Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Nianze kwa kuwatakia heri na baraka tele ziwe kwenu mwaka huu wote wa 2017
Wakati wa uongozi wa awamu ya nne, wanafunzi wa vyuo vikuu walikuwa wakicheleweshewa hela zao za kujikimu kesho yake utawasikia wako mitaani wakiandamana kuelekea ikulu, awamu hii ni kama wote wamepata na inawajia kwa muda muafaka!
Wafanyakazi nao, ni kama nyongeza za mishahara walizokuwa wakililia na kupanga migomo ya hapa na pale awamu ya nne ni kama awamu hii yote yametimizwa! Hatusikii migomo wala maandamano bali malalamiko ya chini kwa chini!
Wanasiasa nao ndo kama mnavyoshuhudia tena, matamko na mbwembwe za hapa na pale za enzi zile za awamu ya nne kwa sasa kimya kabisa ezi ifu kuna asilimia Mia ya uhuru wa kisiasa!
Yaani kifupi, sisi wabongo kumbe tuna hulka ya kuwaonea watu na kuwapa wakati mgumu sana wale wanaonekana kutupa nafasi kubwa ya kusikiliza matatizo yetu!
Kumbe dawa yetu ni kupigwa mikwara kwenda mbele maana wakati mwingine nao makelele mengi ukiyasikiliza yanaweza kukumislead! Piga mikwara baba, kumbe watanzania wapole tu! Wanaangalia sura, mwenekano na kariba!
Wameshindwa kuwatetea wanakagera, wanafunzi waliokosa mikopo, wafanyakazi walionyima stahiki zao, wastaafu waliopunjwa na kunyimwa stahiki zao (ila kumbe wakilalamika kupitia magezeti wanasaidiwa kama yule wa gazeti la mwananchi badala ya kusaidiwa wote!)
Kumbe watanzania wanasoma nani wamfanyie mbwembwe za migomo na maandamano!