Watanzania tuamue tunataka Rais Dikteta au dhaifu

Why utulimit kati ya hao wawili wa ovyoovyo? Eti Dhaifu vs Dikteta... Hatuwezi kuwa na Raisi jasiri, mwerevu, mwanademokrasia na mwenye hekima? Hawa hatuwapendi to that extent
Unataka kusema wote waliopita hawakuwa na sifa hizi?.Nani kati ya Watanzania unaowajua ana sifa hizi?
 
Tangu tupate Uhuru,wafuatao waliitwa marais madikteta Tz:Nyerere,Mkapa na sasa Magufuli.Marais wafuatao waliitwa Marais dhaifu:Mwinyi na Kikwete.Watanzania wamekuwa na kawaida sasa akitoka rais wanayemwita dikteta anayefuata ni yule wanayemwita dhaifu.Kila anayeondoka Watanzania humtukana aidha kwa udikteta wake au udhaifu wake.Nyerere walimwita "haambiliki" kutokana na kutopenda kuchukua ushauri aliokuwa anapewa.Mwinyi alidhihakiwa na kuitwa "mzee ruksa" kwa kuruhusu kila kitu.Mkapa aliitwa "mbabe na dikteta" kutokana na misimamo yake.Kikwete akaitwa "rais dhaifu" kwa kuruhusu sana demokrasia ifanye kazi.Magufuli sasa anaitwa "dikteta" na kuwa hasikilizi ushauri.Kwa fomula hii,rais atakayefuata atakuwa rais atakayeitwa "rais dhaifu". Akatayefuata baada yake atakuwa dikteta.Lakini wote wataondoka wanatukanwa kwa udikteta wao au udhaifu wao.WATANZANIA TUAMUE,TUNATAKA RAIS DIKTETA AU DHAIFU.

Kwanza hakuna maendeleo wala mafanikio kwa serikali kuongozwa na ccm.

No matter nani anatawala kutoka ccm. Ccm ni mauti ya taifa. Kuwaambia watu wachague nani kati ya dhaifu na dikiteta kutoka ccm, ni kuwaambia wachague wanataka kufa kifo kimoja kati ya kifo cha moto au kifo cha maji.

Kama vile mauti ni ileile, hata ccm ni ileile inayoua nchi kwa nji a nyingi.
 
Tunataka Rais mwenye kujali wananchi wake:

A - Huduma za Afya Kwanza (Madawa Hospitalini yawepo ya kutosha na chanjo)

Sasa tunakata Bima ya Afya ya TAIFA, halafu unaandikiwa nenda pharmacy --

B- Mikopo kwa wanafunzi wote walio dahiliwa na TCU kuingia chuo kikuu

Kumbuka ni Mkopo.. na sio Msaada

C- Kutengeneza ajira

D - Nishati kuwa nafuu

E - Kukusanya kodi kwenye Madini na Gesi

F - Uhuru wa Kujieleza

G- PESA YA KAGERA iende kwa wahusika

H - FAO LA KUJITOA PPF

NA HUO Udikteta tuuone kwa Mafisadi akina LUGUMI, ESCROW, na Majambazi

Hatutaki ujinga wa kushikia bunduki Watanzania wasio hata na kisu mkononi

Mpelekee hii Habari Mzee JPM, Ni Ushauri tu
Hio B ikitekelezwa hayo mengine pesa za kuyatekeleza zitatoka wapi??? Watu wenyewe hamtaki kulipa kodi...mkibinywa tu kidogo mnalialia oooh tunakamuliwa visababu vingiiii....
 
Neither of them,

Tunahtaji rais mwerevu ambaye anaweza ku "serve the best for last" Maana tumechelewa.

Pia ni vigumu kufahamu kias cha uzuri wa rais aliyepo, kipimo ni kura 2020, ingawa kwa kawaida aina ya rais km Magufuli kura zake ztaongezeka kwa kuwa anagusa matarajio ya kundi kubwa la watanzania km ilivyotokea kwa Mkapa kupanda chart na si kushuka km ilivyomtokea Kikwete
Umemaliza kila kitu na ngoja niishie hapa kwani ambaye hajaelewa ni kilaza
 
Rais msikivu anayeheshimu katiba na sheria za nchi.
Rais anayejali maslahi ya nchi siyo kukaa kimya kwenye issue muhimu za Taifa kama ufisadi wa Lugumi, escrow, kivuko cha bagamoyo, vyeti fake vya Bashite na uvamizi wake, anayelipa kodi kama Watanzania wengine. Anayekubali kushauriwa. Asiyeongoza nchi kwa vitisho na kejeli na pia asiye muongo.
 
Unataka kusema wote waliopita hawakuwa na sifa hizi?.Nani kati ya Watanzania unaowajua ana sifa hizi?
Soma nilichoandika sio kunilisha maneno... wewe dada vipi? Nani anaongelea waliopita au hujui hoja iliyo mezani ni ipi?
 
Adui wa nchi hii ni Ujinga, Maradhi na Umaskini na ndio visabishi vya Maendeleo Duni. Na ili tuendelee tunahitaji mambo manne. 1. Watu 2. Ardhi 3. Siasa Safi 4. Uongozi Bora.
Tutafute mtu wa kuyasimamia hayo.
 
Kwa kifupi rais dikteta hatakiwi.Tunataka rais mwenye maamuzi magumu na msikivu kwa wananchi.
 
tumebadili gia angani kwasasa tunamtaka rais dhaifu na Ndio maana tunakumbuka utawala wa jk.
 
Tunataka rais anayeheshimu katiba aliyoapa kuilinda. Baaasi
Tena hakuapa kuilinda tu, aliapa pia kuitetea na ndio maana akakabidhiwa vyombo vya kumwezesha kufanikisha hilo jukumu la kulinda na kutetea hiyo Katiba. Kiongozi tuliye naye hivi sasa kashindwa kuilinda wala kuitetea na badala yake kwa jeuri akaamua kuivunja...kitendo hicho ni sawa uhaini na ni uhalifu usiosameheka kwani kunahatarisha hatma ya taifa.
 
Back
Top Bottom