Watanzania tubadilishe mfumo tulionao

Watanzania tubadilishe mfumo tulionao

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
17,920
Reaction score
24,756
Tumekuwa kichekesho kwa mataifa ya Afrika na dunia kwa ujumla. Tanzania lilikuwa taifa lililo mstari wa mbele Afrika kwa wale mnaokumbuka miaka ya 1980 mwanzoni na Nyerere alikuwa mwanzilishi na mwenyekiti wa nchi zilizokuwa mstari wa mbele barani Africa. Tanzania ilikuwa ikisaidia nchi za Afrika kujikomboa na wakoloni. Tanzania tulikuwa tunaongoza kwa demokrasia na amani.

Siku hizi tumeishia kuwa taifa llisiloweza hata kutoa takwimu halisi za magonjwa, tumeishia kuwa watu hata wakushindwa kushika na kuongoza zile nafasi za msimu za uenyekiti wa taasisi za kimataifa.

Tanzania tumekuwa siku hizi hata kwenda hapo Ethiopia kuhudhuria mikutano tunashindwa, usiseme kuvuka bahari ndio kabisa imekuwa kama mwiko. Tumekuwa taifa la kujifanyia mambo kienyeji enyeji.

Nyerere angekuwa hapa angeshangaa mno jinsi bunge lilivyogeuzwa taasisi ya chama cha siasa. Angeshangaa mno jinsi viongozi wanavyosujudiwa, angeshangaa mno jinsi upendeleo wa wazi unavyofanyika kila mahali. Nchi hii ilikuwa kimbilio lakini tunaona sasa tunaanza kukimbiwa na kuwekwa katika orodha ya nchi sisizokuwa na uhuru wa kuongea wala haki za msingi za binadamu.

Watanzania tuwe makini tuache ulimbukeni wa kumshabikia mtu au chama bila kujua madhara tunayopata. Tunahitaji kujenga mfumo imara na sio kutegemea matamko ya viongozi wetu. Tukiacha hali inavyokwenda sasa tutajuta sana lakini tutakuwa tulishachelewa.
 
Kwani hao tuliowasaidia wanasemaje kuhusu hili!!!au tulitumia nguvu kubwa kutaka tuonekane wema sana.
 
Back
Top Bottom