Watanzania tuna salamu ndefu sana

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,692
40,948
Habarini za sikukuu bandugu??

Hii hulka ipo sehemu nyingi na kwa makabila mengi.

Salamu ni kama ifuatavyo;

1. Mambo vipi, ukimjibu poa ataongezea niajee?? Utamwambia fresh tu. Au Badala ya niaje atatumia nambie?? Mwisho atamalizia mambo mengine?

2. Habari yako, nyumbani wazima? Mama/mumeo hajambo, watoto wanaendeleje? Flani amesharudi toka shule? Haya ukifika nisalimie wote.

Haya ndio maisha Yetu, na lazima ujibu maswali yote kwa kila utayekutana nae, usipojibu Tayari umetengeneza uadui.
 
Mambo yanaenda lakini.... Naona upo..... Vipi lakini mishe zinaenda.....

Watanzania tunapenda kujadili, na huo ni mjadala siyo salaam.
Usipokuwa makini unaweza chelewa unakokwenda kama unatembea kwa miguu.

Unakuta more than 20 min ni salamu tu.
 
Habarini za sikukuu bandugu??

Hii hulka ipo sehemu nyingi na kwa makabila mengi.

Salamu ni kama ifuatavyo;

1. Mambo vipi, ukimjibu poa ataongezea niajee?? Utamwambia fresh tu. Au Badala ya niaje atatumia nambie?? Mwisho atamalizia mambo mengine?

2. Habari yako, nyumbani wazima? Mama/mumeo hajambo, watoto wanaendeleje? Flani amesharudi toka shule? Haya ukifika nisalimie wote.

Haya ndio maisha Yetu, na lazima ujibu maswali yote kwa kila utayekutana nae, usipojibu Tayari umetengeneza uadui.
Ni utamaduni mzuri. Kwanza unaendelea ukaribu na pia ni rahisi kugundua kama rafiki/ndugu yako hayupo sawa hata kama atajibu yupo sawa. Inapunguza isolation kwa watu wenye hatari ya kupata msongo wa mawazo. Ndio maana takwimu za watu kujiua kutokana na msongo wa mawazo kwa nchi kama TZ ni ndogo kulinganishwa na mataifa yasio na utamaduni wa kusalimiana au kuwasiliana kwa namna yetu.
Na pia sio kwamba wao hawana tamaduni zao, mfano wapo ambao salamu zao wanapenda kuongelea hali ya hewa (Uingereza), wapo wanaopenda kujadili michezo (Ujerumani) n.k.
 
Salamu ndefu ina logic
 
Ila ni mtihani kwa wasiokuwa na maneno mengi
 
Kuna jamaa nilikutana naye njiani.. akasalimia mambo nikajibu poa then nikaendelea na safari...

Jamaa akaenda kulalamika huko mbele eti nimempita tu kama simjui... nilishangaa sana nikawaambia mbona tumesalimiana?

Watu ukiwasalimia juu juu wanasema una dharau!!
 
Huwa natembea haraka haraka kuepuka salamu ndefu. Mbio mbio tunasalimiana kwa kupungiana mikono tu.

Salamu ndefu zinasababishwa na watu kuwa wavivu na kukosa cha kufanya. Ndio maana wana muda wa kurefusha hadithi.

Tufanye kazi. Magufuli Oyeeee. Hapa kazi tu.
 
me nadhani ni kwa sababu watanzania wengi hawana kazi za kufanya hasa huko vijijini ndio haya mambo ya kusalimiana lisaa lizima yapo...
 
Write your reply...

Sisemi lolote hapa

Ila zna raha yake unaeza kupata dili za pesa
 
Back
Top Bottom