kweli na Haki.



Forgo #Jf
 
Back
Top Bottom