Watanzania ni watu wenye wivu mno

Watanzania ni watu wenye wivu mno

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,202
Sijawahi ona kwa nini sisi watanzania ni Watu wenye wivu sana,

Wakikuona una matatizo Kiuchumi watakuhurumia Machoni pao tu ila wakiwa pembeni wanakucheka.

Ukikomaa na kupiga hatua kadhaa za mafanikio, Majungu na Maneno yataanza, mara mchawi, mara mwizi, mara Jambazi, mara fisadi, Huwa wanasahau kabisa ule wakati wako uliokuwa unaangaika na tatizo/Shida zako.

Watanzania sisi ata umchukue mtu mahala pa chini na kumpa msaada/ kazi ya kufanya bado akikuona unafanikiwa lazima akuonee Wivu na kukuombea mabaya.

Huu Wivu huwa tunatoa wapi? Hatutaki kuona wale tuliowasaidia kuwa juu zaidi yetu,
Hatutaki kuona wale waliotusaidia kuendelea kuwa juu zaidi ya sisi tuliosaidiwa kwa nini?.

Wivu ndio unafanya tusiendeleee,Ni wivu tu hakuna kingine,
Jirani ana wivu, Ndugu ana wivu, Rafiki wana wivu, kila sehemu ni Wivu maendeleo tutayapata wapi?

Jana uliniona mimi zero IQ nauza mishikaki ukawa unapita na kunipa moyo ili nizidi kupambana, leo nimedunduliza kahela kangu na kufungua kibanda cha kiepe unapita huku umenuna kuona vile nimepiga hatua moja mbele kukuzidi wewe.

Wivu wote huo unatoka wapi, Kwa nini tusishindane kwenye Wivu wa maendeleo,
Leo mimi nimefungua duka la reja reja, wewe kesho fungua Duka la vitu vya Jumla,

Leo mimi nimenunua piki piki ya kutembelea, wewe kesho nunua IST yako, Tushindane kwenye Wivu wa vitu ili tufanye Maendeleo. Tusishindane kwenye Wivu wa kurudishana Nyuma.

Cc Zero IQ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zero IQ,
Ni kweli, majitu mengi yana wivu na roho mbaya sana. Kuna wakati nilifikiri elimu inasaidia, wapi! Mashetani ya Tanzania yenye wivu,chuki na roho mbaya yapo kwenye matabaka yote. Limtu hujalikosea kitu wala kulidhulumu lakini linakuombea hata ufe tu, kisa una mafanikio fulani. Mimi ni victim wa hili jambo, nimeumizwa sana.
 
Haha pole sana mkuu, hii ipo sana, na wengine wanaogopa kumsaidia mtu kwakuwa anajua akikusaidia basi unaweza pita mafanikio yake.
 
Hilo ni tatizo LA mwanadamu.
Hata Israel ilipovamiwa na kubomolewa na wababeli majirani zao Edom walifurahi mno japo Israel haikuwahi kuwakosea.

Kuwa imara usikubali hayo yakakuathili.
Usitake ueleweke ili upendwe, bado utashambuliwa.

Yesu, Socrates, galileo, Newton, copenicus hawakueleweka ila waliacha alama
 
Sijawahi ona kwa nini sisi watanzania ni Watu wenye wivu sana,

Wakikuona una matatizo Kiuchumi watakuhurumia Machoni pao tu ila wakiwa pembeni wanakucheka.

Ukikomaa na kupiga hatua kadhaa za mafanikio, Majungu na Maneno yataanza, mara mchawi, mara mwizi, mara Jambazi, mara fisadi, Huwa wanasahau kabisa ule wakati wako uliokuwa unaangaika na tatizo/Shida zako.

Watanzania sisi ata umchukue mtu mahala pa chini na kumpa msaada/ kazi ya kufanya bado akikuona unafanikiwa lazima akuonee Wivu na kukuombea mabaya.

Huu Wivu huwa tunatoa wapi? Hatutaki kuona wale tuliowasaidia kuwa juu zaidi yetu,
Hatutaki kuona wale waliotusaidia kuendelea kuwa juu zaidi ya sisi tuliosaidiwa kwa nini?.

Wivu ndio unafanya tusiendeleee,Ni wivu tu hakuna kingine,
Jirani ana wivu, Ndugu ana wivu, Rafiki wana wivu, kila sehemu ni Wivu maendeleo tutayapata wapi?

Jana uliniona mimi zero IQ nauza mishikaki ukawa unapita na kunipa moyo ili nizidi kupambana, leo nimedunduliza kahela kangu na kufungua kibanda cha kiepe unapita huku umenuna kuona vile nimepiga hatua moja mbele kukuzidi wewe.

Wivu wote huo unatoka wapi, Kwa nini tusishindane kwenye Wivu wa maendeleo,
Leo mimi nimefungua duka la reja reja, wewe kesho fungua Duka la vitu vya Jumla,

Leo mimi nimenunua piki piki ya kutembelea, wewe kesho nunua IST yako, Tushindane kwenye Wivu wa vitu ili tufanye Maendeleo. Tusishindane kwenye Wivu wa kurudishana Nyuma.

Cc Zero IQ

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakaribia kukubaliana na wewe. Wivu ni DHAMBI mbele za Mungu ,hivyo wengi wanaishi katika dhambi hiyo na Mungu hawezi kuachilia baraka zake.Ndio maana wengi hulia vyuma vimekaza
 
Hii kitu ni shida na inawatafuna wengi, ukiwa na roho ya wivu na unafikiunafiki hutakaa utoboe na hata ukitoboa utatoboa kwa shida sanaa.
Kuna mtu alishaleta uzi huku alimsaidia jamaa hadi akapata kazi nchi za n'gambo Ila haikupita muda jamaa akaenda kumchomea kwa boss wao jamaa akafukuzwa kazi akarudishwa bongo, na alijiapiza kutokumsaidia yeyote yule maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom