Watanzania tuna salamu ndefu sana

Watanzania tuna salamu ndefu sana

Kuna zile 'ntambuzi' (salamu) za wagogo..... mtu anakusimulia hadi paka wake alivyokunywa maziwa ya mtoto na hiyo bi bado salamu tu.
Utasikia nhiiiiiiii, nhiiiiiiiiii.....
😀😀😀😀😀😀
 
Sio tz pekee, urefu wa salamu itategemea na watu wanaosalimiana hapo
 
Mie naona ni nzuri sana,sikujua umuhimu wa salam hizo hadi nikiwa nyumbani Tz,ugenini mtu anakupita kama kaona paka.

Inaonesha watanzania tunajali.
 
Salam ndefu inaonyesha hulka nzuri katika mawasiliano ya wawili hao au kundi hilo. Huwezi ukawa too short kwa watu wako wa karibu, inabidi uongee ili kuweka bond kati yenu. Kuna msemo wa kizungu wansema "silence is a rerationship killer", Ukiwa mkimya mwenzio au mtu wako wa karibu anatafsiri labda anakukera kwa yeye kuongea au labda anaongea sana. sasa inafikia muda naye anajifunza kutoka kwako, mkikutana mna gumiana kama mabubu ,"mambo vipi?", "poa" kwisha mnakaa kimya.
Vijana kama marafiki au classmates, au school mate, mnapaswa kuchangamkiana na hiyo inaongeza/nogesha uhusiano miongoni mwenu au kati yenu. Hii inaanzia kwenye urafiki wa kawaida hadi kwenye ndoa na familia. Ukianza kuona wenzako wanaongea saaana, wakikaa kimya ,mtajikuta wote mnakuwa kimya halafu mnaanza ohoo home pana boa hakuna stori, kila mtu kanuna tuuu utadhani tumegombana.
Sisemi uongee saana ,hapana lakini salaam ndefu ni gesture nzuri kwa marafiki wenye mahusiano mazuri, inaonyesha kila mmoja ana mmiss mwenzie. Sasa ukimsalimia mwenzio "mambo vipi?", akajibu "poa" kasha wote mkakaa kimya ndio nini, unapo extend maongezi ni jamabo zuri kwamba mwenzio anaonyesha anao muda nawewe. sasa ukijidai una haraka wakati unaenda mjini kuzurura inakusaidia nini. Unataka uonekane wa maana wakati huna maana yoyote, ni upuuzi. Hata kwa mzazi, mdogo, kaka au dada, mke ,mume msalimie muongee kidogo mchekeshe mfurahiane sio muwe kama kondoo mtachukiana bure.
Kwa kifupi ongezeni nyama kwenye salamu, hata ukisalimia hadi paka wa jirani kwani kuna ubaya gani? mwenzi atacheka na kila akikuona au kukukumbuka ata cheka au kusmile hilo ndio jambo zuri. Acheni kujenga tamaduni mbaya, mara wasukuma mara sijui wagogo, kwani kuna asiyekuwa na kabila Tanzania hii? Tuwe vijana wachangamfu na kufurahishana kuanzia nyumbani hadi mtaani. trust me haya nayaandika hapa mnaweza kuya puuza ukiya practice utafurahi na kuwa mwenye furaha kila mahali.
Hutoogopa kukutana na watu, hutoogopa ku open conversation, hutoogopa kuonge na yeyote awe mkubwa au mdogo, maana kila mtu atakuwa amesha kufahamu hulka/aiba yako kwamba wewe ni mcheshi au mzungumzaji mzuri, na ni jambo zuri kuliko kuwa mkimya muda woote, hakuna mtu anataka kuwa na mtu mkimya muda wote. Muwe charming wote wavulana kwa wasichana, na hii huanzia kwenye salamu.
 
Mie naona ni nzuri sana,sikujua umuhimu wa salam hizo hadi nikiwa nyumbani Tz,ugenini mtu anakupita kama kaona paka.

Inaonesha watanzania tunajali.
Hawajui hawa, salama ndefu nzuri sana tu. Mi natamani nikikutana na mtu hata tukae chini tusalimiane vizuri. nani asiyependa kupendwa humu? Open up guys achenI usera mbuzi na salamU za kizungu eti "Hi" na "Hi" NDIO NINI? WEWE SIO MZUNGU KWANINI UJITIE UZUNGU?!
Yani ongeeni hata kilugha chenu mkiweza ,hakuna asiye na lugha yake Tanzania, kama hajui lugha yake shauri yake na ulimbukeni wake. Usiogope kuitwa mshamba, just be yourself.
 
Mnasalimiana hadi mnakaa kwenye jiwe
Na hii ndio mi napenda sasa, yani mkiachana inakuwa ni kwasababu tu ya majukumu, otherwise mngeendelea kukaa kwenye jiwe mpige story mpaka ziishe muangaliane mcheke kasha muanze mwanzo.
 
Mzee watu ambao wanasalamu ndefu ni Wasukuma aisee yani wakikutana salam tu sio chini ya 20-30 dk kwa ufupi
Yaani niliwahi kuwaona mpaka nilishangaa ... usiombe upande nao gari moja sasa .... huwa wana makelele kama nyuki wa machine ... mtu aliyekaa siti ya nyuma let say katika bus kama la abood anaweza kaunza kupiga story na mwenzake anaye safiri nae aliyekaa siti ya mwanzo kabisa karibu na dereva ...

Makelele ya hapo sasa ..utachoka mwenyewe
 
Hizi ndizo salama na mashoga zetu.

Shoga: mambo luckyline
Mie: poa,
Shoga: kwema?
Mie : kwema WAP?
Shoga: nn tena, Nipe umbea
Mie: umbea sina ushuzi mtupu mfyuuuuuuuux
Shoga: wapi shemeji?
Mie : shemeji my takoo, ongea mambo ya maana achana na mikosi asubuhi hii
Shoga: 😀😀😀wacha weee nyooo huna lolote nyau wewe.
Mie: mpuuzi mkubwa wataka umbea wangu, wako je?
Shoga: ushuzi mtupu sina lolote😀😀
Mie: huna jipya ukilipata utanitafuta.
Shoga: 😀😀tena nimekumbuka hivi yule kaka ulonambiaga yupo?
Mie: yupo tena? Yule mwanangu wa kitaa best yangu?
Shoga: eee huyoooooo
Mie:😀😀😀huyu mshikaji wangu hana jipya ndugu namjua kila kitu, huyu anapenda mteremko tudemu twake tubakujaga tunalia kwangu nimwambie kama kaoa maana huyu mshikaji anamke nyie hamjuagi.
Shoga: wacha weeee, wee nifowadie ntadili nae😀
Mie : nikupe no ama?
Shoga : mmmh ntamtafutaje?
Mie: tena anakuulizia sana wacha Leo nimkumbushe:
Mshikaji: oya vip?
Mie 😛poa una jipya?
Mshikaji: afu yule Shoga yako nammaindigi kinyama
Mie: mpuuzi mkubwa wewe unavyopenda vutoto vidogo yule Dada anajielewa na ubahili wako utaweza?
Mshikaji: mambo gani sister , mie dume bana Nipe no kama VIP:
Mie: utajibeba hii hapa.
Shoga: yule kaka kapiga ila nahisi ni mshenzy mim naonaga mtu wa maana:
Mie: kama ushaona mshenzy basi mfukuze kisomi:
Shoga: kisomi ndio maana gani?
Mie :usije mtukana yule ni mwanangu hapa kitaa:
Shoga: nimwambieje sasa?
Mie:dawa moja ya kumfukuza mwanaume hapa dunia ni kumwomba pesa, ingawa mm sijawahi omba, ila hii ndio dawa yao.
Shoga: kweli eee, nimwombe shilling ngapi?
Mie: mwombe tu laki 5, ukimwomba hela ndogo kama laki atakupa.
Shoga: asante, Leo hii namfukuza.
Mshikaji: oya sister dah mwanangu yule dem kanipiga kiziinga kichwa kinauma, nataka kweli nimechoka na vitoto vidogo, ila hiyo hela sina.
Mie: 😀😀😀😀😀😀 wewe si dume?
Mshikaji: dah naachia ngazi ujue? Shoga: asante kwa ushauri Siku hizi hata hanitafuti.
Mie: 😀😀😀😀😀😀😀
Shoga: haya mamiiii nilikuwa nakusalimia tuuu.byeee🙌🙌🙌🙌😀
 
Oi...aje!? Nimemaliza hapo. Mtu mzima ni habari za sahizi? Kama atamaindi sijamsalimia shkamoo kimpango wake. Mzee wangu tu tunasalimiana mambo vp, aisee sipendi shkamoo kama kitu gani sijui, nshagombana sana na dadaangu kisa shkamoo siiwezi yani
 
Back
Top Bottom