Watanzania tuliambiwa tuandamane tukakataa. Acheni tuendelee kudhalilishwa

Mifumo ikiwa mibovu watakula vipi sasa
Usijali hata hao walioiweka mifumo nao wamo mumohumo muda si mrefu (hata 20 years) wataungana na nyie kupinga hiyo mifumo mibovu na kuungama wasamehewe. Hapo ndio itakakua mwanzo mzuri
 
Wote mmemsikia Ndugai alivyokuwa anaongea kama "Mungu". Hii yoye ni kwa sababu watawala wameshajiridhisha sisi watanzania hatuna cha kuwafanya.

Tuliambiwa tudai haki yetu tukagoma. Na mimi nasema acheni tuendelee kuburuzwa maana tumezidi ukondoo.

Katiba iko wazi kuhusu ukomo wa ubunge pale anapokoma kuwa mwanachama wa chama kilichomsabibisha kupata ubunge. Ndungai hajali sheria na hakuna cha kumfanya.

Maskini Tanzania yangu.
Wanasiasa siyo wa kuwaamini, kama unaandamana kisa mwanasiasa kakuambia, huenda hadai haki yako anadai kula kwake. Hawa hawa akina Halima ndiyo nao walikuwa mstari wa mble kusema tuandamane, ila kumbe walikuwa wanasema tuandamane kisa walikosa ubunge. Muulize sasa Halima tuko tayari kuandama uone kama atatakubali.
 
Usijali hata hao walioiweka mifumo nao wamo mumohumo muda si mrefu (hata 20 years) wataungana na nyie kupinga hiyo mifumo mibovu na kuungama wasamehewe. Hapo ndio itakakua mwanzo mzuri
True.Lowasa, Sumaye,membe,Mkapa baada ya mfumo kuwatupa eti nao utamani katiba mpya Hali walipokuwa wakipigiwa kelele juu ya kuleta katiba mpya walikunja nyuso na wakaona haiwahusu. Hata kina jiwes and company siku mfumo ukiwatupa si ajabu watakuja kuandika vitabu pia wataitamani.
Wanasema watawala wa kiafrica huwa na akili baada ya mfumo kuwatupa.
 
Wote mmemsikia Ndugai alivyokuwa anaongea kama "Mungu". Hii yoye ni kwa sababu watawala wameshajiridhisha sisi watanzania hatuna cha kuwafanya.

Tuliambiwa tudai haki yetu tukagoma. Na mimi nasema acheni tuendelee kuburuzwa maana tumezidi ukondoo.

Katiba iko wazi kuhusu ukomo wa ubunge pale anapokoma kuwa mwanachama wa chama kilichomsabibisha kupata ubunge. Ndungai hajali sheria na hakuna cha kumfanya.

Maskini Tanzania yangu.
Aaah wapi, si kwamba hakuna cha kumfanya. Hili si Bunge la ugogoni. Ngoma ndiyo kwanza imeanza. Upumbavu ni mzigo. Ataondoka na zigo lake la upumbavu na kutuachia Bunge letu la JMT.
 
Wote mmemsikia Ndugai alivyokuwa anaongea kama "Mungu". Hii yoye ni kwa sababu watawala wameshajiridhisha sisi watanzania hatuna cha kuwafanya...
Ni kweli mkuu. Niliwahi kushauri humu kuwa dawa ni kuacha kabisa ule mtindo wa kitanzania wa kubebana kila mtu ajisimamie maisha yake. Hakuna kuombana chumvi, kibaba, wala chochote.

Mtu akipigika aachwe afe peke yake na wanaomuhusu. Kenya ukiwa kapuku unakufa njaa hakuna kubebana hovyo. Itafika mahali hadi kila mtu ahusishe machungu yake na watawala hawa fisi weusi.

Tutaelewana tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom