Tangu tupate Uhuru,wafuatao waliitwa marais madikteta Tz:Nyerere,Mkapa na sasa Magufuli.Marais wafuatao waliitwa Marais dhaifu:Mwinyi na Kikwete.Watanzania wamekuwa na kawaida sasa akitoka rais wanayemwita dikteta anayefuata ni yule wanayemwita dhaifu.Kila anayeondoka Watanzania humtukana aidha kwa udikteta wake au udhaifu wake.Nyerere walimwita "haambiliki" kutokana na kutopenda kuchukua ushauri aliokuwa anapewa.Mwinyi alidhihakiwa na kuitwa "mzee ruksa" kwa kuruhusu kila kitu.Mkapa aliitwa "mbabe na dikteta" kutokana na misimamo yake.Kikwete akaitwa "rais dhaifu" kwa kuruhusu sana demokrasia ifanye kazi.Magufuli sasa anaitwa "dikteta" na kuwa hasikilizi ushauri.Kwa fomula hii,rais atakayefuata atakuwa rais atakayeitwa "rais dhaifu". Akatayefuata baada yake atakuwa dikteta.Lakini wote wataondoka wanatukanwa kwa udikteta wao au udhaifu wao.WATANZANIA TUAMUE,TUNATAKA RAIS DIKTETA AU DHAIFU.