Watanzania ndivyo tulivyo

KXY

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
880
327
Nawasalimu wana jukwaa!

Nchi yetu ya Tanzania siyo ndogo kwa eneo wala idadi ya watu, napotumia neno watanzania kama ilivyo mazoea (japo si sahihi) ninaangazia zaidi wale walionizunguka. Kwangu watanzania ni ndugu zangu, majirani, niliosoma nao na ninaoendelea kukutana nao katika shughuli za kila siku. Inawezekana haupo kwenye makundi hayo, kama ndivyo nisamehe kwa kukuunganisha katika mada hii.

Ndivyo tulivyo;
1. Tunapenda mazingaombwe
Sijui ni wangapi kati yetu tumewahi kuomba hela nyumbani tukiwa wadogo ili tuangalie mazingaombwe, nafikiri hili bado linaathari kwetu mpaka leo.
Mifano hai ni hii
  • Siasa - Viongozi wanaowajibika na kuweka mipango ya muda mrefu na kuwa wafuatiliaji hawapendwi na hawadumu. Tunapenda viongozi wafanya mazingaombwe wale wa nitawafanyia hiki na kile, nitaongea na huyu na yule mambo yetu yatakuwa safi. Tunataka kuvuna bila kupanda
  • Michezo - Tunafahamu fika kwamba tuna wachezaji wachache sana wenye sifa za kimataifa, mfano kwa mpira wa miguu hatujafanikiwa kuwa na watanzania hata wawili tu kwenye ligi kubwa duniani kwa sasa. Cha kushangaza inapofika muda wa kuwania nafasi za kushiriki mashindano makubwa matumaini yetu pia yanakuwa makubwa. Tunataka kuvuna bila kupanda
  • Imani - Mpaka kufikia utu uzima mtu aliyelelewa kiimani kwa imani yake, amesoma maandiko ya kumjenga kiimani bado hana hiyo imani. Akitokea mwana mazingaombwe akamfunulia siri za utajiri na mafanikio anasahu yote na kuwa mfuasi wa huyo ili naye apate hayo mafanikio. Tunataka kuvuna bila kupanda
2. Tunaamini katika pande mbili tu
Watanzania tumezoea na kuchukulia kama sheria kwamba shilingi haiwezi kusimama, lazima ianguke na ikianguka pande zake ni mbili tu. Naomba nitoe mifano michache pia hapa.
  • Siasa - Kitaifa tuna chama tawala na vyama vya upinzani, pande mbili. Tumezoea hivyo tuna pande mbili hatuna sera za kutenganisha vyama kwamba chama A na Y ni mlengo wa kushoto, C na F ni mlengo wa kati na kadhalika. Kama unataka usiwe mtanzania sema huna upande, watanzania tunatambua pande mbili tu hivyo hautakuwa mwenzetu.
  • Michezo - Nikirudia mfano wa mchezo wa soka, kitaifa tuna timu mbili na zilizobaki zote zitatafutiwa upande na kuitwa tawi la moja ya hizo timu mbili. Wewe wekeza unavyojua, leta wachezaji toka Amerika ya Kusini lakini timu zitabaki mbili.
  • Imani - Hapa japo pagumu lakini watanzania hawapati shida wao wanatambua dini mbili tu. Ukiwa tofauti japo ni mambo ya kiimani watanzania hawatakuelewa lazima utaitwa majina mabaya.
3. Hatupendi kusoma
Kwa kutambua hilo nitaishia hapa kwa sasa.

Ahsanteni.
 
Kwa kutambua hilo nitaishia hapa kwa sasa.
Aiseee! Nashauri nchi ifanywe kuwa jimbo la Urusi, maana huko over 90% ni well-educated.

^A large percentage of the Russian population has traditionally attained at least an upper secondary education. The figures remained high in 2011: 94% of 25-64 year-olds hold at least an upper secondary qualification. By contrast, the OECD average is 75%, while the average for G20 countries is 60%.^
 
Back
Top Bottom