Watanzania Tumemkosea nini Mungu?

Watanzania Tumemkosea nini Mungu?

EXTERMINATOR

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
343
Reaction score
90
Ni nchi iliyojaaliwa rasilimali nyingi kuliko hata nchi zilizoendelea kama Japani. Kati ya maajabu 7 ya asili Afrika matatu yamo Tz serengeti, ngorongoro, kilimanjaro. Ni nchi ya 3 Afrika kwa uzalishaji dhahabu, tuna kila aina ya madini ikiwemo Tanzanite ambayo ipo Tz pekee kwenye hii sayari.Tuna mbuga nyingi za wanyama,mito, ardhi nzuri ya kilimo.Tuna bahari, mito, maziwa makubwa kuliko nchi yoyote AfrikaTuna rasilimaliwatu ya kutosha45m. Pamoja na majaliwa yote hayo Tz ni nchi masikini sana na raia wake wanatafuta mali kwa viungo vya binadamu, wanauana kwa hisia za ushirikina,wanaendekeza udini,wamejikita kwenye wizi na ufisadi n.k. Kwa profile ya natural resources endowment tupo vizuri kuliko nchi nyingi kwenye sayari yetu lakinitunaongoza kwa umasikini na mambo ya kupuuzi na ushirikina. Hii laana tumemkosea nini Mungu waTz?
 
Mnamzingizia mungu tu , ni kutokana na unafiki, fitina na ubinafsi uliowajaa ndio maana hamtoki, kazi uchawi na kuoneana choyo tu, uvivvu kibao !
 
Mnamzingizia mungu tu , ni kutokana na unafiki, fitina na ubinafsi uliowajaa ndio maana hamtoki, kazi uchawi na kuoneana choyo tu, uvivvu kibao !

Naongezea kusema na tuna laana ndo maana hatuendelei.Hili nchi ni cho nina mwaka mmoja wa kukaa hapa nasepa zangu mbele huko kwenye wenye akili timamu.Ili u copy na mambo ya nchi hii lazima uwe na akili nusu la sivyo BP inakuhusu.
 
Usisahau Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na watu wapole...wanaogopa kuhoji chochote kwa kuwa watawaudhi wakubwa....
 
Mnamzingizia mungu tu , ni kutokana na unafiki, fitina na ubinafsi uliowajaa ndio maana hamtoki, kazi uchawi na kuoneana choyo tu, uvivvu kibao !

Nimeuliza hivyo kwa kuwa tuliowengi tunaamini Mungu yupo na kwa imani hizo tunaamini kuwa ndiye aliyetujaalia uzima na rasilimali tulizo nazo. Iweje tushindwe kuzitumia ipasavyo kwa ajili ya faida yetu na vizazi vyetu badala yake tunafanyavitu vya kijinga na kupoteza muda kwa mambo yasiyo na nia ya maendeleo kama vile kugombania haki ya kuchinja na mengine kama hayo?
 
Mungu katuumba kwa mfano wake katupa uwezo wakutambua mabaya na mazuri sasa kama sisi uvivu tumeona ni mzuri na unafiki na ubinafsi basi tunajitia laana wenyewe kwa ujinga wetu wakukosa hekima yakutumia rasilimali tulizo nazo kiakili!
 
Kilichobaki ni kutubu makosa yetu kwa Mungu kama Taifa, napendekeza hili lifanyike kitaifa kabisaa siyo vikundi vikundi, hiyo moja pili ni hili ambalo nadhan ni muhimu kupita la kwanza kwa mtazamo wangu, ni kurudisha uhusiano mwema na Israel ingawa ina mgogoro na Palestina, Israel tupokee tu kama marafiki zetu na Palestina nao tuwapokee kama marafiki zetu tu kama wengine nadhan hao wote wawili watajenga heshima kwetu kwa jinsi tunavyowaheshimu wao baaaaasii.
 
Ni nchi iliyojaaliwa rasilimali nyingi kuliko hata nchi zilizoendelea kama Japani. Kati ya maajabu 7 ya asili Afrika matatu yamo Tz serengeti, ngorongoro, kilimanjaro. Ni nchi ya 3 Afrika kwa uzalishaji dhahabu, tuna kila aina ya madini ikiwemo Tanzanite ambayo ipo Tz pekee kwenye hii sayari.Tuna mbuga nyingi za wanyama,mito, ardhi nzuri ya kilimo.Tuna bahari, mito, maziwa makubwa kuliko nchi yoyote AfrikaTuna rasilimaliwatu ya kutosha45m. Pamoja na majaliwa yote hayo Tz ni nchi masikini sana na raia wake wanatafuta mali kwa viungo vya binadamu, wanauana kwa hisia za ushirikina,wanaendekeza udini,wamejikita kwenye wizi na ufisadi n.k. Kwa profile ya natural resources endowment tupo vizuri kuliko nchi nyingi kwenye sayari yetu lakinitunaongoza kwa umasikini na mambo ya kupuuzi na ushirikina. Hii laana tumemkosea nini Mungu waTz?

Tunapebda sana kuzunguuka point ya msingi.
Umasikini ni hali ya uhitaji wa mambo yote ambayo ungepaswa kuwa nayo. Umasikini ni Roho na ni laana kamili. Umasikini unatokana na kukosa kibali Mbele za Mungu. Kumbukumbu la Torati 28:15-28. Umasikini ni matokeo ya laana wakati wowote.
in this regard, watanzania tumelaaniwa kwa sababu tumemwacha Mungu. Tutamtafuta mchawi na hatutampata.

Soma, Kumb 28:15-
Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
16 Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.
17 Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia.
18 Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
19 Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo,
20 Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.
21 Bwana atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki.
22 Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.
23 Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma.
24 Bwana atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie.
25 Bwana atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani.
26 Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza.
27 Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.
28 Bwana atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;
29 utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.
30 Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake.
31 Ng'ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako, usile nyama yake; utanyang'anywa punda wako mbele ya uso wako kwa jeuri, usirudishiwe; kondoo zako watapewa adui zako, usipate mtu wa kukuokoa.
32 Wanao na binti zako litapewa taifa lingine, na macho yako yataangalia, na kuzimia kwa kuwatamani mchana kutwa; wala hapatakuwa na kitu katika uwezo wa mkono wako.
33 Matunda ya nchi yako, na taabu yako yote, vitaliwa na taifa usilolijua; utaonewa tu, na kupondwa chini daima;
34 hata uwe mwenye wazimu kwa yaonwayo na macho yako, utakayoyaona.
35 Bwana atakupiga magoti na miguu kwa jipu lililo zito, usilopata kupozwa, tokea wayo wa mguu mpaka utosi wa kichwa.
36 Bwana atakupeleka wewe, na mfalme wako utakayemweka juu yako, kwa taifa usilolijua wewe wala baba zako; nawe huko utatumikia miungu mingine ya miti na mawe.
37 Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza Bwana.
38 Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila.
39 Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu.
40 Utakuwa na mizeituni katika mipaka yako yote usijipake mafuta yake; kwa kuwa mzeituni wako utapukutika.
41 Utazaa wana na binti, lakini hawatakuwa wako wewe; kwa sababu watakwenda utumwani.
42 Miti yako yote, na mazao ya nchi yako, nzige watakuwa nayo.
43 Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe utazidi kushuka chini.
44 Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa mkia.
45 Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza;
46 nazo zitakuwa juu yako kwa ishara na ajabu, na juu ya uzao wako milele;
47 kwa kuwa hukumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote;
48 kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta Bwana juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza.
49 Bwana atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usiloufahamu ulimi wake;
50 taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana;
51 naye atakula uzao wa ng'ombe wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako mpaka utakapokwisha kuangamizwa; wala hatakuachia nafaka, wala divai, wala mafuta, wala maongeo ya ng'ombe wako, wala wana-kondoo wako, hata atakapokwisha kukuangamiza.
52 Naye atakuhusuru katika malango yako yote, hata kuta zako ndefu, zenye maboma, ulizokuwa ukiziamini, zishuke, katika nchi yako yote kila upande; naye atakuhusuru katika malango yako yote kila upande, katika nchi yako yote aliyokupa Bwana, Mungu wako.
53 Nawe utakula uzao wa tumbo lako mwenyewe, nyama ya wana wako na binti zako aliokupa Bwana, Mungu wako; katika mazingirwa na katika mkazo utakaokazwa na adui zako.
54 Mtu mume kati yenu aliye mwororo na laini sana, jicho lake litakuwa ovu juu ya nduguye, na juu ya mke wa kifuani mwake, na juu ya masalio ya wanawe waliosalia naye;
55 hata asitake wao mmojawapo apewe katika nyama ya wanawe atakaowala, kwa kuwa hana kitu kilichomsalia kwake; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako yote.
56 Mwanamke kati yenu aliye mwororo na laini, ambaye hangehatirisha kuweka wayo wa mguu wake nchi kwa umalidadi na ulaini, jicho lake huyu litakuwa ovu juu ya mume wa kifuani mwake, na juu ya mwanawe, na juu ya binti yake,
57 na juu ya mchanga wake atokaye katikati ya miguu yake, na juu ya wanawe atakaowazaa; kwa kuwa atawala kwa siri, kwa uhitaji wa vitu vyote; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako.
58 Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari na utisho, Bwana, MUNGU WAKO;
59 ndipo atakapofanya Bwana mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana.
60 Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe.
61 Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo Bwana juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa.
62 Nanyi mtasalia wachache kwa hesabu, ninyi mliokuwa mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi; kwa kuwa hukuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako.
63 Tena itakuwa, kama vile alivyokuwa akifurahi Bwana juu yenu kwa kuwatendea mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo atakavyofurahi Bwana juu yenu kwa kuwapoteza na kuwaangamiza; nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi mwingiayo kuimiliki.
64 Bwana atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe.
65 Wala katika mataifa hayo hutapata raha iwayo yote, wala hutakuwa na kituo cha wayo wa mguu wako; lakini Bwana atakupa huko moyo wa kutetema, na macho ya kuzimia, na roho ya kudhoofika;
66 na uzima wako utakuwa na wasiwasi mbele yako; nawe utakuwa na woga usiku na mchana, wala hutaamini kamwe maisha yako;
67 asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona.
68 Bwana atakurudisha tena Misri kwa merikebu, kwa njia ambayo nilikuambia, Hutaiona tena po pote; nanyi huko mtajiuza nafsi zenu kwa adui zenu kuwa watumwa na wajakazi, wala hapana atakayewanunua.
 
Kilichobaki ni kutubu makosa yetu kwa Mungu kama Taifa, napendekeza hili lifanyike kitaifa kabisaa siyo vikundi vikundi, hiyo moja pili ni hili ambalo nadhan ni muhimu kupita la kwanza kwa mtazamo wangu, ni kurudisha uhusiano mwema na Israel ingawa ina mgogoro na Palestina, Israel tupokee tu kama marafiki zetu na Palestina nao tuwapokee kama marafiki zetu tu kama wengine nadhan hao wote wawili watajenga heshima kwetu kwa jinsi tunavyowaheshimu wao baaaaasii.

Absolutely. Tukifanya hivyo kama taifa Mungu atatujazi. Kwenye kumbukumbu la torati,inavyosema...

Tena itakuwa, mambo haya yote yatakapokujilia, baraka na laana nilizoweka mbele yako, nawe utakapozikumbuka kati ya mataifa yote, huko atakakokupeleka Bwana, Mungu wako,
2 nawe utakapomrudia Bwana, Mungu wako, na kuitii sauti yake, mfano wa yote nikuagizayo leo, wewe na wanao, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;
3 ndipo Bwana, Mungu wako, atakapougeuza utumwa wako, naye atakuhurumia, tena atarejea na kukukusanya kutoka mataifa yote, huko alikokutawanyia Bwana, Mungu wako.
4 Watu wako waliotawanyika wakiwako katika ncha za mbingu za mwisho, kutoka huko atakukusanya Bwana, Mungu wako; kutoka huko atakutwaa;
5 atakuleta Bwana, Mungu wako, uingie nchi waliyomiliki baba zako, nawe utaimiliki; naye atakutendea mema, na kukufanya uwe watu wengi kuliko baba zako.
 
Mkuu, kweli kabisa...dawa ni toba tu mwanzo mwisho, hakuna njia yoyote itakayotuokoa zaidi ya hapo!
 
Mnamjaribu Mungu kujaribu kumfanya dikteta awe mtakatifu mnafikiri Mungu anapenda hayo?
 
Mungu hausiki na chochote naamini ni tamaa na uvivu na ujinga causing all this chaos
 
Mungu hausiki na chochote naamini ni tamaa na uvivu na ujinga causing all this chaos

Tamaa, uvivu na ujinga havizalishi dhambi mbele ya Mungu? hata Taifa nayo pia hupata adhabu kama Taifa, hii ipo kabisa
 
Ni nchi iliyojaaliwa rasilimali nyingi kuliko hata nchi zilizoendelea kama Japani. Kati ya maajabu 7 ya asili Afrika matatu yamo Tz serengeti, ngorongoro, kilimanjaro. Ni nchi ya 3 Afrika kwa uzalishaji dhahabu, tuna kila aina ya madini ikiwemo Tanzanite ambayo ipo Tz pekee kwenye hii sayari.Tuna mbuga nyingi za wanyama,mito, ardhi nzuri ya kilimo.Tuna bahari, mito, maziwa makubwa kuliko nchi yoyote AfrikaTuna rasilimaliwatu ya kutosha45m. Pamoja na majaliwa yote hayo Tz ni nchi masikini sana na raia wake wanatafuta mali kwa viungo vya binadamu, wanauana kwa hisia za ushirikina,wanaendekeza udini,wamejikita kwenye wizi na ufisadi n.k. Kwa profile ya natural resources endowment tupo vizuri kuliko nchi nyingi kwenye sayari yetu lakinitunaongoza kwa umasikini na mambo ya kupuuzi na ushirikina. Hii laana tumemkosea nini Mungu waTz?

Tatizo linajieleza katika post yako.

Tumejikita katika natural resources wakati katika knowledge economy natural resources bila human resources hazisaidii kitu.

Halafu kila kitu kumsingizia mungu, mungu mungu...
 
Back
Top Bottom