Watanzania sisi sio creative including Viongozi wengi wa serikali

Basham

JF-Expert Member
Oct 10, 2014
743
429
Amani iwe kwenu wanaJF

Kama heading inavosomeka, watanzania tumekua tukiitegemea sana serikali kwa kila kitu bila ya sisi kujituma katika kujitafutia ili kujikimu na ugumu wa maisha unaikabili nchi yetu.

Pia viongozi wetu wameshindwa kubuni njia mbadala ya kijipatia vyanzo vya fedha mbali na kutegemea Ruzuku kutoka serikali kuu, Kwa mfano Wakurugenzi wetu wangekua watu ambao ni wabunifu na kutengeneza vyanzo vingine vya mapato kwa kila halimashauri zingejiendesha vizuri sana. Zaidi ya vyanzo vile vile ambayo ni vya miaka nenda rudi na havikidhi mahitaji au bajeti ya halimashauri

Ongezea na Mengine, Yangu ni hayo tu

Nimewaza tu kwa uelewa wangu
 
Mleta mada nilitegemea wewe ungelitaja baadhi hivyo vyanzo vingine lakini kumbe anayeliona tatizo naye ana tatizo lile lile analolizungumzia!!
 
CHADEMA ni creative? Mbona walishindwa uchaguzi wa raisi na mbona wanaishi kwa kutegemea ruzuku ya serikali tu
 
Siri ya ubunifu ni uhuru
watu wajione huru kukataa chochote na kuanzisha chochote
bila uhuru hakuna ubunifu
 
MTOA MADA NI SEHEMU YA TATIZO. iMAANA HADI UNAANDIKA UJAONA SOLN HATA MOJA, TENA UNAOMBA WATU WAONGEZEE MATATIZO
 
MTOA MADA NI SEHEMU YA TATIZO. iMAANA HADI UNAANDIKA UJAONA SOLN HATA MOJA, TENA UNAOMBA WATU WAONGEZEE MATATIZO
Sio waongeze matatizo bali waongeze njia za kutatua matatizo
Kwa mfano unaruhusu machinga kufanya biashara popote kwa nini wasijengewe mazingira mazuri ya biashara na wawekewe sera za kuwalinda sio kila siku wanayumbishwa serikali itajipatia kodi,
 
Mkuu tambua zaidi ya 85% ya watanzania nimaskini na wanaishi vijijini.
Na katika 15% iliyobaki 10% ni waoga na wachumia tumbo hawajajikita katika ubunifu, ni watu wa kuyachukulia maisha mwisho waje ni kumiliki gari, nyumba na kuzaa full stop. Sasa usitegemee kwa mfumo huu watapatikana wabunifu.. Maybe after 200 yrs to come.. <3
FANYA YAKO, AFRICA & TANZANIA NI PASUA KICHWA.. May be ndio tunabeba laana na maovu ya dunia nzima
 
Serikali inatakiwa iweke mifumo ya kuwapa watu nafasi ya kutoa michango na mawazo yao katika kutumia ubunifu wao na haki milki pia, Itoe nafasi kwamba kila mwenye mawazo au ubunifu wowote serikali inamsaidia Mtaji
 
Back
Top Bottom