Watanzania tumempa kazi Lowassa

Watanzania tumempa kazi Lowassa

Tukundane

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2012
Posts
12,231
Reaction score
9,552
Watanzania tumempa kazi Lowassa ya kuichapa CCM,hakuna mtu mwingine anayeweza akawachapa CCM zaidi ya Lowassa kwa kuwa amekaa nao muda mrefu,amefanya kazi katika serekali ya CCM kwa kipindi kirefu,ujanja wao wote na hila zao zote mpaka rangi za nguo zao za ndani ana zifahamu.

Pamoja na propaganda zote zinazopigwa na CCM kuwa Lowassa ni mgonjwa hataweza kuongoza nchi lakini kwa kuwa Lowassa ana wamudu CCM wananchi tutakwenda na Lowassa kwa kuwa kazi ya kuongoza nchi ni rahisi kuliko kazi ya kuwaondoa CCM madarakani kwa kuwa nchi haitegemei kuongozwa na mtu mmoja.

Ugumu wa kazi ya kuiondoa CCM madarakani ulianza kujidhihirisha pale ambapo watu wengi kama Mrema na wengine walipojaribu kuiondoa CCM madarakani wakashindwa kwa kuwa kazi ya kuiondoa CCM ni ngumu kuliko kazi ya kuongoza nchi.Ambayo hata kama utakuwa na nguvu kama tembo CCM inaweza ikakushinda,hata kama utakua na afya iliyothibitishwa na Mungu mwenyewe,kuwa ni mzima CCM inaweza ikakushinda.

Hata kama CCM watapiga propaganda vipi,kuwa Lowassa ni fisadi na kwa kuwa CCM wameshindwa kutuhakikishia kuwa baada ya Lowassa kujiuzuru ufisadi ndani ya serekali ya CCM umekwisha,wananchi tutakuwa na Lowassa.

Hata kama ikitokea Lowassa akafa siku moja baada ya kuiondoa CCM madarakani,watanzania tutamuenzi kama shujaa pekee aliyefanya kazi nzito ya kuiangusha CCM iliyowashinda watu wanaojiona kuwa wana afya bora kuliko wenzao.
 
watanzania tutamuenzi kama shujaa pekee aliyefanya kazi nzito ya kuiangusha CCM iliyowashinda watu wanaojiona kuwa wana afya bora kuliko wenzao.

Nami Nasema Bega Kwa Bega Na Mh. LOWASA.

Huyu Ndie Shujaa Wa Karne Ambaye Watanzania TUNAMHTAJ kuliko wakati Mwngne Wowote, Kutuvusha mpaka Nchi Ya Neema Na Baraka Tele
 
Huu mwaka lazma wakae,ukiona mpaka dodoma watu hawaitaki tena ccm,ujue mwisho wao umefika,watu wamechoshwa na ufisadi,ahadi hewa,ujangiri uliopitiliza,rushwa,huduma duni za kijamii,bunge la wasinziaji na wagonga meza "Ndiyoooooooo" hakika,MUNGU aendelee kuwa na wana mabadiliko ktk jitihada hizi za kuingoa fisiem
 
Lowassa, Ukawa ndio mpango mzima..

Lowassa ni SHUJAA WA MPYA ktk UKOMBOZI WA WATANZANIA...!!!

Ni shujaa haswaa... nashindwa kuandika neno la kusema hisia zangu halisi...!!

Anyway Lowassa chaguo la Mungu...!!!
 
Watanzania tumempa kazi Lowassa ya kuichapa CCM,hakuna mtu mwingine anayeweza akawachapa CCM zaidi ya Lowassa kwa kuwa amekaa nao muda mrefu,amefanya kazi katika serekali ya CCM kwa kipindi kirefu,ujanja wao wote na hila zao zote mpaka rangi za nguo zao za ndani ana zifahamu.

Pamoja na propaganda zote zinazopigwa na CCM kuwa Lowassa ni mgonjwa hataweza kuongoza nchi lakini kwa kuwa Lowassa ana wamudu CCM wananchi tutakwenda na Lowassa kwa kuwa kazi ya kuongoza nchi ni rahisi kuliko kazi ya kuwaondoa CCM madarakani kwa kuwa nchi haitegemei kuongozwa na mtu mmoja.

Ugumu wa kazi ya kuiondoa CCM madarakani ulianza kujidhihirisha pale ambapo watu wengi kama Mrema na wengine walipojaribu kuiondoa CCM madarakani wakashindwa kwa kuwa kazi ya kuiondoa CCM ni ngumu kuliko kazi ya kuongoza nchi.Ambayo hata kama utakuwa na nguvu kama tembo CCM inaweza ikakushinda,hata kama utakua na afya iliyothibitishwa na Mungu mwenyewe,kuwa ni mzima CCM inaweza ikakushinda.

Hata kama CCM watapiga propaganda vipi,kuwa Lowassa ni fisadi na kwa kuwa CCM wameshindwa kutuhakikishia kuwa baada ya Lowassa kujiuzuru ufisadi ndani ya serekali ya CCM umekwisha,wananchi tutakuwa na Lowassa.

Hata kama ikitokea Lowassa akafa siku moja baada ya kuiondoa CCM madarakani,watanzania tutamuenzi kama shujaa pekee aliyefanya kazi nzito ya kuiangusha CCM iliyowashinda watu wanaojiona kuwa wana afya bora kuliko wenzao.
Mkuu , thank you very much!, this is very inspirational!, natamani ungepata fursa ya kupanda jukwaani kwenye ile mikutano inayotangazwa live ili watanzania wote wayasikie haya!.

Ushindi kwa Lowassa, utapatikana kwa the spirit of victory itakayofungua the will powers za ushindi, zitakazomfanya Lowassa ashinde kwa kishindo despite all the odds!.

Pasco

Baada ya MUNGU, anafuata LOWASSA!!!

Magamba lazima yaondoke mwaka huu! ...Hakuna namna tena!!!
 
Kwa kweli sasa hivi TANZANIA inamhitaji LOWASA kuliko wakati mwingine wowote tangia nchi yetu ipate Uhuru.Nchi imekwama kwenye Lindi la rushwa na ufisadi uliorutubishwa na CCM.
Wananchi tunahitaji tutoke hapa tulipo tusonge mbele.Hatuoni mwingine wa kututoa hapa tulipo tofauti na Huyu shujaa wetu wa karne Mh.EDWARD NGOYAI LOWASA.
 
Lowassa punde akiichukua nchi- vizazi vijavyo watasoma Tanganyika imewahi kuwa na mashujaa wawili. Nyerere alietupa uhuru na Lowassa aliesukuma gurudumu la maendeleo. Hao wengine watatupwa kwenye dustbin la history
 
Askari wakihakikisha ulinzi nyumbani kwa Amiri jeshi anayesubiri kuapishwa EL
12003135_399403616918909_5243387698178289955_n.jpg
 
Pata muda wa kumwomba Mungu kabla ya kufanya maamuzi, tii sauti yake chukua hatua, mbali na hapo ni kujuta tuu, hakuna neema!
 
Pata muda wa kumwomba Mungu kabla ya kufanya maamuzi, tii sauti yake chukua hatua, mbali na hapo ni kujuta tuu, hakuna neema!

Huwezi ukafanya maombi katikati ya mapambano,maombi yanafanyika kabla ya kuanza mapambano, kinachofuata ni kupigania kile ulichoambiwa ukifanye baada ya kuomba na kwa kutumia silaha ile ambayo umeelekezwa kuwa ukiitumia itakuwezesha kushinda.

Na kama hukuomba kabla ya kuanza mapambano unategemea kuomba katikati ya mapambano, usitegemee muujiza zaidi ya kujuta kama ulivyosema kwa kuwa Mungu ni wa mipango hakurupiki kama nyati aliyekurupushwa kichakani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom