Watanzania tujiandae kisaikolojia

Watanzania tujiandae kisaikolojia

B.G TANTAWI

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
496
Reaction score
379
Lolote laweza kutokea mwaka 2015, Chadema wameapa kwa miungu wote kuwa lazima Waingie IKULU mwaka 2015, Chama cha Mapinduzi kinaapa kuwa Lazima kitaendelea kutawala kwa miaka 100 ijayo.

Wana Jf Tujadili haya masuala mawili, tusivutwe na ushabiki wa vyama vyetu, tujadili Uhalisia hapa,

Chama cha mapinduzi kimeongoza kwa zaidi ya miaka 50 sasa, lakini tumeona maendeleo iliyoyaleta na kama kawaida udhaifu haukosekani tumeona madhaifu yake.

Kuna watu hawapendi kuona na kukubali maendeleo hayo ila wamejikita zaidi katika madhaifu je hii ni sahihi?

Hebu Tuangalie Maendeleo ya CCM toka Uhuru, nakubali mni-challenge, au muongeze mengine zaidi,

Ingawa huduma za jamii ni haki yetu ya lazima kuzipata kutokana na kodi tunazotozwa lakini CCM imefanikiwa kuzijenga, au kuzianzisha na hapa naomba niwe very specific:

Barabara za lami zimetengenezwa-na zinaendelea kutengenezwa/kujengwa jamani mwenye macho haambiwi tazama, kutokea Musoma-Dar ni lami, Dar hadi Mbeya ni lami, Dar hadi Tabora ni lami, Dar hadi kilimanjaro ni lami, ongezeeni na zingine hapa.

UMEME: Ingawa umekuwa wa kusuasua lakini tunaupata maeneo mengi yana umeme na sasa wameanza kuupeleka Vijijini, jamani mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Hospitali zimejengwa ingawa kuna malalamiko hapa kuwa dawa hazipo, hazitoshi, wazee wanatozwa pesa badala ya kutibiwa bure, akina mama wajawazito wanatozwa pesa, ila wamejitahidi hizi ni changamoto.

Elimu, hapa napo CCM imejitahidi kuna shule nyingi, vyuo vikuu na vyuo vya kawaida hapa napo wamejitahidi sana ingawa kuna changamoto nyingi kama vile Ubora wa elimu, maslahi ya walimu nk. ongezeeni.

Maji: wamejitahidi sana na wanaendelea kujitahidi kuwapatia maji wananchi.

CCM inataka iendelee kutawala, unadhani sasa ni bora iendelee kutawala nchi kwa mafanikio hayo na changamoto hizo na zingine?

Kwa maoni yangu mimi hapa nina majibu mawili ya ndiyo iendelee na hapana isiendelee, kwa nini?

Ndiyo iendelee kwa sababu,

Kwa sasa, hapa nchini kilichobaki ni changamoto tu na siyo matatizo, kwa mfano, Elimu tunayo ila changamoto ni Ubora, maslahi bora ya walimu nk. hatuna matatizo hapa, hivyo hivyo katika Maji, Barabara, n.k.

Hapana isiendelee, hapa ni kwamba tunahitaji mtu au watu wenye maamuzi na utashi wa ku-shughulikia hizo changamoto, kwa mfano, Mitaala ya Elimu hii ahiitaji fedha ni maamuzi tu, maslahi ya walimu hapa ni maamuzi tu unadhibiti matumizi yasiyo ya lazima kwa mfano, Ununuzi wa Shangingi, kudhibiti mianya ya rushwa, kusimamia raslimali za nchi ipasavyo kwa manufaa ya wananchi wako, kukusanya kodi pasipo kumwogopa mtu au chama. hapa ni maamuzi tu!

Sasa je, Ndani ya CCM tunaweza kupata mtu mwenye uthubutu huu wa kushughulikia hizi Changamoto kati ya hawa wafuatao?

Bernad Membe---Mbunge wa Mtama--JIMBO lake amelifanyia nini toka amekuwa Mbunge? je Kuna barabara za lami au nzuri? je kuna maji? Huduma za afya zipo? nyota njema huonekana asubuhi. Je nje ya Jimbo lake watanzania mnamuonaje?

John Pombe Magufuli---Mbunge wa Chato--Jimbo lake kalifanyia nini? je kuna Barabara, Maji, huduma za afya,vp Elimu jimboni mwake? Je nje ya jimbo lake watanzania mnamuonaje?

Samweli sita----Mbunge wa Urambo---Jimbo lake kalifanyia nini? Je kuna barabara, Maji, Huduma za Afya, vp Elimu? Je nje ya jimbo lake watanzania mnamuonaje?

Edward Lowasa---Mbunge wa Monduli---Jimbo lake kalifanyia nini? Je kuna barabara, Maji, Huduma za afya, vp Elimu? Je nje ya jimbo lake watanzania mnamuonaje?

ROSE MIGIRO---jimbo lake kalifanyia nini? Watanzania mnamuonaje nje ya jimbo lake?

Emmanuel Nchimbi--Jimbo lake kalifanyia nini? watanzania mnamuonaje nje ya jimbo lake?

Je ikiwa hawa mmojawapo akapewa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM je ataweza kukabiliana na changamoto hizo?

Hakika tuna changamoto nyingi sana na hizi hapa ni mojawapo:

Mfumuko wa bei za vitu, Tunahitaji Rais mwenye uwezo wa kupambana na mfumuko wa bei za vitu kama vile Mchele, sukari, mahindi nk. njia rahisi ya kupambana na hili ni kuandaa mashamba makubwa ambayo yatasimamiwa na JKT, kazi yao itakuwa ni Kulima kwa Tracta mahindi, maharage, mchele nk. hecta 1000 au zaidi huko kilombero, Mbeya, iringa nk. na kulisha nchi. hili linawezekana ikiwa wadau watashilikishwa ipasavyo ili kutoathili wakulima wadogo wadogo
na ziada tunauza nje ya nchi.

CCM wakitaka kutawala miaka 100 na zaidi lazima wananchi wa kawaida wale vizuri na wawe na uwezo wa kununua chakula kwa bei nzuri!

kisaikolojia, mtu akiwa anakula vizuri na anapata mahitaji yake kwa urahisi mtu huyo hatakuwa anawaza-waza!

Utawala bora: hapa lazima tupate Rais mwenye kuthubutu ambae atakuwa na uwezo wa kupambana na rushwa kwa vitendo, madawa ya kulevya, matumizi mabaya ya fedha za umma, kuchukua hatua kali dhidi ya wahujumu uchumi, watendaji dhaifu, nk.

Ajira.

Viwanda.

Kuthubutu..

Ongezeeni na zingine........

Je kati ya hao nani anaweza kupambana na changamoto hizo?

Chadema wanataka mwaka 2015 waingie ikulu, kuweza wanaweza je wanaweza kupambana na changamoto hizo? ingawa sijajua Chadema wanaziitaje, ni Matatizo au changamoto, lakini wanaenda ikulu kufanya nini?

Ingawa hawajawahi kuingia ikulu na ndo huenda ikawa mara yao ya kwanza kwa hiyo hatuwezi kuwahukumu ila tuyaangazie majimbo yao, hawa wanatajwa tajwa kuwa huenda watagombea Urais,

Dr. W. P. Slaa--Jimbo la Karatu toka mwaka 1995-2010 je Jimbo lake amelifanyia nini? kuna barabara za lami, Maji, Umeme, huduma za afya je? Je nje ya Jimbo lake watanzania mnamuonaje?

Mbowe Aikael--Jimbo lake Hai, je jimbo lake kalifanyia nini? watanzania mnamuonaje nje ya Jimbo lake?

Kabwe zuberi zito--Jimbo lake Kigoma kaskazini, Je jimbo lake kalifanyia nini? Watanzania mnamuonaje nje ya jimbo lake?

Note: Acheni ushabiki wa vyama katika kuchangia thread hii, tuwe analytical, logical etc. Tanzania ni yetu sote na sote tuna nia njema na nchi yetu, sote tutaondoka hapa duniani tutawaacha watoto, wajukuu na vitukuu vyetu, please jadilini kwa hoja kama una mshawasho na chama chako acha kuchangia.

CCM oyee! Chadema oyeee!
 
...daaah ! we jamaa..? ningoje kwanza...
 
DR.Slaa, Mbowe na Zitto walishawahi kukusanya hata senti moja ya Kodi katika nchi hii?
 
Nyama, dagaa, bamia, mchicha, kabechi, samaki! Vyote chungu kimoja.

Kiswahili cha kisiasa, eti rushwa ni takrima! Matatizo ni changamoto!
 
Zitto ameshasema afikirii kugombea tena si ubunge wala Urais na ametutahadharisha tusiwaamini wanasiasa si wakweli si watawala wala wapinzani! Salute kwako kaka Zitto
 
Last edited by a moderator:
kuhusu kuungana hiyo habari sahau,kuna watu wameinvest kwenye vyama wanategemea returns,si umeona kambi ya upinzani bungeni? muungano wa sasa ni POLITICAL GAME
DR.Slaa, Mbowe na Zitto walishawahi kukusanya hata senti moja ya Kodi katika nchi hii?
Wanapojinadi majimboni chagua mbunge ccm/chadema akuletee maendeleo wanamanisha nini? POROJO !!
 
Safari ya mageuzi tunajau iliponzia. Itakapoishia na huu ukaidi wa chama watawala is anybodies guess.
 
kuhusu kuungana hiyo habari sahau,kuna watu wameinvest kwenye vyama wanategemea returns,si umeona kambi ya upinzani bungeni? muungano wa sasa ni POLITICAL GAME
Wanapojinadi majimboni chagua mbunge ccm/chadema akuletee maendeleo wanamanisha nini? POROJO !!

Mwanzoni niliwaamini sana wanasiasa lakini sasa....... Msiwaamini wanasiasa Zitto
 
Last edited by a moderator:
Kiongozi, unaposema elimu ipo ila tatizo ni ubora unamaanisha nini? kuna watoto wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika, kwa hawa unamaanisha kwamba wameelimika ila katatizo ni ubora? alafu mkija kuboresha mtawaboreshea vipi hawa? unaelewa madhira ambayo watakutana nayo hao watoto siku usoni? na ukumbuke hili linatokea kwa mara ya kwanza katika taifa hili toka tupate uhuru, je unategemea tukiwaachia ccm wakabidhi serikali ya awamu ya tano kwa ccm ni nini kitatokea katika sekta elimu?

unasema kuna vyuo, unajua maana ya chuo kikuu wewe? University? unaweza kugoogle hapo uelewe maana ya universe ni nini? wanachuo wetu wanapata universal education? kwamba tatizo ni ubora, mkija kuboresha mtaboresha kwa hao watu?

unazungumzia barabara, unajua hizo barabara zitadumu kwa muda gani? mwaka juzi nilisafiri kwa basi kutoka dar kwenda arusha barabara yote ilikuwa imewekwa rami, wiki juzi nimepita barabara hiyo hiyo nimekuta kuna kipande kikubwa sana kinarudiwa, unajua ni nani analipia kurudiarudia hizo barabara? unajua kwamba mpaka leo kuna barabara zimeachwa na wakoroni zikiwa na ramani na mpaka leo zina rami? kwa nini zinazotengenezwa sasa zinadumu miaka miwili? Ninaishi tabata huu mtaa wenye chuo cha mama rwakatare , barabara hii imewekwa rami mwezi wa nne, unajua kwamba mwezi wa sita ilifanyiwa ukarabati baada ya kuharibika ndani ya miezi miwili tu baada ya mkandarasi kumaliza kazi? unajua nani analipia hizi barabara? ni kilometer ngapi zinazotajwa kila siku ambazo zimefanyiwa upumbavu huu?

Anyway
Mimi hoja yangu ya msingi ya kutaka hawa watu waondoke ni kwamba hawajui majukumu yao, ni waganga njaa tu, na ni aibu na fedheha kubwa sana kwamba imetokea wamepata fursa za namna hii, tena kwa kipindi kirefu namna hii.

Wameshindwa kutengeneza maziringa kwa watanzalnia kuweza kuboresha maisha yao. wameshindwa na wanastahili kuondoka.
 
viongozi wa sasa na wachama kilichopo madarakani wanatengeneza famlia zao za badae sio taifa lao labadae awatufai
 
Kwa jinsi Mungu alivyoijalia nchi yetu raslimali lukuki na nyingine ambazo hazipatikani sehemu yeyote hapa duniani,labda na ulimwenguni kote. Nanaweza kukonclude kwamba kwa miaka 50 ambayo ccm imetawala nchi yetu maandeleo yaliyopatikana kwa wananchi kwa ujumla ni kuduchu sana ukilinganisha raslimali tulizonazo.
Kwa kipindi cha miaka 50 ya utawala wa CCM tumeshuhudia watendaji wakuu wa serikali ambao wengi wao ni wanachama wa CCM, Wanasiasa wenye vyeo vya juu ndani ya CCM na wafanyabiashara wakubwa waliojificha CCM wanavyojinufaisha kwa raslimali za nchi hii bila kuwafikiria wananchi wa kawaida walio wengi.
Inasikitisha sana kusikia mwanasheria mkuu wa serikali ambaye baadae aligeukia ubunge mzee wa vijisenti kuficha fedha nchi za nje kinyume cha utaratibu na kudai ni vijisenti bila kuchukuliwa hatua wakati sheria ipo wazi,
Inasikitisha na kufurahisha sana kusikia kwamba mzee madiba kakataa kuhudhuria uzinduzi wa jumba la ghorofa ambayo Rais mstaafu wa nchi hii amejengewa na wawekezaji wa Afrika kusini katika mazingira ya utata.
Inasikitisha sana kusikia kwamba rais wa nchi anawasamehe wezi walioiba fedha za serikali za akaunti ya nje , nadhani labda angesubiri wafungwe na ndipo awasamehe kwenye sherehe za uhuru hapo kidogo ningemwelewa.
Inasikitisha sana kusikia kwamba kuna wajinga wametorosha wanyama wetu akiwemo Twiga wazimawazima.Wakati Serikali inayojiita makini ya ccm imezubaa.
Inasikitisha sana kuona watendaji wakubwa serikalini na kwenye chama cha CCM walivyokuwa na ukwasi mwingi kupita wafanyabiashara lukuki ambao wanafanya biashara zao kihalali, inashangaza sana watu hawa Mf. Bw Ezekie Maig kununua nyumba ya thamani ya zaidi ya M700. hivi kwa kipato cha wapi? Au bwn Lukuv kununua nyumba kwa Tsh Milion 800 na kisha kuibomoa na kujenga nyingine kwa thamani ya zaidi ya 1 Bilioni Tsh
Inasikitisha sana kusikia kuna watu wanajenga jengo la ghorofa nyingi karibu na Ikulu yetu hadi linakamilika na kuanza kutumika kinyume cha utaratibu.
Inasikitisha sana kusikia IGP anaibiwa upanga wa dhahabu ofisini kwake katika mazingira ya kutatanisha.
Namalizia kwa kusema kwamba kuna madudu mengi sana yamnafanyika kutokana na CCM kushindwa kutawala na kuwasimamia watendaji wa Serikali.
Kwa mtazamo wangu ningependelea kuona chama cha CCM kinapumzika ili kuachia nafasi kwa chama kingine kuongoza nchi hii.
CCM wameshindwa kusimamia vizuri rasilmali za taifa hili na kuwawezesha watanzania kuishi maisha mazuri.
 
Kiongozi, unaposema elimu ipo ila tatizo ni ubora unamaanisha nini? kuna watoto wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika, kwa hawa unamaanisha kwamba wameelimika ila katatizo ni ubora? alafu mkija kuboresha mtawaboreshea vipi hawa? unaelewa madhira ambayo watakutana nayo hao watoto siku usoni? na ukumbuke hili linatokea kwa mara ya kwanza katika taifa hili toka tupate uhuru, je unategemea tukiwaachia ccm wakabidhi serikali ya awamu ya tano kwa ccm ni nini kitatokea katika sekta elimu?

unasema kuna vyuo, unajua maana ya chuo kikuu wewe? University? unaweza kugoogle hapo uelewe maana ya universe ni nini? wanachuo wetu wanapata universal education? kwamba tatizo ni ubora, mkija kuboresha mtaboresha kwa hao watu?

unazungumzia barabara, unajua hizo barabara zitadumu kwa muda gani? mwaka juzi nilisafiri kwa basi kutoka dar kwenda arusha barabara yote ilikuwa imewekwa rami, wiki juzi nimepita barabara hiyo hiyo nimekuta kuna kipande kikubwa sana kinarudiwa, unajua ni nani analipia kurudiarudia hizo barabara? unajua kwamba mpaka leo kuna barabara zimeachwa na wakoroni zikiwa na ramani na mpaka leo zina rami? kwa nini zinazotengenezwa sasa zinadumu miaka miwili? Ninaishi tabata huu mtaa wenye chuo cha mama rwakatare , barabara hii imewekwa rami mwezi wa nne, unajua kwamba mwezi wa sita ilifanyiwa ukarabati baada ya kuharibika ndani ya miezi miwili tu baada ya mkandarasi kumaliza kazi? unajua nani analipia hizi barabara? ni kilometer ngapi zinazotajwa kila siku ambazo zimefanyiwa upumbavu huu?

Anyway
Mimi hoja yangu ya msingi ya kutaka hawa watu waondoke ni kwamba hawajui majukumu yao, ni waganga njaa tu, na ni aibu na fedheha kubwa sana kwamba imetokea wamepata fursa za namna hii, tena kwa kipindi kirefu namna hii.

Wameshindwa kutengeneza maziringa kwa watanzalnia kuweza kuboresha maisha yao. wameshindwa na wanastahili kuondoka.

Mkuu Sangara nashukuru kwa maoni yako mazuri sana, ni kweli kabisa kuwa barabara za cku hizi hazidumu, na barabara ya tabata hiyo naifahamu sana nakubaliana na wewe mkuu, na hiyo ya Arusha naipata mkuu.
 
Sasa kinachokufanya utumie muda wako kuandika habari za barabara ni nini? Mi nimetoka kijijini juzi, ndugu zangu wamepigika na maisha kiasi kwamba ngozi zao zimekuwa kama miti alafu unakuja kuandika huku kwamba kuna changamoto? changamoto kwa nani? usitake kuniharibia weekend yangu aisee.
 
Yangefanyika mengi zaidi ya hayo. Kumbuka ufisadi kamawa EPA na mafedha yaliyofichwa nje ya nchi kama mifano halisi kuwa maendeleo hayo unayosema ni kiduchu! Bila ufisadi CCM ingefanya mengi!
 
jambo moja ujue na uliweke kwenye akili yako na ufahamu: nchi hii si mali ya chama cha siasa kiwacho chochote. ni mali yetu Watanzania.
 
Tatizo ni kwamba, wanasiasa wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuwaaminisha wananchi kwamba wao ndio wanahaki ya kuelekeza nchi hii inaendeshwa namna gani, kiasi kwamba makundi mengine yote yanaonekana hayafai.
 
Back
Top Bottom