Kauli ya kuitwa 'wanyonge' ndio silaha hatari wanayoitumia viongozi ili wananchi wasitoke nje ya boksi

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,300
33,919
Tangu kuchaguliwa kwa John Magufuli kuwa Rais wa Tanzania, msamiati wa "wananchi wanyonge" umeleta mjadala mkubwa sana kwenye medani za siasa hapa nchini. Rais Mwenyewe amekuwa kila mara akihanikiza kwamba yeye ni "Rais wa wanyonge"

Ni nani hao watanzania wanyonge ambao kila mwanasiasa wa kitanzania anadai kuwatetea. Ni vigezo na sifa zipi walizonazo hao watanzania wanyonge na ni kwa nini wao tu ndiyo wanasiasa wanashindania kuwatetea?

Ni chama gani ama ni mwanasiasa gani ni nguli katika kuwapigania wananchi wanyonge!? Ni wakati gani hasa tutajua kama yanayofanywa yanafanywa kwa niaba ya wananchi wanyonge wa Tanzania?
 
Wamachimga, mamantilie, bodaboda, . Mimi siyo mnyonge sijawahi kunyongwa na mfumo Wa Utawala/Uongozi. Naweza kujitetea nazijua Haki zangu. Naishi kwa kutumia dola 10 kwa siku. Najua kusoma na kuandika. Ninalipa kodo kupitia Umeme, Maji, Road licence, jengo na kununua bidhaa dukani
 
DAB, jeska, muro na wengine wapenda mbeleko.

Sisi wengine tunapambana na hali zetu hata nyongeza za mwaka za mshahara zimepelekewa wanyonge.
 
Pia mkuu jumlisha na kauli kama 'wananchi masikini' kwa ukweli kwa sisi tunao amini kwamba maneno yanaumba hizi kauli za kusema wananchi wanyonge mara masikini zinaumba sana matukio ya unyonge na umasikini naamin kwa viongozi wetu watumie hata misamiati ya kutia moyo na matumaini

Afadhali hata msamiati wa 'nchi yetu tajiri will be donor country ' hata kama hauna uhalisia kwa sasa lkn ni wa matumaini angalau
 
Wanyonge ni walala hoi kama alivyokuwa anawaita Marehemu Mtikila (Wasukuma makwama,vibarua, wabeba zege..nk) sio Magabachori kama kina Manji.
 
Labda tuwaombe hao lumumba watuambie watanzania wanyonge ni watu gani?

Ova
Siwaoni wakitupa tafsiri ya wanyonge. Maelezo ya Mbuyimayi nyongeza ya "wananchi Maskini" nayo pia ni msamiati usiofafanuliwa na unajenga picha kwamba kuna watu wamezaliwa kuwa maskini.
 
Watanzania wanyonge ndio mtaji wa wanasiasa.... wanyonge kwa maana mafukara wasio na kipato cha kuaminika.
 
Back
Top Bottom