Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,443
- 113,452
MkuuPascal Mayalla,
Hivi ni kweli kwamba eneo lililokumbwa na njaa itokanao na ukame wa muda mrefu litaneemeka likikumbwa na mafuriko ya El Nino na Tsunami?
Tunafahamu kuwa ukame ni ukosefu wa maji wa muda mrefu, na mafuriko husababishwa na maji mengi. Sasa je, hao waliokuwa hawana maji miaka na miaka, sasa wakipata maji in form of mafuriko wataita hiyo neema au balaa jingine?
Penye ukame watu hawapandi wala kuvuna kwa kuwa maji ni muhimu sana. Je penye mafuriko watu watapanda na kuvuna?
Je penye mafuriko, hyumba za wale wachovu wenye njaa zitabaki zimesimama?
Vipi wale watoto walegevu, hawatasombwa na maji kweli?
na magonjwa ya milipuko yatawaacha watu kweli mafuriko yakijiri?
Kama wewe ndiye mwenye mamlaka ya kuwaletea neema hao viumbe waliokumbwa na ukame miaka mingi, je utawaletea mafuriko (maji mengi) ili kufidia ukosefu wao wa maji wa miaka mingi?
Au utawaletea maji yaliyo sawa na mahitaji yao ili wapate kunywa, kufua, kulima, kupanda na kuvuna?
Utotole
hii falsafa ulioitumia hapa ni ya kiwango cha juu kuliko level yangu. Nimetoka kapa!.
Paskali