Lkn naamini wapinzani wangekua kwenye vyombo vya maamuzi makelele Yao yangewashitua watawala wangetafuta namna ya kulishughulikia swala hili na Watanzania tungepata afueni.
Umejichanganya mkuu! Wapinzani wanapigania;
- Uraia pacha wa watoto wao
- Ruzuku, inaingia mifukoni mwao
- Nafasi za mamlaka/madaraka
Uwe muungwana tu kusema, aliwahi kuwepo mtu aliyewahi kukerwa na hizo kero na akaonesha nia ya dhati kuzitatua, SIO WAPINZANI.
Unajua kuwa sukari imepanda, kisa mvua? Wapinzani wamefanya nini?
Unajua kuwa umeme ni shida, unaambiwa matengenezo, mara mvua hakuna, unakubaliana nayo hayo? Wapinzani wamefanya nini?
Unajua kuwa mamlaka za maji zimefeli vibaya, wapinzani wako kimya!
Unayo taarifa, nauli zimepanda, wao kimya?
Unajua kuwa hatuna dawa, hatuna chakula cha akiba? Bashe anakanya twende, wao wanafanya nini?
Ni mengi mno ya hovyo nchi hii, CCM wanatengeneza matatizo kwaajili ya maslahi yao...wapinzani wanapambania maslahi yao.
Niambie, maandamano ya kwanza kabisa waliyokusudia kufanya, dhima yake ilikuwa nini?